Friday, September 11, 2015

HABARI - SEPT.11.2015| STAR TV

HABARI - SEPT.11.2015| CHANNEL TEN

KUTOKA FACEBOOKMvua yasimamisha mechi za US Open


Michuano ya US Open kwa upande wa kinadada imesimamishwa kwa muda baada ya mvua kali kunyesha hali iliyosababisha ugumu wa mchezo huo. Serena Williams atapaswa kusubiri mpaka ijumaa ya leo kuendelea na ratiba ya kalenda ya Grand slam ya nusu fainali kwa wanawake ambapo atacheza dhidi ya Roberta Vinci. Hali hiyo ya mvua haikuzuia mchezo wa wanaume na uliendelea kama ulivyopangwa ambapo matumaini ya bara la Afrika kuendelea kuwepo katika michuano hiyo yalifikia tamati baada ya Kevin Anderson wa Afrika Kusini kushindwa kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali kwa kufungwa na Stan Wawrinka seti 6-4 6-4 6-0.
Nusu kwa wanaume  fainali itakuwa:
Roger Federer vs Stan Wawrinka.
Novak Djokovic vs Marin Cilic.

Kwa hisani ya BBCSWAHILI

Wednesday, July 15, 2015

MWADUI KUTIMKIA AFRIKA KUSINI KUJIFUA

Kikosi cha Mwadui FC


Kocha wa timu ya Mwadui FC ya Shinyanga Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amesema wanatarajia kuuomba uogozi wa matajiri hao wa kanda ya ziwa kukiwezesha kikosi hicho kwenda nchini Afrika Kusini kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa 2015-2016 ambapo wao watashiriki ligi hiyo.
“Tunashukuru Mungu timu yetu imeanza ‘pre-season’ vizuri tukiwa na wachezaji wetu wote wapya tuliowasajili pamoja na walioipandisha timu hii, pre-season inaendelea vizuri tena sana kama tutaendelea hivi basi naamini tutakujakuwa washindani kama ilivyokuwa Kajumulo enzi za uhai wake”, amesema Julio, kocha mkuu wa Mwadui FC.
“Sunday Kayuni yeye ni ‘consultant’ kwahiyo amekuja huku kwa kazi hiyo na yeye anatoa ushauri wa hapa na pale lakini tunafanya kazi kubwa kusema kweli tunafurahia uwepo wake kwasababu yeye anaupeo mkubwa, kwahiyo tunaamini katika huo u-consultant wake atatusaidia kwa namna moja au nyingine”, ameeleza.
“Tumeuomba uongozi ili tuone kama tunaweza kupata safari ya South Africa maana sisi (Mwadui Mining) kule ndio makao makuu yetu ili tuweze kuendelea na pre-season kidogo kuimalizia na baadae kupata mechi za kirafiki ambazo zitatuweka pazuri”, ameongeza.

 “Mbeya City walifanya vizuri kwasababu wako nje ya Dar es Salaam, Dar es Salaam kuna vishawishi vingi sana lakini unapokuwa sehemu kama Mbeya, kule unafanya mazoezi magumu ambayo yanaingia ndani ya mwili, kwahiyo sisi hapa kwetu Mwadui ni sehem nzuri tupo mgodini tuna uwanja mzuri ambao nafikiri katika Tanzania ni uwanja wa pili baada ya uwanja wa Taifa”, alimaliza Julio.

Source:http://shaffihdauda.co.tz/

BAADA YA SIKU MOJA YA SEMINA, UTAONDOKA UKIWA NA UHAKIKA WA KWENDA KUSHINDA KWENYE BIASHARA NA UWEKEZAJI NA KUINUKA KIMAISHA!


Saturday, July 11, 2015

KITUO CHA POLISI BUNJU A CHACHOMWA MOTO

Wananchi wenye hasira waishio maeneo ya Bunju A wamechukua hatua hiyo ya kukichoma kituo hicho kidogo cha Polisi baada ya Gari kumgonga mtoto wa shule ya Msingi ya Bunju A na kufa hapo hapo.

Baada ya tukio hilo la kugongwa mtoto huyo,wanafuzi walikusanyika na kufunga barabara hiyo ya bagamoyo kwa kuishinikiza Tanroad kuweka matuta katika eneo hilo.Baada ya Muda si mrefu wananchi wa eneo hilo wenye hasira kali walichukua hatua hiyo ya kukivamia kituo hicho kilicho maeneo hayo na kuanza kukichoma moto na baadae Jeshi la Polisi kufika na kuwatanyisha wananchi hao.

Baadhi ya wanachi wamekamatwa kuhusiana na tukio hiloMAKADA WA CCM WAJITENGA NA MAAMUZI YA KIKAO

Wajumbe wa kamati kuu ya CCM hajakubaliana na maamuzi yaliyotoka kwenye kikao kilichofanyika jana usiku kuwateua wagombea wa nafasi ya Urais kupitia CCM kwa kutofuata katiba ,wanasema kikao hakikupokea majina yote, kililetewa majina machache yaliyojadiliwa na kamati ya maadili,Pia anasema katiba inataka mtu anayekubalika ndiye apewe nafasi lakini kikao kiliminya wanaokubalika kwa maslahi ya wasiokubalika haya yalisemwa na Mh.Nchimbi mbele ya waandishi wa habari,kwa sababu hiyo wajumbe hao wa kamati kuu ambao ni mh.Kimbisa,mh Sofia Simba na Mh.Nchimbi,wamejitenga na maamuzi ya kikao hicho na kutoyaunga mkono


Friday, July 10, 2015

MKUTANO WA WADHAMINI WA NDONDO CUP NA VIONGOZI MBALIMBALI NA MAKABIDHIANO YA VIFAA VYA MICHEZO

Ugiriki yatoa mapendekezo mapya kwa wakopeshaji wake

 Viongozi wa Ugiriki wametuma mapendekezo ya mageuzi ili kupata makubaliano na wakopeshaji wake na kukomesha mgogoro unaoendelea.
Viongozi hao wamepania hasa kuongeza VAT na mageuzi ya pensheni. Mapendekezo ambayo, dhidi ya matatizo yote, hayaonekani kuwa tofauti sana na kile kilichokuwa kinatakiwa na wakopeshaji wa Athens, ambao wanapaswa kuyajadili leo Ijumaa asubuhi.
Ugiriki hatimaye imetuma mapendekezo yake kwa ajili ya mageuzi kabla ya kutamatika kwa muda wa mwisho uliyowekwa na viongozi wa Ulaya. Mapendekezo hayo yanapaswa kufuata mkondo wa masharti yaliyopendekezwa na wakopeshaji wa wake.
Serikali ya Ugiriki imejikubalisha kuongeza VAT kwa asilimia 23 kwa ajili ya chakula na asilimia 13 kwa ajili ya hoteli. Serikali ya Ugiriki pia imepania kufuta au kusamehe polepole VAT zinazotozwa katika visiwa vya Ugiriki.
Ugiriki pia imepania kuongeza kodi katika makampuni makubwa na mashrika mengine yasiyo ya kiserikali. Kodi kwa bidhaa za anasa na matangazo ya biashara kwenye televisheni itawekwa mara moja. Bajeti takatifu katika sekta ya ulinzi itapunguzwa Euro milioni 300 na ubinafsishaji uliosimamishwa baada ya Alexis Tsipras kuchukua hatamu ya uongozi wa nchi, utarejeshwa.
Mageuzi mapya ya pensheni pia yanatazamiwa pia kufanyika. Umri wa miaka 67 unapaswa kuwa kigezo cha kukatisha tamaa ya kustaafu mapema pamoja na kufuta au kusamehe polepole posho ya mshikamano (EKAS).
Kulingana na nakala ya mapendekezo iliyotolewa na serikali ya Ugiriki, Ugiriki inataka suluhisho " ili kurekebisha" madeni yake makubwa, kwa asilimia 180 ya Pato la Taifa, pamoja na "pakiti ya Euro bilioni 35" iliyotengwa kwa ukuaji. Serikali ya Ugiriki imesema pia iko mbioni kutafuta fedha kwa jumla ya Euro bilioni 53.5 ifikapo mwishoni mwa mwezi Juni mwaka 2018 ili kufidia majukumu yake yanayohusiana na malipo yake ya mkopo.

Alshabab lawaachilia wanajeshi 2 wa Kenya

Polisi nchini Kenya wanasema kuwa maafisa wawili wa jeshi la Kenya waliotekwa na wanamgambo ya AL Shabaab yapata miaka miwili iliyopita wameachiliwa huru.
Mkuu wa polisi Joseph Boinnet amesema kuwa wanajeshi hao walikuwa wanahamishwa hamishwa upande wa Somalia kutoka kambi moja ya Al shabaab hadi nyingine.

Hakutoa maelezo zaidi juu ya namna walivyoachiliwa lakini amesema kuwa wako katika hali nzuri ya afya.

MESSI SINGANO AMWAGA WINO AZAM FC

Mchezaji wa zamani wa Simba Messi Singano,amesajiliwa na Timu ya Azam FC kwa mkataba wa miaka 2.
Hii inaonyesha kuwa Messi alikuwa amepania kujiunga na timu hiyo ya Azam FC baada ya kumalizana na Simba iliyomkuza.
Messi akisaini mkataba huo mbele ya viongozi wa Azam FC

Uzi mpya atakaotinga Messi akiwa na Azam FC


Wednesday, July 8, 2015


MAYWEATHER UVULIWA MKANDA WA UBINGWA

Hatua za kuvuliwa mkanda huo wa ubingwa wa WBO,uzito wa Welterweight unaohusisha kilo 67 na 77 ambao alishinda mwezi mei mwaka huu dhidi ya Manny Pacquiao kutokana na kushindwa kufuata sheria na kanuni za Shirikisho holo.
Kamati ya Mashindanoya WBO imesema kwamba haina jinsi ya kufanya zaidi ya kumvua mkanda huo Mayweather ambaye ameshindwa kulipa ada kutoka kwenye pambano alilopigana na Pacquiao.
Siku ya Ijumaa iliyopita ndio ilikuwa mwisho kwa Mayweather kutimiza vigezo hivo vya ubingwa wa WBO ikiwemo kulipa ada ya dola 200,000 kutoka katika pambano lake na Pacquiao pamoja na kujivua ubingwa wa uzito wa lightmiddleweight wa WBCna WBA 

Biotech factory for ant-malaria larvae launched in Tanzania

ZOEZI LA UANDIKISHWAJI DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA LAPIGA HODI MKOA WA PWANI

Jumla ya watu 11,248,194 wamekwishwa andikikishwa kwenye Daftari la kudumu la wapiga kura zoezi ambalo bado linaendelea kwa sasa nchini likiwa limepiga hodi mkoani Pwani.
Haya yalisemwa na Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi ya Taifa Ndg.Damiani Lubuva kijijini Msoga kata ya Msoga wilayani Bagamoyo mbele ya Mh.Raisi Dk.Jakaya Kikwete mara baada ya kujiandikisha.
Bw.Lubuva alisema kuwa lengo la Tume ni kuandikisha Watanzania Milioni 21 hadi23 kote nchinimara zoezi hilo litakapofikia tamati kati ya mwezi Julai na Agosti mwanzoni kama hakutatokea matatizo  
Anasema changamoto zilizojitokeza ni za kawaida hasa kutokana na mfumo huo kuwa ni mpya hivyo lazima kuwe na changamoto kama ilivyo kwenye jambo lolote jipya lazima liwe na changamoto zake
Mkoa wa Pwani unajumla ya vituo 1,752 vya kujiandikisha na mashine 932 ambapo kata ya Msoga kuna jumla ya vituo 17.Zoezi hilo lilianza jana na litamalizika Julai 20.
Ni fursa kwa wakazi wa Mkoa wa Pwani kujiandikisha katika daftari lakudumu la kupiga kura na kupata nafasi ya kuchagua viongozi wanaowataka katika uchaguzi.
Raisi Akijiandikisha kwenye Mfumo Mpya wa Kielekroniki wa BVR

Raisi akichukuliwa Alama ya Vidole na Afisa Tehama wa Tume

Raisi akipokea kitambulisho chake cha kupiga Kura kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume Bw.LubuvaPicha kwa hisani ya Michuzi Blog

Monday, July 6, 2015

BASIL MRAMBA NA DANIEL YONA WAHUKUMIWA

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam  imewahukumu kwenda jela miaka mitatu aliyekuwa waziri wa fedha wa zamami Basil Mramba na aliyekuwa waziri wa Madini na Nishati wa zamani Daniel Yona baada ya kukutwa na hatia ya uhujumu uchumi na matumizi mabaya ya ofisi na kuisababishia Serikali hasara ya Sh.Bilioni 11.7


USA 5-2 JAPAN KOMBE LA DUNIA LA WANAWAKE