Wednesday, January 2, 2013

TRUE SAD STORY


ILIKUWA siku ya furaha…kwanza kukutana na familia yako maeneo ya Tabata…pili kuisikiliza historia yako na mke wako Wastara ilivyokuwa ya kustaajabisha.
Katika mahojiano Wastara alijizuia asitokwe machozi lakini ilishindikana alilia sana na hadi wakati huo hakuamini kama umemuoa akiwa hana mguu mmoja. Ni maajabu sana.
ILIKUWA HIVI. Wastara aligoma katakata kuwa hapandi pikipiki kamwe, ukamlazimisha alipogoma ukamuuliza.
“Unanipenda” akajibu ndio.
“Unaniamini” akajibu ndio.
“Basi utapanda pikipiki kama unaniamini”
Wastara akapanda…..kilichotokea mbele ni ajali mbaya, wewe haukuumia lakini Wastara akaupoteza mguu wake baada ya hospitali kushauri kuwa ukatwe maana hauwezi kuunganika.

Wakati Wastara anakatwa mguu, kidume ukaamua kutafuta mahari, ukamtolea….hata akiwa hajapona vizuri UKATANGAZA ndoa, na mwanamke asiyekuwa na mguu..tena akiwa bado ana kidonda kikubwa. WEWE NI WA AJABU SANA.
Ilifikia kipindi cha kucheka hasahasa ulipokuwa unacheza na Wastara….mchezo wa kumnyang’anya mguu wake wa bandia na kukimbia nao naye anakukimbiza. Ilikuwa inashangaza.
Baada ya mastori mengi ya kusisimua, Wastara akatukaribisha pilau la nguvu……amakweli anajua kukarimu wageni.
Baada ya kushiba sasa tukaungana kupiga picha hii ya ukumbusho,
Waliosimama nyuma: Wastara, Yvonne cherry Monalisa, George Iron mosenya.
Mbele: Sonia, Hayati SAJUKI, na Suzan Lewis NatashA

**Sipendi kukusifia sana angali u marehemu sasa…lakini ulikuwa mchangamfu na upendo wako wa ajabu kwa Wastara….wanao wanaume wachache sana duniani..kumuoa mtu aliyekuwa mzima kabisa kisha akakatika mguu???? Ni ngumu sana.
umeondoka na PENZI la maajabu, PENZI la kusadikika

**MUNGU akulaze mahali unapostahili JUMA KILOWOKO...SAJUKI…Amen.
 


A George Iron mini documentary, 2012

No comments:

Post a Comment