Tuesday, December 4, 2012

RAILA NA KALONZO WAUNGANA



Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga, kupitia chama chake ODM wametia saini makubaliano ya kuunda muungano wa kisiasa na Makamo wa Rais Kalonzo Musyoka ikiwa ni maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa taifa hilo wa Machi mwakani.
Huu utakuwa muungano wa pili kabla ya tarehe ya mwisho (04-12-2012) iliyowekwa na msajiri wa vyama vya siasa iliyotaka vyama hivyo viwe vimekamilisha taratibu za kisheria za muungano wa vya muungano wao katika siku tisini.Hii ni baada ya kushuhudia muungano mwingine kati ya Uhuru Kenyatta na William Ruto mapema wiki hii.

No comments:

Post a Comment