Wednesday, January 16, 2013

PROFESOR J AZUSHIWA KIFO

Mwanamuziki mkongwe kutoka Tanzania, Profesa Jay amezushiwa kufariki dunia leo... Habari hizo ambazo zimesambaa mtandaoni ikiwa ni zaidi katika mitandao ya jamii zikizusha msanii huyu maarufu na wa siku nyingi kufariki dunia... WHAT???
Hii si mara ya kwanza kwa watu maarufu nchini Tanzania kuzushiwa kufa, hivi karibuni msanii AliKiba pia alizushiwa kufariki dunia kwa ajali ya gari jijini Dar, lakini habari zikaja kuthibitishwa kuwa si kweli....
     Baada ya tuhuma hizi, ambazo hazijaeleweka zilipoanzia, Profesa Jay a.k.a Heavy Weight Mcee alianza kupokea simu mbalimbali kutoka kwa watu wake wa karibu kutaka kuhakikisha ni kweli ama la.
Habari hizi zilimshtua yeye pia na kuamua kuandika kwa watu wake kupitia ukurasa wa twitter kudhihirisha yuko poa na ni mzima kabisa.

No comments:

Post a Comment