Friday, November 30, 2012

SENEGAL WAPIGWA FAINI

Shirikisho la Soka Barani Afrika limeipiga marufuku Senegal isitumie uwanja wa Leopold Sedar Senghor, Dakar, kwa michuano ya kimataifa kwa kipindi cha mwaka mmoja kama adhabu ya vurugu iliyotokea wakati wa mechi mnamo mwezi Oktoba.
Shirikisho la Kandanda la Senegal pia lilipigwa faini ya dola za Kimarekani 100,000 kwa vurugu zilizofanywa na makundi ya mashabiki baada ya mchuano wa mchujo wa kuwania Kombe la Afrika dhidi ya Ivory Coast.
Sasa itabidi timu hiyo ya Simba wa Teranga  itafute kiwanja kingine kwa ajili ya michuano ya mchujo itakayofanyika mwaka ujao ya Kombe la Dunia 2014. Watacheza na Angola, na Uganda.
Mnamo 2007 Togo iliadhibiwa baada ya mashabiki wao kuzua fujo baada ya kutupwa nje ya mchuano wa Kombe la Afrika la 2008 na wageni Mali.
Iliibidi Togo icheze michuano mitatu iliyofuatia katika kiwanja ambacho kilikuwa hakihusishwi na upande wowote, na ikapigwa marufuku kucheza katika kiwanja cha kimataifa kwa muda wa miezi sita.

JAMAA NI MKALI


SYRIA BILA MAWASILIANO

Huduma za mtandao na simu zilikatika katika mji mkuu wa Damscus pamoja na maeneo ya katikati mwa Syria.
Kumekuwa na mapigano zaidi huko Damascus na karibu na uwanja wa ndege, kati ya vikosi vya serikali na waasi.
Kulikuwa na safari moja tu ya ndege iliyofanikiwa Alhamisi.
Serikali inasema hali hiyo ilisababishwa na waasi, lakini habari zinaeleza kuwa ni serikali ndiyo iliyokatiza mfumo wa mawasiliano ili kuzuia mawasilaino kati ya wapiganaji waasi.

HADHI YA PALESTINA YAPANDA UMOJA WA MATAIFA

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limepiga kura ya  na kupitishwa kuboresha hadhi ya Palestina.Mkutano 193 wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa walipiga kura na kuipa Palestina hadhi ya kuwa mwanachama mwaangalizi, matokeo ambayo yalikuwa sana yanatarajiwa.

ZANZIBAR WAWASHIKA SHATI RWANDA

Zanzibar Heroes jana iliwashika shati Rwanda baada ya kuwafunga 2-1,Zanzibar ndio walioanza kuongoza kufungu mabao yote mawili na baadae Rwanda walirudisha goli 1.Vijana wa Zanzibar walionekana kuwa makini sana katika mchezo huo

Thursday, November 29, 2012

UHURU NA RUTO WAKO HURU

Mahakama Kuu nchini Kenya imewakubalia wanaharakati nchini kenya kufuta kesi iliyokuwa ikiwakabili Makamu Waziri mkuu nchini humo Uhuru Kenyata na Mbunge wa Eldorate William Ruto

MUHIMBILI YAANZISHA HUDUMA MPYA


Hospitali ya Taifa ya Muhimbili imeanzisha huduma mpya kwa watoto wanaozaliwa kabla ya muda.
Huduma hii ina miezi minne tu sasa tangu ianzishwe hospitalini hapo na inaitwa kangaroo.Huduma hii inamuezesha mtoto aliyezaliwa kabla ya muda kuweza kupata joto analostahili.Huduma hii hutumika kwa mama kufungwa mtoto kwa kitambaa maalum kwenye tumbo lake mfano wa mnyama Kangaroo

KUNDI LA AL-QAEDA YAITAKA MALI KUKATAA ASKARI WA KIGENI

Kamanda wa juu wa vikosi vya Al-Qaeda Kaskazini mwa Afrika amewataka Wananchi wa Mali kukataa kuingiliwa kati na wageni kama njia ya kutatia mgogoro wa nchi hiyo.
Amesema mgogoro huo unaweza kutatuliwa ndani kwa njia ya Maridhiano baina ya Waislamu bila kumwaga tone la damu
Vikundi mbalimabli baadhi vikiwa na uhusiano na Al-Qaeda vimekuwa vikipigana kudhibiti upande wa Kaskazini kwa muda wa miezi nane baada ya jeshi kuipindua serikali mwezi Machi

TANZANIA YALALA 1-0

Jana Tanzania ilijitupa uwanjani kupambana na Burundi,katika mchezo wake wa pili Tanzania ilipoteza mchezo huo baada ya kufungungwa bao 1 kwa njia ya Penati iliyopatikana Dk 50 ya mchezo baada ya mshambuliaji wa Burundi Suleiman Ndikumana kukwatuliwa eneo la hatari na beki Shaban Kapombe.Penati hiyo ilipigwa na Ndikumana na kufunga ikiwa ni goli lake la 4 katika mashindano hayo ya Tusker Challenge Cup yakifanyika nchini Uganda.Leo Zanzibar inajitupa uwanjani kuivaa Rwanda

WAASI WA M23 WAANZA KUNDOKA GOMA

Hatimaye Waasi wa Kikundi cha M23 wameamua kuachia mji wa Goma na kwenda kujikusanya katika mji wa Sake nje kidogo ya Goma.Msemaji wa kundi hilio amesema wanjesh wa M23 wataondoka Goma hatua kwa hatua.hatua hii imekuja baada ya juhudi za Mataifa jirani na Kimataifa

Wednesday, November 28, 2012

ONA HII


RAIS MISRI APINGWA NA WANANCHI





Waandamaji nchini Misri wamekesha katika viwanja vya Tahrir wakimpinga Rais

Morsi kwa hatua yake ya kujilimbikizia madaraka.Maeneo mengine nchini humo wanandamanaji wamejikusanya kupinga hatua hiyo ya Raisi Mursi.Wanadamanaji hao walikesha wakiimba nyimbo mbalimbali za kumlaani Raisi
Morsi

TANZANIA KIVAA BURUNDI

Baada ya Ushindi wao wa kwanza,Leo Tanzania inaingia tena uwanjani kuivaa Burundi