Saturday, March 30, 2013

Shetta Ft Rich Mavoko - Sina Imani Final

AJALI YA KUANGUKA KWA JENGO KATIKA PICHA

Mheshimiwa Raisi akiwasili eneo la tukio

Rais jakaya Mrisho Kikwete akiangali madhara

Mheshimiwa Mbatia akisalimiana na Rais


Umati wa watu pamoja na waokoaji

Raisi akipata maelezo kutoka kwa Kamanda Kova




Picha zote kwa hisani ya Michuzi

Thursday, March 28, 2013

Nelson Mandela back in hospital with lung infection

Wasichana wadogo waongoza kuambukizwa VVU nchini

Ripoti ya viashiria vya Ukimwi nchini katika mwaka 2011/12 imeonyesha kuwa wasichana wenye umri wa kati ya miaka 23 na 24 wameambukizwa virusi vya Ukimwi kwa asilimia 6.6, ikilinganishwa na wavulana wa umri huo ambao ni asilimia 2.8.

Akisoma ripoti hiyo jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania, (Tacaids), Dk Fatuma Mrisho alisema kiwango cha wasichana wa umri huo wenye virusi ni mara mbili zaidi ya wavulana.

Akizindua ripoti hiyo, Rais Jakaya Kikwete alisisitiza Watanzania na sekta zote zinazojihusisha na mapambano dhidi ya Ukimwi, zitilie mkazo umuhimu wa kukomesha unyanyapaa na kuhamasisha upimaji wa hiari.

“Watanzania zaidi ya milioni mbili wamefariki tangu Ukimwi ugundulike miaka 30 iliyopita, tunatakiwa tupambane kwa dhati kabisa,” alisema Rais Kikwete.
Alipongeza ongezeko la idadi ya watu waliopima kwa hiari na kuwataka wanaume kupima badala ya kuwaachia jukumu hilo wanawake.

Rais pia alizitaka taasisi za Ukimwi, kudhibiti kasi ya maambukizi katika miji mikubwa na katika barabara kuu zikiwemo za Chalinze na Njombe.
“Maeneo hayo yanahitaji nguvu zaidi, hata maeneo yenye kiwango kidogo cha maambukizi nayo yasibweteke yanahitaji tahadhari,” alisema.

Kuhusu tohara kwa wanaume, Rais Kikwete alisisitiza zaidi tohara kwa wanaume na kwamba wasiotahiriwa wanaongeza kasi ya maambukizi kwa asilimia 60 na wanaotahiriwa wanapunguza kwa asilimia 60 pia.

Kwa upande wake, Dk Kikwete alisema maambukizi kwa vijana wenye umri mdogo yanatokea wakati vijana hao wana umri wa kati ya miaka 15 na 19 na matokeo yake kuwa wazi katika umri wa miaka 23 na 24. Alisisitiza kuwa matokeo haya ni kama ya sensa na kwamba si kila Mtanzania mwenye umri wa miaka 14 hadi 49 amepimwa.

“Kwa jumla asilimia 2.0 ya wasichana na wavulana wenye umri wa miaka 15 hadi 24 wana maambukizi ya virusu,” alisema. Hata hivyo ripoti hiyo ilionyesha kuwa kasi ya maambukizi kwa Tanzania nzima, imepungua kutoka asilimia 5.8 mwaka 2008 hadi kufikia asilimia 5.1 mwaka 2011/2012.

Utafiti wa kwanza wa aina hii ulifanywa mwaka 2003 -2004 ambapo maambukizi yalikuwa asilimia 7.06.
Utafiti mwingine ulifanyika mwaka 2009-2010 ambapo maambukizi yalishuka toka asilimia 7 hadi asilimia 5.8

Pia, ripoti hiyo ilionyesha kuwa asilimia tisa ya wasichana na 10 ya wavulana wenye umri wa miaka 15 na 24 walianza kujamiiana kwa mara ya kwanza kabla ya kutimiza miaka 15.
Ripoti hiyo ilionyesha kuwa Mkoa wa Njombe una maambukizi ya juu zaidi ya asilimia 14.8 ya maambukizo kuliko mikoa yote Tanzania.

Maeneo ya visiwani yana asilimia ndogo zaidi ya maambukizi ambapo Unguja ilikuwa na asilimia 1.2 na Pemba asilimia 0.5 tu
“Matokeo ya ripoti hii yatatupa mwanya zaidi wa kujua nini kifanyike na wapi nguvu iongezwe katika kupambana na maradhi haya hatari,” alisema Kikwete.

Takwimu za sasa zinaonyesha kuwa maeneo ya mijini yana maambukizi mengi zaidi ambapo kwa wanawake ni asilimia 6.2 na wanaume ni asilimia 3.8
Ripoti hiyo ilionyesha kuwa zaidi ya robo ya Watanzania walioko kwenye ndoa wana maambukizi ya Ukimwi.

Mahakama yabatilishia uamuzi wa rais Misri

 
Mahakama ya rufaa nchini Misri, imeamuru kiongozi mkuu wa mashtaka aliyefutwa kazi na rais Mohammed Morsi kurejeshwa kazini mwezi Novemba.


Mahakama hiyo imefutilia mbali uamuzi wa rais Mosri kumteua mwendesha mkuu wa mashtaka mwingine Talat Ibrahim.
Hatua ya Bwana Morsi kumfuta kazi Abdel Maguid Mahmoud, iliwaudhi sana majaji wakuu walioina kama hatua ya kuhujumu mamlaka yao.
Hii ilikuwa hatua ya kwanza kama hii kutokea baada ya rais Mosri kujiongeza mamlaka makubwa.
Hatua ya rais Morsi iliindolea idara ya mahakama mamlaka yake ya kuweza kubatilisha uamuzi wowote tatanishi alioutoa . Lakini rais Morsi baadaye alibatilisha uamuzi wake baada ya maandamano makubwa kumpinga.
Kiongozi wa mashtaka wa sasa bwana Mahmoud, aliteuliwa na rais wa zamani Hosni Mubarak.
Aidha Talaat Ibrahim naye alitakiwa kudurusu uchunguzi kuhusu vifo vya waandamanaji waliopinga serikali ya Mubarak.
Afisaa mkuu wa serikali aliambia BBC kuwa serikali itakata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama ya juu zaidi nchini Misri.
Bwana Morsi amekabiliwa na matatizo chungu nzima tangu kuchukua mamlaka mwezi Juni mwaka 2012 baada ya uchaguzi wa kwanza kufanyika tangu kuondolewa mamlakani kwa Mubarak.

Shaa - Crazy ( Official Video )

Wednesday, March 27, 2013

Chege Feat. Malaika - Uswazi Take Away (Official video)

PRESS RELEASE: ‘SIRI YA KUUAWA ZITTO YAFICHUKA’-SIO KWELI

‘SIRI YA KUUAWA ZITTO’
Katika gazeti la Mtanzania toleo na. 7269 la Jumatano Machi 27, 2013 kuna habari yenye kichwa chenye maneno ‘ SIRI YA KUUAWA ZITTO YAFICHUKA’ na vichwa vidogo ‘yadaiwa ilipangwa anyweshwe sumu hotelini’ dk. Slaa atajwa kumtuma Saanane kummaliza’. Habari hii imeniletea usumbufu mkubwa kwani ndugu, jamaa, marafiki na wapiga kura wangu, wamejazwa na wasiwasi mkubwa sana kwamba ninaweza kuuwawa. Napenda kusema yafuatayo:
Moja, sijawahi katika maisha yangu yote kukutana na mtu anayeitwa Ben Saanane na hivyo hicho kikao ambacho inasemekana nilikuwa naye na akajaribu kunipa sumu hakijawahi kutokea. Imetajwa Hoteli ya Lunch Time ambayo sio tu sijawahi kufika, pia hata siijui ipo wapi. Haijawahi kutokea mimi kufanya kikao cha pamoja na Ben Saanane, Juliana Shonza na Mtela Mwampamba. Hivyo habari iliyoandikwa ni ya kufikirika na hivyo naomba mwandishi ahakikishe kuwa vyanzo vyake vya habari vimempa habari sahihi.
Pili, Siamini kamwe kuwa Katibu Mkuu wa chama changu anaweza kupanga kuniua maana hana sababu ya kufanya hivyo. Napenda kurudia kusema kwamba mimi ninaamini kuwa kila nafsi itaonja mauti. Kila mtu atakufa. Kama nitakufa kwa kuuwawa na mtu mwingine ndio itakuwa nimeandikiwa hivyo na Mungu. Ndio maana hata siku moja silalamiki kuhusu vitisho vya kuuwawa nk. Kama kuna mtu anafikiria kuwa kumuua Zitto ndio furaha ya maisha yake atakuwa anajidanganya tu maana Zitto anaweza kufa kimwili lakini mawazo, fikra na maono ya Zitto yataishi tu. Siogopi kufa maana maisha niliyoyachagua ndio haya ambayo yamejaa vitisho. Muhimu kwangu ni kufanya kazi zangu kwa bidii, uhodari na uaminifu. Siku zote nitasimamia ukweli bila kujali uchungu wa ukweli huo.
Tatu, nawashauri watu ambao wamehama CHADEMA na kuhamia vyama vingine watumie muda wao kujenga vyama vyao badala ya kila siku kuzungumzia masuala ya chama ambacho wao sio wanachama tena. Kama mtu kaamua kuhama CHADEMA anapoteza haki ya kujadili masuala ya CHADEMA maana kama angekuwa anapenda kuyajadili asingehama. Naonya mtu yeyote ambaye anatumia jina langu ili kufanikisha malengo yake ya kisiasa. CHADEMA sio pango la watesaji wala wauaji. Kama kuna mwanachama wa chama kingine cha siasa anayedhani kuna mtu ndani ya CHADEMA anapanga mipango ovu aende kwenye vyombo vya sheria kumshtaki. Matendo ya mtu mmoja yasifanyiwe propaganda kama ni malengo ya taasisi.
Nne, Nawashauri viongozi wa CHADEMA na hasa wanachama tutumie muda wetu kujenga mshikamano ndani ya chama. Fitna, majungu, uongo, uzandiki nk kamwe havijengi chama. Chama chetu lazima kiwe mfano bora wa kuheshimu demokrasia na haki za binaadamu. Wananchi hawawezi kutoa dola kwa chama chenye mifarakano. Tusiruhusu kugawanywa kwa matakwa ya watu wachache. Tusimamie misingi ya kuanzishwa chama chetu.

Kabwe Zuberi Zitto, Mb
Dar-es-Salaam
Jumatano, Machi 27, 2013

SERGIO GARCIA ACHEZA GOFU MPAKA JUU YA MITI!!

Tuesday, March 26, 2013

Mkasi - SO6E05 with Man Water

CHEKA KIDOGO

Wanajeshi 13 wa SA wauawa CAR

Wanajeshi 13 wa Afrka Kusini waliuawa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati wakati waasi walipouteka mji mkuu, Bangui, Jumapili. Haya yalitangazwa na Rais Jacob Zuma.
Bwana Zuma alisema Afrika Kusini "inajivunia" wanajeshi wake waliopambana na "waasi".
Bwana Zuma alisema wanajeshi wengine 27 walijeruhiwa, na mmoja hajulikani alipo.
"Ni kipindi cha huzuni kwetu sisi… Twajivunia wanajeshi wetu 200 waliopambana na waasi," aliuambia mkutano wa waandishihabari katika mjii mkuu, Pretoria.
Msemaji wa waasi hao, Erick Massi, aliiambia BBC kwamba kiongozi wa Seleka, Michel Djotodia, ambaye ameshajitangaza kuwa rais, anapanga kufanya uchaguzi wa kidemokrasia, lakini hajasema utafanywa lini.

Thursday, March 21, 2013

Rais Obama awasili nchini Israel

Rais Barack Obama amewasili nchini Israel. Hii ni ziara yake ya kwanza kama rais wa Marekani.
Huku akiwasili, waandamanaji walikusanyika na ulinzi kuimarishwa nchini Israel na katika maeneo ya Palestina.
Bwana Obama anategemewa kukutana na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na rais wa Palestina Mahmoud Abbas wakati wa ziara yake ya siku tatu.
Vita nchini Syria na wasiwasi kuhusu nia za Iran za kinyuklia ni kati ya maswala muhimu zungumziwa katika ziara yake hiyo.

Lwakatare aachiwa, kisha akamatwa tena

Mkuu wa Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilfred Lwakatare na mwenzake Joseph Ludovick Rwezaura wamefutiwa mashtaka ya ugaidi yaliyokuwa yanawakabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kuachiwa huru, lakini walipotoka nje ya chumba cha mahakama “wakakamatwa tena”.

Habari kutoka mahakamani Kisutu zinasema kuachiwa kisha kukamatwa tena kwa watuhumiwa hao kunatokana na makosa ya kisheria yaliyofanywa wakati waliposomewa mashtaka kwa mara ya kwanza.

Makosa hayo ni pale washtakiwa walipoulizwa iwapo wanakubali au wanakana makosa yao, hali mahakama ya Kisutu ikiwa haina uwezo wa kusikiliza kesi za ugaidi.

Washtakiwa hao waliachiwa huru jana saa 3.00 asubuhi na Hakimu Mkazi, Emilius Mchauru baada ya Wakili wa Serikali, Prudence Rweyongeza kuwasilisha hati kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), akiiomba mahakama kuwaachia chini ya kifungu cha 91 (1).

Kifungu hicho kinampa mamlaka Mkurugenzi huyo wa Mashtaka kufuta mashtaka pale anapoona hana sababu ya kuendeleza mashtaka ya mtuhumiwa bila hata ya kutoa sababu zilizosababisha kufanya hivyo.

Hakimu Mchauru alikubaliana na hati hiyo na kuwafutia mashtaka washtakiwa hao waliokuwa wanakabiliwa na kesi namba 37 ya mwaka 2013, iliyokuwa na mashtaka manne yanayohusu vitendo vya ugaidi.

Hata hivyo, baada ya mshtakiwa huyo kuachiwa huru na Hakimu Mchauru, alipotoka nje ya chumba cha mahakama, askari ambao walikuwa wamevaa sare na nguo za kiraia walimkamata Lwakatare ambaye aligoma kukamatwa akidai hadi awepo wakili wake.

Baadaye alifika wakili wake, Peter Kibatala hivyo alikubali kuwekwa chini ya ulinzi. Hivyo askari walimchukua na alipofika karibu na mahakama ya wazi, alifungwa pingu na baadaye kwenda kuhifadhiwa ndani ya gari la polisi akiwa chini ya ulinzi mkali.

Ilipofika saa 4:10 asubuhi, Lwakatare na mwenzake, Ludovick walipandishwa tena kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi, Aloyce Katemana na kusomewa kesi mpya PI namba 96 yenye mashtaka manne yanayofanana na yale ya awali ya ugaidi.

Akisoma hati hiyo mpya ya mashtaka, Wakili Rweyongeza alidai kuwa washtakiwa hao walifanya kosa hilo la jinai kinyume na kifungu cha 384 cha sheria ya kanuni ya adhabu, sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho 2002.

Rweyongeza alidai kuwa Desemba 28, mwaka jana katika eneo la King’ong’o, Wilaya ya Kinondoni, washtakiwa hao kwa pamoja walikula njama ya kumdhuru kwa sumu Dennis Msacky ambaye ni Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mwananchi, kinyume na kifungu cha 227 cha sheria ya kanuni ya adhabu.

Wakili huyo wa Serikali katika shtaka la pili alidai kuwa washtakiwa hao kwa pamoja walikula njama ya kufanya kosa la jinai kinyume na kifungu cha sheria cha 24 (2) cha sheria dhidi ya ugaidi sura ya 21 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Alidai kuwa washtakiwa hao, Desemba 28,2012 walishirikiana kupanga njama za kumteka nyara Msacky kinyume na kifungu cha 21 cha sheria inayopinga ugaidi.

Katika shtaka la tatu, wanadaiwa kufanya mkutano wa vitendo vya kigaidi kinyume na kifungu cha 5 (a) cha sheria namba 21 inayopinga ugaidi iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Aliendelea kudai kuwa siku ya tukio, washtakiwa hao walipanga na kushiriki katika mkutano wa kupanga kitendo cha ugaidi cha utekaji nyara dhidi ya Msacky.

Kwa mujibu wa shtaka la nne, Lwakatare anadaiwa kuhamasisha vitendo vya ugaidi.
Aliongeza kudai kuwa siku hiyo ya tukio, Lwakatare akiwa mwenye nyumba, akijua, aliruhusu mkutano kati yake na Ludovick ufanyike katika nyumba yake kwa lengo la kuhamasisha vitendo vya kigaidi dhidi ya Msacky.

Kabla ya kufutwa kwa kesi hiyo, Hakimu Mchauru alitakiwa kutoa uamuzi kama washtakiwa hao watapata dhamana ama la, kutokana na hoja zilizokuwa zimewasilishwa na mawakili wa pande zote mbili.

Hata hivyo, suala hilo halikujadiliwa baada ya Hakimu Katemana kusema kwamba hakuwa na muda wa kulisikiliza kwani alikuwa anawahi kesi nyingine.Kesi hiyo sasa imeahirishwa hadi April 3, mwaka huu na mawakili wa pande zote mbili watapata fursa ya kujadili suala hilo.

Lwakatare anatetewa na mawakili watano, Peter Kibatala, Mabere Marando, Abdallah Safari, Nyaronyo Kicheere na Tundu Lissu.

 
 
Source:Mwananchi

[AUDIO] Brand New: Matonya - Sembule

Monday, March 18, 2013

Mkasi - SO6E04 With Khadija Kopa



Source:Mkasi

Rich Mavoko - One Time (Official Video)

Askari wa Usalama agongwa na kufariki hapo hapo Bamaga!



Ndugu zangu, huyu mama alitusimamisha sisi tupishe msafara, tukaipisha na yeye akakaa pembeni, ulikua msafara wa magari zaidi ya 50 na yalikua speed kubwa tuu zikiwemo na ambulance.


Sasa huyu mama kosa lake pengine ni hili:

Alihisi kuna watu wameunga tela msafara wa jamaa so akawasimamisha mungu saidia alisimamisha gari 2 zilizokua in a very high speed. Bila ya kuangalia nyuma ya zile gari akaanza kuruhusu gari from Shekilango road na hapo ndipo Discovery 4 kama sio 3 ilipofika kwenye mataa ikiwa na speed kama 120 hivi ikashindwa kusimama na kutanua ili isigongane mna magari yanayo-cross from Shekilango.

Jinsi gani ambavyo kifo kinamuita mtu mama yule alikua upande wa TBC badala ya kua upande wa sinza so jamaa alichofanya ni kukwepa madaladala hamadi traffic huyu hapa jamaa akapita. Sasa sisi tulichokua tunakiona sekunde ya kwanza ni kua jamaa kapanda ukingo ya barabara na kusepa, ila baada ya sekunde kumi niligundua kua kuna tukio zaidi ya tulichokiona nikashuka as i was walking ndio nikaona kofia ya traffic akili ikanijia sasa na wala sikutaka kwenda kuona maana wanaotazama waliniashiria kua si kitu kizuri kutazama.

Ila nimejifunza kua maisha haya jamani hatujui lini ni siku yetu, yule mama nina uhakika kabisa hakujua kama angekutwa na lililomkuta.

Binafsi nimechukulia kama fundisho kwangu, sina mtazamo kama wa wachangiaji wengi wa juu yangu

Source:Jamii Forum

[AUDIO] Brand New: Peter Msechu ft. Joh Makini - Kumbe

Friday, March 15, 2013

MH.ZITTO AIBUKA KIDEDEA

Mhe Zitto Kabwe ameibuka kidedea kwenye uchaguzi wa kumtafuta mwenyekiti wa kamati ya hesabu za Serikali (PAC) baada ya kumbwaga Mhe. Cheyo kwa kupata kura 13 kati ya 17.
Zitto awali alikuwa ni mwenyekiti wa POAC, kamati iliyovunjwa siku chache zilizopita na kuunganishwa na kamati ya PAC.


Source:jamii Forum

Utekaji, uuaji watu Tanzania: Nani atafuata baada ya Kibanda?

Hali ya usalama nchini inaonekana kutia shaka wananchi hasa kufuatia mfululizo wa matukio ya watu kutekwa, kuteswa hata kuuawa.
Kwa bahati mbaya ni kwamba kadri siku zinavyokwenda mbele, vitendo vya watu kutekwa vinaonekana kuongezeka, huku hofu kuu ikiwa ni nini kinachosababisha hayo au akina nani hasa walioko nyuma ya vitendo hivyo vinavyoonekana kutishia maisha watu.
Watanzania waliowahi kutekwa
Baadhi ya watu ambao wameuawa katika mazingira yenye utata ama yanayofanana nay a utekaji ni mwanasheria maarufu nchini, Profesa Jwani Mwaikusa. Msomi huyu ambaye alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kitivo cha sheria, aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa nje ya nyumba yake, huku wauaji wakiondoka bila kupora chochote zaidi ya mkoba na makaratasi aliyokuwa nayo.
Profesa anakumbwa kwa mengi, mojawapo ni kwamba alikuwa mmoja wa mawakili walikuwa wakiwatetea washtakiwa wa mauaji ya kimbali  Rwanda. Alikuwa akimtetea mfanyabiashara maarufu nchini Rwanda, Yussuf Munyakazi aliyekuwa akihusishwa na mauaji hayo katika kesi iliyokuwa ikiendelea katika Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR), jijini Arusha.
Aliyekuwa akimtetea afungwa
Hata hivyo ICTR ilimtia hatiani Munyakazi kwa kumfunga miaka 25 kwa maelezo kuwa alihusika kwa namna moja ama nyingine kuendesha mauaji ya kimbari na kuteketeza familia huko Rwanda.

Munyakazi katika mashtaka yake alitakiwa na Serikali ya Rwanda akashtakiwe nchini kwao, lakini alikataa kwa kuhofia kutotendewa haki.Ni jitihada za Profesa Mwaikusa, zilizosababisha kesi yake iendeshwe ICTR Arusha hadi ilipotolewa hukumu.
Wakati hukumu inatolewa, Profesa Mwaikusa alishauawa na watu wasiojulikana, jijini Dar es Salaam, kitendo ambacho kinaonekana kumuumiza Munyakazi, kutokana na ukweli kuwa msomi huyo alikuwa ana uwezo mkubwa katika masuala ya sheria, kiasi cha kufanikisha asipelekwe Rwanda, kama Serikali ya nchi hiyo ilivyotaka.
Mhadhiri huyo  mahiri aliuawa nyumbani kwake barabara ya Makonde eneo la Salasala, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Wakati Mwaikusa akijiandaa kushuka katika gari lake, watu hao walimgongea kioo na kumwamuru kushuka, inaelezwa kuwa Profesa Mwaikusa alisita, ndipo walimpommiminia risasi hadi kufa.
Wakati wamemaliza kumpiga risasi, alitokea mpwae Profesa Mwaikusa, Gwamaka Daudi (25), kwa lengo la kumnusuru, kwa bahati mbaya naye aliuawa kwa kupigwa risasi mgongoni.
Baada ya kuwaua ndugu wawili, watu hao walianza kutoweka, kwa mbele wakaona kikundi cha watu ambalo walilitilia shaka kwamba wanataka kupambana nao, ndipo walipompiga risasi mtu mwingine aliyejulikana kwa jina la John Mtui (45).
Kama hiyo haitoshi matukio mengine zaidi ya watu kutekwa na hata kuuawa yanaonekana kuendelea.

Source:Mwananchi

Katiba mpya Zimbabwe? Kura yafanyika leo

Zimbabwe inapigia kura ya maoni kielelezo cha katiba hii leo, ikiwa ni mara ya kwanza tangu uchaguzi ufanyike nchini humo uliokumbwa na utata mwaka wa 2008.
Hata hivyo malalamiko yametolewa kuwa huenda nchi hio haijajiandaa vilivyo kutokana na ukosefu wa fedha za kutosha na wachunguzi wanadai kuwa wamefungiwa nje ya shughuli hiyo.
Mugabe na Tsvangirai
Lakini kwa mara ya kwanza inaonekana kuwa hakuna kizungumkuti kikubwa katika kura hii. Chama chake rais Robert Mugabe ZANU - PF na kile cha upinzani ambacho sasa kiko katika serikali ya muungano MDC, vyote vinaunga mkono kielelezo hicho cha katiba.
Katiba hiyo inapendekeza kuhifadhiwa nafasi ya rais mwenye nguvu nyingi serikalini na hii inampa rais Mugabe uwezo wa kusalia madarakani kwa miaka kumi zaidi.
Hata hivyo kura hii ya maoni haijawachangamsha sana wananchi wa Zimbabwe huku raia wengi wakionekana kulenga zaidi uchagzui mkuu unaopangwa kufayika miezi chache zijazo.
Katiba mpya inatazamiwa kunyoosha njia ya kufanyika uchaguzi huo mkuu japo kuna wasiwasi kwa machafuko zaidi kutokea nchini humo

Thursday, March 14, 2013

Muziki Gani-Ney wa Mitego ft Diamond





MKUU WA USALAMA CHADEMA AKAMATWA

Dar es Salaam. Mkuu wa Kitengo cha Usalama wa Chadema,Wilfred Lwakatare jana alikamatwa, akahojiwa na kupekuliwa na polisi kwa tuhuma za uchochezi wa uvunjifu wa amani.

Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso aliliambia Mwananchi jana kuwa Lwakatare alikamatwa kutokana na taarifa zilizopatikana kutoka katika video kwenye mitandao ya kijamii zikimuonyesha akiwahamasisha watu kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani au uhalifu. Alipoulizwa mahali na lini alikamatwa Lwakatare, Senso alisema hilo halijalishi, lakini jambo la msingi ni kwamba wako naye kwa ajili ya uchunguzi na hakutaka kuweka bayana ni lini wangemwachia.

Siku nzima ya jana mitandao ilikuwa imetawaliwa na habari ya picha ya video ikimwonyesha Lwakatare akidaiwa kupanga mikakati ya kumteka Mhariri Mtendaji wa Mwananchi, Dennis Msacky. Lwakatare alionekana akitoa maelekezo kwa watu, ambao sura zao hazikuonekana, akiwataka kufuatilia nyendo za Msacky.

Alionyeshwa akiwataka watu hao kumkamata bila ya kumdhuru Msacky, lakini wamtupe mbali kama njia ya kumnyamazisha. Alikuwa anamtuhumu Msacky kama alikuwa anashirikiana na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe ili kukihujumu chama chao.

“Inabidi mfahamu nyendo za mtu huyu, kama anapenda vitu kama kutembea usiku au kinywaji anachokunywa,” alinukuliwa kwenye mtandao huo.

Pia anaonekana kwenye video hiyo akitoa mbinu mbalimbali za namna ya kufanya utekaji nyara.

Wakili wa Lwakatare alonga
Wakati akihojiwa na kupekuliwa, Lwakatare aliongozana na wakili wa kujitegemea, Nyaronyo Kicheere, ambaye alilieleza Mwananchi kuwa mteja wake alichukuliwa kutoka ofisini kwake kwenye Makao Makuu ya Chadema yaliyoko Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Kicheere alidai kuwa hakuwa na uhakika kuwa Lwakatare alikamatwa muda gani ofisini kwake kwani yeye aliitwa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi saa 9.00 alasiri.Mwananchi, hata hivyo, lina taarifa kuwa Lwakatare alikamatwa na askari wanne saa 7.00 mchana na kupelekwa Makao Makuu ya Polisi.

Lwakatare, ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini kupitia CUF na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, alipokamatwa alifuatana na maofisa kadhaa wa Chadema akiwamo Ofisa wa Ulinzi wa chama hicho, Hemed Sabula na Ofisa wa Mawasiliano aliyejulikana kwa jina moja tu la Karungebe.

Alichukuliwa ndani ya gari aina ya Land Cruiser na kupelekwa moja kwa moja Makao Makuu ya Jeshi la Polisi katikati ya jiji la Dar es Salaam.

Mahojiano
Kicheere alisema Lwakatare alihojiwa kwa tuhuma za uchochezi ingawa alidai polisi hawakubainisha ni uchochezi upi.
Mahojiano hayo kwa Lwakatare yaliongozwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Obadia Jonas.
“Lwakatare alihojiwa kuanzia saa 9.00 alasiri hadi 9.55 jioni na tuhuma zilizomkabili ni uchochezi. Ila askari hawakuniambia ni uchochezi upi,” alieleza Kicheere. Alisema kuwa baada ya mahojiano yale waliamriwa kwenda nyumbani kwa Lwakatare kwa ajili ya upekuzi.

Upekuzi
Lwakatare, ambaye anaishi eneo la Kimara King’ong’o jijini Dar es Salaam, alisindikizwa na askari saba walioongozwa na ACP Jonas. Katika msafara huo wa kwenda kupekua nyumbani kwake, maofisa wa Chadema walizuiwa kuongozana naye, isipokuwa mwanasheria wake, Kicheere, ndiye aliruhusiwa kuongozana naye.

“Tunavyoongea na wewe hivi sasa ni kwamba upekuzi unaendelea katika vyumba vya nyumba . Kwa sasa tuko ndani ya chumba chake cha kulala,” alieleza Kicheere.

Kicheere alisema upekuzi huo ulianza saa 10.30 jioni na ulilenga katika kutafuta nyaraka ambazo zingeweza kutumika kama ushahidi wa tuhuma hizo. Alisema kuwa baada ya kumalizika kwa upekuzi kilichokuwa kinatakiwa kufuata ni kuandikisha maelezo katika Kituo cha Kikuu cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.

“Hawa jamaa wanaendelea na upekuzi na hawajapata kitu chochote muda huu tunavyoongea na wewe. Ila tukimaliza tutarudi Kituo Kikuu cha Polisi kwa ajili ya kuandikisha maelezo,” aliongeza Kicheere.

Dk Slaa anena
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema polisi walifika katika ofisi za chama hicho Kinondoni jijini Dar es Salaam na kuomba kuzungumza na Lwakatare.


Source:Mwananchi
 

KIJIWE UGHAIBUNI

Kijiwe 12 from Luke Joe on Vimeo.


By:Dj Luke

[AUDIO] Brand New: Suma Mnazaleti ft. Tunda Man - Tuko Wangapi

PAPA MPYA APATIKANA

Kadinali Jorge Mario Bergoglio wa Argentina amechaguliwa kuwa Papa mpya wa Kanisa Katoliki.
Kadinali Bergoglio anakuwa mtu wa kwanza kutoka Amerika kusini kuchaguliwa kuwa Papa.
Mara tu baada ya kuchaguliwa alichagua jina la Papa Francis I.
Awali moshi mweupe ulishuhudiwa ukifuka kutoka bomba la kutolea moshi katika kanisa la Sistine Chapel na kufuatiwa na kengele kupigwa. Hii ilikuwa ni ishara kwa walimwengu kuwa makadinali ambao walianza mchakato wa kumchagua Papa mpya hatimae walikuwa wamefaulu katika kazi yao.
Kadinali Bergoglio anachukuwa mahali pa Papa Benedict XVI, ambaye alijiuzulu mwezi uliopita akisema hana nguvu na uwezo wa kuendelea kuliongoza Kanisa Katoliki.
Makadinali 115 wamekuwa faraghani tangu siku ya Jumanne alasiri na wakaanza mchakato wao kwa kupiga kura mara nne kwa siku.
Ilikuwa inahitajika kuwa angalau Makadinali 77 yaani theluthi-mbili wangeliweza kumpigia kura mmoja wao ili aweze kutangazwa kuwa Papa mpya.
Na kabla ya mchakato huo kuanza kulikuwa hakuna dalili za kuonyesha nani angelichaguliwa.
Moshi mweupe
Maelfu ya watu kutoka sehemu mbali mbali duniani walikwa wamekusanyika katika ukumbi wa Kanisa la St Peter tangu siku ya Jumanne.
Muda mfupi kabla ya Kadinali Bergoglio kujitokeza , maelfu ya watu walionekana wakikimbia kuelekea ukumbi wa St Peters ili kuweza kumshuhudia Papa mpya akitangazwa

Wednesday, March 13, 2013

Makundi Geita yapatanishwa

Mdau wa Habari na Amani, Eric Shigongo mwishoni mwa wiki aliongoza jitihada za kusuluhisha mgogoro unaofukuta miongoni mwa watu wa Buselesele na Katoro wilayani Geita.
Shigongo akishirikiana na Mbunge wa Busanda-CCM,  Lolesia Bukwimba licha ya kukutanisha makundi yanayosigana pia waliandaa mashindano ya soka ili kuhamasisha amani katika eneo hilo.
Akizungumza na gazeti hili jana, Shigongo alisema kuwa wamefikia hatua kubwa katika utatuzi wao kwani viongozi wa dini hizo walifikia mwafaka na kusaini mkataba wa amani.
Katika vikao hivyo ambavyo viliwashirikisha Mbunge Bukwimba na viongozi wa Serikali Wilaya ya Geita, Mchungaji Isaya Ikiri na Sheikh Ismail Ibrahim waliwekeana saini ya makubaliano ya amani.
Shigongo alisema kuwa kati ya makubaliano waliyofikia pande hizo mbili ni kuwa Waislamu kuendelea kuchinja, lakini Wakristo wanaweza kuchinja lakini nyama yao isiingie katika biashara ya bucha.
“Pia pande zote mbili zimetakiwa kuwa makini, kwamba atakayekiuka makubaliano hayo kachukuliwe hatua za kisheria kama mtu binafsi na sio dini ihusishwe,” aliongeza Shigongo.sio dini Sheikh Ibrahim, ambaye yuko katika msikiti wa Katoro, aliithibitishia gazeti hili juu ya mwafaka huo

Tuesday, March 12, 2013

Solo Thang Ft Godzilla - Uwezo Mia Mia [ Official Video ]

Juba, Khartoum zasaini mkataba wa mafuta

Salva Kiir, Sudan Kusini na Omar Bashir, Sudan.
Serikali za Sudan na Sudan kusini zimesaini mkataba mpya wa kurejelea uchimbaji na usafirishaji wa mafuta kutoka Sudan Kusini kupitia mabomba ya Khartoum.
Mkataba huu unakomesha mzozo uliokuwa kati ya nchi hizo mbili kwa muda wa mwaka mzima. Serikali ya Juba ilikatiza uchimbaji mafuta Januari mwaka uliopita kufutia mtafaruku juu ya ada zinazotozwa.
Waziri wa habari wa Sudan ya kusini Barnaba Marila Benjamin, ameambia BBC kuwa nchi hizo zimeafikiana na kusaini mkataba juu ya ugawaji wa fedha za mafuta kufuatia upatanishi ulioongozwa na rais wa zamani wa Afrika Kusini Thabo Mbeki.
Nchi hizo mbili zilitishia kuingia vitani kutokana na mvutano hasa juu ya mafuta na mipaka tangu Sudan ya Kusini ijitenge kuwa huru mwaka wa 2011.

Wamiliki tv watishia kuzima mitambo



Dar es Salaam. Wamiliki wa vituo vya utangazaji vya televisheni nchini, wamesema watasitisha kurusha matangazo ndani ya mwezi mmoja kuanzia sasa kutokana na kushindwa kumudu gharama za uendeshaji.

Hatua hiyo inatokana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuzima mitambo ya analojia na kuhamia dijitali Desemba 31, mwaka jana kitendo walichodai kimepunguza mapato yanayotokana na matangazo.

Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (Moat), Reginald Mengi alisema hakuna haja ya kurusha matangazo kwa hasara.
Mengi alisema kutokana na kuanza kwa mfumo wa dijitali, watangazaji wamesitisha kutoa matangazo kwa sababu wananchi wengi hawana ving’amuzi.

“Kama mamlaka itashindwa kurudisha ule mfumo wa analojia kuwa sambamba na dijitali hadi wananchi watakapokuwa na ving’amuzi, tutazima televisheni zetu ndani ya mwezi mmoja ujao,” alisema Mengi.

“Ibara ya 18 ya Katiba imekiukwa kutokana na wananchi kunyimwa fursa ya kupata habari, hivyo hali hii hatutaki iendelee,” alisema Mengi.

Mengi ambaye pia ni mmiliki wa vituo vya televisheni vya ITV, EATV na Capital TV, alisema licha ya nchi za Afrika, Tanzania imekuwa ya kwanza kuzima mitambo ilhali wananchi hawakuwezeshwa kumudu gharama za ving’amuzi.

“Nchi ambazo zimeendelea kwa kila kitu kama Uingereza, Marekani, Japan na kwingineko kuzima mitambo ya analojia walitumia zaidi ya miaka minane kwa nini sisi tumewahi hivi wakati hatujajipanga?” alihoji Mengi.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Sahara Media Group na mmiliki wa Kituo cha Star Tv, Samwel Nyalla alisema hivi sasa wanaendesha biashara hiyo kwa hasara.

Nyalla alisema hadi mwaka 2015, hali itakuwa mbaya kutokana na kukosa ving’amuzi.
Mkurugenzi wa Utangazaji wa TCRA, Habby Gunze alisema wao hawakualikwa katika mkutano huo hivyo hawajui chochote. Gunze alimtaka mwandishi kwenda ofisini leo.

“Sisi hatujui chochote na kama unataka maelezo mengine njoo kesho (leo) ofisini kwetu uonane na Mkurugenzi Mkuu (Profesa John Nkoma), ili tuzungumze kwa ‘fact’ (kwa ushahidi) kipi kinachoendelea,” alisema Gunze.

Nukuu
“Kama mamlaka itashindwa kurudisha ule mfumo wa analojia kuwa sambamba na dijitali hadi pale wananchi watakapokuwa na ving’amuzi tutazima televisheni zetu ndani ya mwezi mmoja ujao labda TBC ndiyo itakayobaki”.


Source:Mwananchi

Monday, March 11, 2013

ICC yatupilia mbali kesi dhidi ya Muthaura

Mahakama ya kimataifa ya ICC inatupilia mbali kesi ya uhalifu dhidi ya binadamu iliyokuwa inamkabili aliyekuwa mkuu wa utumishi wa umma nchini Kenya Francis Muthaura.
Hii ni baada ya shahidi mkuu katika kesi hiyo kusema alitoa ushahidi wa uongo.
Muthaura alihusishwa na ghasia za baada ya uchaguzi Kenya mwaka 2007 kwa kuwa mmoja wa wale waliopanga na kufadhili mashambulizi ya uklipza kisasi dhidi ya jamii moja.
Kiongozi wa mashtaka, Fatou Bensouda alisema anafutilia mbali mashtaka yote dhidi ya Francis Muthaura ambaye anatuhumiwa kwa uhalifu ikiwemo mauaji na ubakaji baada ya kutokea dosari katika ushahidi.
Wakati huohuo mawakili wa rais mteule wa Kenya Uhuru Kenyatta nao wanatarajia baadaye leo kuwashawishi majaji katika mahakama hiyo kudurusu ushahidi ambao viongozi wa mashtaka walitoa dhidi ya Kenyatta kwa tuhuma kuwa alihusika na ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007
Mawakili wa Kenyatta wanatarajiwa kutoa hoja yao siku mbili baada ya Kenyatta kushinda uchaguzi wa urais , wa kwanza kufanyika tangu ghasia za baada ya mwaka 2007.
Mawakili wanasema majaji wanapaswa kudurusu kesi hiyo hasa baada ya shahidi mmoja kutoa ushahidi wa uongo na hivyo kuhujumu kesi dhidi ya Uhuru na mshukiwa mwingine Francis Muthaura.
Kenyatta alishinda uchaguzi wa wiki jana licha ya kesi anayokabiliwa nayo katika mahakama ya ICC kwa kosa la uhalifu dhidi ya binadamu, ikiwemo mauaji, ubakaji na kuwalazimisha watu kuhama makwao.
Viongozi wa mashtaka wanamtaja kama mmoja wa wahusika katika ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007.
Kenyatta, ambaye ni mtoto wa rais mwanzilishi wa Kenya, Jomo Kenyatta ni mmoja wa watu matajiri wakubwa zaidi barani Afrika na anasisitiza kuwa hana hatia.
Kesi dhidi ya Kenyatta itaanza mwezi Julai

UNAJUA KIPAJI CHA MTOTO WAKO?

Nchimbi atimua mabosi sita polisi, makuruta 95

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi amewafukuza kazi maofisa watano wa Polisi na kumsimamisha kazi kwa mwezi mmoja Kamishna msaidizi Mwandamizi wa jeshi hilo kutokana na makosa mbalimbali.
Pia, Dk Nchimbi amewafukuza makuruta 95 waliokuwa Chuo Cha Polisi (CCP), Moshi kutokana na kugundulika kutumia rushwa kupata ajira.
Kamishna msaidizi Mwandamizi wa Polisi aliyesimamishwa kwa mwezi mmoja ni Renatus Chalamila akihusishwa na rushwa katika kuajiri.
Alisema taarifa za uchunguzi za kamishna huyo, ambaye anashughulikia masuala ya ajira zimewasilishwa kwa Rais Jakaya Kikwete, ambaye ndiye mwenye mamlaka ya kumfukuza kazi.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Dk Nchimbi alisema maofisa watatu kati ya hao watano wamefukuzwa kutokana na kugundulika kuwa walikamata dawa za kulevya aina ya cocaine lakini zilipopelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali alidai zilikuwa ni chumvi na sukari.
“Kama mtakumbuka mkoani Mbeya, Aprili mwaka jana zilikamatwa kilo 1.9 za dawa za kulevya na polisi walithibitisha hilo lakini zilipopelekwa kwa Mkemia Mkuu zikagundulika ni chumvi na sukari,” alisema na kuongeza:
“Niliunda timu kuchunguza kama ni kweli kwa kuwa askari walituthibitishia ni dawa za kulevya, timu ilichunguza na kugundua kilichokamatwa hakikuwa kilichopelekwa kwa Mkemia Mkuu.”
Dk Nchimbi alisema kutokana na hilo, amewafukuza kazi, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Peter Elias ambaye alikuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Mbeya, Mrakibu wa Polisi, Jacob Kiango aliyekuwa Msaidizi wa Mkuu wa Upelelezi mkoani humo na Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Charles Kinyongo aliyekuwa Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia mkoani humo.
“Nimemwagiza kiongozi wa polisi awafungulie mashtaka ya kijeshi askari hawa kwani ajira zao zimesitishwa kuanzia jana (juzi Jumamosi),” alisema Dk Nchimbi.
Alisema ofisa mwingine aliyefukuzwa kazi kuanzia jana ni Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Peter Matagi aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Kagera kwa kuwapiga na kuwabambikizia kesi zisizo na dhamana wananchi.
“Mwaka jana kulikuwa na mgogoro wa ardhi katika Kijiji cha Nyakasimbi huko Kagera kati ya wanakijiji na mmiliki mmoja wa shamba, wananchi waliona kuwa mmiliki wa shamba hilo ana eneo kubwa hivyo walikubaliana katika mkutano wa kijiji kuingia kwenye shamba hilo kwa nguvu,” alisema Dk Nchimbi na kuongeza:
“Waliingia na kuanza kuswaga ng’ombe kuelekea kwa Mkuu wa Wilaya, walikamatwa watu 12 lakini wawili walifanikiwa kutoroka na walisafiri hadi Dodoma kumwona mbunge wao, ambaye aliomba kuonana na mimi.”
Dk Nchimbi alisema licha ya kukubali kuonana nao,  ilishindikana baada ya watu hao kukamatwa wakidaiwa kuwa ni majambazi ambao walikuwa wakitafutwa huko Karagwe.
“Nilimpigia simu Kamanda wa Polisi Kagera nikitaka kuonana na hao majambazi katika Hoteli ya Dodoma na waliletwa na niliwasikiliza na kugundua kuna tatizo la wao kubambikiziwa kesi ya ujambazi wa kutumia silaha ambayo huwa haina dhamana,” alisema.
Alisema aliunda timu ambayo aliiongoza akiwa na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Aggrey Mwanri na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole Medeye na kusimamia uchunguzi na Ofisi ya Mwanasheria wa Serikali iligundua hakuna mashtaka kama hayo na ndiyo maana Matagi anafukuzwa kazi na kushtakiwa kijeshi.

Source:Mwananchi

Mkasi With Millard Ayo

Kamati mpya za Bunge kuanza kazi

Kamati za Kudumu za Bunge zinatarajiwa kuanza  kukutana na kutekeleza majukumu ya Kibunge  jijini Dar es Salaam kuanzia Machi 18, ikiwa ni kipindi cha nusu muhula wa  uhai wa Bunge.
Vikao vya kamati hizo vitaanza mara baada ya kukamilika kwa uundwaji wa Kamati Mpya za Bunge pamoja na uchaguzi wa wenyeviti wa Kamati hizo utakaofanyika Ijumaa ya wiki hii.
Mwishoni mwa mkutano wa 10 wa Bunge mwezi uliopita, Spika wa Bunge, Anne Makinda alitangaza mabadiliko ya kamati hizo, huku akiifuta Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) iliyokuwa ikiongozwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.
Kutokana na mabadiliko hayo, shughuli za POAC sasa zitafanywa na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) ambayo itaendelea na jukumu lake la msingi la kuchambua taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) pia kwa Serikali Kuu.
Kamati nyingine iliyofutwa ni ile ya Sheria Ndogo, huku zikiundwa kamati mpya tatu na kuzifanyia marekebisho nyingine ikiwa ni hatua ya kuimarisha usimamizi wa Bunge kwa shughuli za Serikali.
Katika mchakati huo, kamati mpya zilizoundwa ni Kamati ya Bajeti, Kamati ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ambayo imetenganishwa kutoka katika Kamati ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.  
Kwa mujibu wa Spika Makinda, majukumu ya kamati mpya ya bajeti ni kufuatilia utekelezaji wa bajeti ya Serikali na sera za fedha pamoja na kuainisha na kupendekeza vyanzo vya mapato ya Serikali na kufuatilia mwenendo wa uchumi.
Kamati hiyo ya bajeti pia imepewa jukumu la kushauri kamati nyingine zote kuhusu bajeti.
Taarifa iliyotolewa jana na Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa ya Ofisi ya Bunge iliyolenga kuufahamisha umma juu ya kuanza kwa kamati hizo nyeti za Bunge.
“Baada ya uundwaji wa kamati mpya na uchaguzi wa wenyeviti, litafuatia zoezi la wajumbe wapya wa Kamati hizo kuhudhuria semina maalumu kuhusu majukumu ya Kamati pamoja na kupitia mpango wa kazi (work plan)” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
Taarifa hiyo ilisema ratiba iliyopo inaonyesha kuwa kamati za kisekta zitatembelea na kukagua miradi ya maendeleo iliyokasimiwa na utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2012/13 kuanzia Machi 18 hadi Machi 23 mwaka huu.
“Tarehe 25 mwezi huu, Spika wa Bunge, Anne Makinda alitoa muhtasari kwa wabunge wote kuhusu mkutano wa 11 wa Bunge ikifuatiwa na kupokea Mpango wa Maendeleo kwa mwaka 2013/14 kutoka serikalini pamoja na mwongozo wa matazamio na upeo wa Bajeti ya 2013/14,” iliongeza taarifa hiyo.
Taarifa hiyo ilisema kuanzia  Machi 26 hadi Aprili 5, Kamati za kisekta zitafikiria na  kuchambua maombi mapya ya fedha kwa Bajeti ya Wizara zilizo chini yake kwa mwaka wa fedha 2013/14 ikifuatiwa na Serikali kufanya majumuisho kwa kuzingatia ushauri wa kamati za kisekta.
Iliongeza taarifa hiyo kuwa baada ya shughuli hizo za kamati, Mkutano wa 11 wa Bunge ambao ni Mkutano wa Bajeti utaanza mjini Dodoma Aprili 9.
“Mzunguko wa Bajeti unakusudiwa kukamilika kabla ya tarehe 30 Juni, 2013 ili kuipa Serikali muda wa kutosha kutekeleza majukumu yake,” ilibainisha taarifa hiyo.

Source:Mwananchi

Saturday, March 9, 2013

Matukio baada ya kutangazwa mshindi Kenya



Matokeo ya mapema ya uchaguzi wa urais nchini Kenya yanaonyesha Uhuru Kenyatta ameshinda na kuepuka raundi ya pili ya uchaguzi.
Lakini tume ya uchaguzi itakagua hesabu hiyo kabla ya kutangaza matokeo baadaye leo jumamosi, siku tano baada ya wakenya kupiga kura. Uhuru amepata asilimia hamsini nukta sufuri tatu na kuzuia kutokea kwa duru ya pili ya uchaguzi.
Matokeo yaliyotolewa na tume ya uchaguzi yanaonyesha kuwa Uhuru alipata kura 6,173,433 huku mpinzani wake Raila Odinga akipata 5,340,546
Hata hivyo tume ya uchaguzi itatangaza matokeo rasmi baadaye leo mwendo wa saa tano asubuhi saa za Afrika Mashariki

Wednesday, March 6, 2013

Rais wa Venezuela Hugo Chavez afariki



Katika taarifa kwa taifa, makamu wa rais wa Venezuela Nicholas Marduro ametangaza kufariki dunia kwa rais Hugo Chavez, 58, kufuatia kuugua muda mrefu maradhi ya Saratani. Rais Chavez ametoweka katika hadhira ya nchi hiyo kwa muda mrefu ambapo alikuwa anapokea matibabu nchi jirani ya Cuba.
Alirejea , mjini Caracas mnamo Februari 18 kwa mara ya kwanza tangu maradhi yake yamzidie ambapo alipelekwa hospitali ya kijeshi kuendelea kupokea matibau. Hata hivyo maelezo zaidi hayakutolewa juu ya afya yake. Waandamanaji waliandamana katika mji mkuu Caracas mwishoni mwa juma wakidai kuwa watu wa Venezuela wanapaswa kupewa habari zaidi kuhusu afya ya rais wao.
Bwana Chavez amekua uongozini nchini Venezuela kwa miaka 14 na anatazamiwa kuleta mageuzi makubwa yaliyolenga zaidi kuimarisha maisha ya raia wa pato la chini

Monday, March 4, 2013

Mkasi - SO6E02 With Kingwendu

Dar waandaa maandano kumpinga Muingereza aliyekashifu viongozi wa nchi

POLISI katika Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, imetoa masharti ya kuruhusu  maandamano ya amani ya kupinga kauli ya kashfa iliyotolewa na raia mmoja wa Uingereza, dhidi ya viongozi wakuu wa nchi.
Maandamano hayo  yaliyoandaliwa na Asasi isiyokuwa ya Kiserikali ya Human Settlements of Tanzania (Huseta), yamepangwa kufanyika Jumatano na yataanzia Viwanja vya Mnazi Mmoja na kuishia  nje ya Ubalozi wa Uingereza hapa nchini.
 Hata hivyo, Kamanda wa Polisi katika Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema hajapata barua ya kuomba kufanyika kwa maandamano hayo. “Lakini nitaangalia maudhui, kama yanafanana na maandamano husika,” alisema.
 Alisema akifika ofisini leo na kuiona barua ya kuomba kufanyika, maandamano hayo atakuwa katika nafasi nzuri ya kuzungumzia maandamano hayo.
“Nikipata barua ya maandamano hayo na kuona maudhui yake, nitakuwa katika nafasi ya ama kuyaruhusu au kutoyaruhusu,"alisema Kova 
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Huseta, Dagan Kimbwereza, alisema Muingereza huyo (jina linahifadhiwa) amekuwa akitumia mitandao ya kijamii, kuwashfu Rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu Mzengo Pinda.
Mwenyekiti huyo alibainisha kuwa raia huyo wa Uingereza bila ya kuwa na  vithibitisho wa kile anachokisema, amekuwa akikashfu mihimili mingine ikiwamo mahakama,tasnia ya habari na wananchi kwa jumla.
“Baada ya kufika ubalozini  wawakilishi wawili watawasilisha azimio lenye saini za Watanzania wakiitaka Serikali ya Uingereza kutoa tamko hadharani kwamba yenyewe haihusiki wala haisaidii dharau na maovu mengine yanayofanywa na raia wake dhidi ya Taifa la Tanzania,”alisema Kimbwereza.
Kimbwereza akionyesha kwa waandishi moja ya chapisho ambalo mtuhumiwa ameandika katika mitandao ya jamii ni ile inayosema;
Kikwete aitaka PCCB (Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na  Rushwa) kupambana na rushwa hadi katika Baraza la mawaziri,’kundi moja la majambazi linaliambia kundi jingine la majambazi kukamata mwizi” .
“Mahakama za Tanzania zimejaa rushwa na hazina uwezo. Rais ndiye msimamizi wa katiba na yeye ndiye mhusika mkuu wa ukiukwaji wa sheria” inasomeka moja ya hoja alizoziandika Sarah katika mitandao ya kijamii. #

Source:Mwananchi

Mauaji siku ya kupiga kura Kenya

mmoja wa majeruhi



Taarifa ambazo bado hazijathibitishwa zinasema kuwa watu 10, wakiwemo maafisa wa polisi wawili, wameuawa mjini Mombasa, Pwani ya Kenya. Tukio hilo lilitokea alfajiri, kuamkia leo wakenya wanapopiga kura.
Hata hivyo polisi walithibitisha vifo vya maafisa wao wawili vilivyotokea wakati polisi walipowapiga risasi washambulizi waliokuwa wamejihami kwa mapanga. Lilikuwa shambulizi la kulipiza kisasi.
Washambulizi hao wanashukiwa kuwa wafuasi wa kundi la Pwani la Mombasa Republican Army (MRC) ambao wamekuwa wakipigania uhuru wa jimbo la Pwani.
Mwandishi wa BBC, Karen Allen, anasema polisi waliweza kuthibitisha vifo vya wanne katika eneo la Changamwe, naye Hassan Majid aliona mtu mmoja kauawa eneo la Mishomoroni. Mwtu mwingine Moja ya miili hiyo ilikuwa imekatwakatwa.
Zaidi ya watu 1,000 waliuawa miaka mitano iliyopita katika ghasia zilizotokea baada ya uchaguzi wa mwaka 2007.


Source:BBC

Mkasi - SO6E01 With Bi Chau

WAKENYA WAPIGA KURA LEO

wakazi wa kibera wakiwa kwenye foleni wakisubiri kupiga kura

Friday, March 1, 2013

Mauaji ya albino,ukataji viungo vyazidi kutikisa nchi (3)

“Usiku wa manane, kati ya saa saba na saa nane hivi, Nilisikia vishindo vya nyayo vikitokea sebuleni ambako mwanangu Shukuru na Edron walikuwa wamelala. Ghafla nikamwona mume wangu ameshika upanga ananishambulia kichwani. Nikawa nashangaa na kuwaangalia usoni bila kujua kwa nini alikuwa ananishambulia. Akasema, “Nyamaza!”

Ofisa mmoja wa polisi alipendekeza nimwulize Kulwa kama mabaki ya Maganga bado yapo kaburini kwa kuwa halikujengewa kwa nondo na zege.
Nilimshauri awasilishe wazo lake kwa viongozi wake ili waiombe Mahakama ruhusa ya kulifukua kaburi la Maganga na kupata uhakika kama viungo vyake bado vipo au vimeondolewa.
Niliwaacha polisi wakiendelea na uchunguzi wao na mimi nikaanza safari ya kurejea Dar es Salaam.
Nilipokea taarifa za jaribio la kumdhuru mtoto wa miezi saba ambaye ana ulemavu wa ngozi, Makunga Baraka Februari 5, mwaka huu katika Kijiji cha Nyaruhande, Kitongoji cha Nyasubi, Kata ya Nyaruhande, Wilaya ya Busega, Mkoa wa Simiyu. Nilizungumza na mama mzazi wa mtoto huyo, Jane Daudi ambaye aliniambia kuwa alikuwa amehifadhiwa kwa muda katika kituo cha polisi kwa usalama wa mwanae.
“Nilipokea simu kutoka kwa mtu aliyejitambulisha kuwa ni George wa eneo la Ndiko. Akaniambia, “Dada nakuhurumia sana kwa kuwa una mtoto mwenye ulemavu wa ngozi.  Niliwasikia watu hotelini wakipanga njama za kuja kumuua.”  Niliogopa sana na nikamweleza mama yangu. Tukaenda hadi kwa mwenyekiti wa mtaa hatukumkuta. Baadaye tukatoa taarifa kwa wanakijiji.
Hawakutuamini. Hawakutaka kuja kutulinda. Kabla ya saa tatu usiku watu watatu walikuja nyumbani kwetu na kuanza kuturushia mawe dirishani na mlangoni. Wanakijiji wakawaona na wakawafukuza lakini hawakuwakamata. Usiku ule wanakijiji walipeana zamu kutulinda.”
“Kesho yake asubuhi Mwenyekiti wa Mtaa akaniandikia barua kwenda polisi na wanakijiji wakatusindikiza. Polisi wanafuatilia taarifa nilizowapa. Naogopa sana. Nahofia maisha ya mwanangu Makunga. Sitaondoka polisi hadi hapo nitakapopata ulinzi mkali,” anasema Jane.
Maria Chambanenge (39)
Nilipokea taarifa nyingine za kushambuliwa kwa Maria Chamanenge (39) katika Kijiji cha Mkowe, Miangalua, Wilaya ya Sumbawanga Vijijini, Mkoa wa Rukwa.
Nilikwenda kumwona Maria katika Hospitali ya Mkoa ya Sumbawanga. Kulikuwa na ulinzi mkali na tulielezwa kwamba tunapaswa kupata kibali cha polisi ili kumtembelea wodini.
Kamanda wa Mkoa wa Polisi alikuwa safarini kikazi.  Maofisa tuliowakuta walituelekeza kuwa kibali kinapatikana kwa Mganga Mkuu wa Mkoa (RMO).
Tulirejea tena hospitali na baadaye tulionana na Kaimu Mganga Mkuu, alitupa idhini ya kuzungumza na Maria lakini chini ya usimamizi.
Maria alikuwa bado ana maumivu makali, baada ya kukatwa mkono wa kushoto. Madaktari walituhakikishia kwamba hali yake inaendelea vizuri kwa upande wa matibabu. Swali lilikuwa je, kwa upande wa kisaikolojia?
Maria ni albino na haoni vizuri. Sasa ameongezewa ulemavu wa viungo. Huyu ni mama wa watoto wanne: Shukuru (8), Edron (6), Rahab (3) na Emma (miezi mitano). Mama huyu ni mke wa tatu wa Gabriel Yohana. Atawaleaje watoto wake akiwa na mkono mmoja sasa? Atafanyaje kazi za nyumbani na za kilimo bila mkono wa pili?
Baada ya kumjulia hali, nilimwomba anielezee jinsi alivyoshambuliwa na kukatwa mkono wa kushoto usiku wa Februari 11, mwaka huu, chumbani akiwa amelala na wanae.
“Usiku wa manane, kati ya saa saba na saa nane hivi, Nilisikia vishindo vya nyayo vikitokea sebuleni ambako mwanangu Shukuru na Edron walikuwa wamelala. Ghafla nikamwona mume wangu ameshika upanga ananishambulia kichwani. Nikawa nashangaa na kuwaangalia usoni bila kujua kwa nini alikuwa ananishambulia. Akasema, “Nyamaza!” Mimi nikawa nalia. Akasema, Pole!  Nyamaza!”

Source:Mwananchi

[AUDIO]Chidi Beenz ft. Barnaba - Me Nafurahi

FID Q - I AM A PROFESSIONAL