Thursday, January 24, 2013

DHAMANA YA LULU YAPIGWA KALENDA

MAHAKAMA Kuu kanda ya  Dar es Salaam imebadilisha siku ya kusilizwa kwa maombi ya dhamana ya Mwigizaji nyota wa filamu nchini, Elizabeth Michael, maarufu kwa jina la Lulu,kutoka  Ijumaa ya kesho hadi Juma tatu ya January 28 mwaka huu.
 Lulu anashtakiwa kwa kosa la kumuua aliyekuwa msanii mwenzake wa fani hiyo, Steven Kanumba, bila kukusudia.
Taarifa za ndani kutoka Mahakamani hapo zilizolifikia tovuti ya Habarimpya.com na kudhibitishwa na vyanzo vya ndani kutoka Mahakamani hiyo zimedai kwamba msanii huyo anaweza kupata dhamana hiyo na kurudi uraiani huku akipangia tarehe nyingine ya kuwasilini Mahakamani hapo kwa ajili ya kesi hiyo.
Awali Lulu alikuwa akikabiliwa na kosa la kuua kwa kukusudia, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, lakini baada ya upelelezi kukamilika alibadilishiwa mashtaka na kuwa ya kuua bila kukusudia, kisha kesi hiyo ikahamishiwa Mahakakama Kuu.

No comments:

Post a Comment