Thursday, February 28, 2013

Gharama ndogo za simu kuongeza masoko na wateja

MKAZI wa jijini Dar es Salaam, Hija Omar analazimika kutumia wastani wa Sh5,000 kwa siku kwa ajili ya mawasiliano ya simu kutokana na kipato chake. Omar anafanya ya kuuza matairi ya pikipiki ya magurudumu matatu.
 Bila kufanya hivyo anaweza kupoteza wateja wake ambao wanategemea chombo hicho kuwafikisha maeneo ya katikati ya Jiji la Dar es Salaam ambako teksi haziwezi kufika kirahisi.
 Omar ana kazi zaidi ya moja na mitandao mitatu tofauti ya simu za mkononi inayomsaidia kuwasiliana na wateja wake.
 “Ninakwepa gharama za kuwasiliana, wateja wangu ambao wapo mitandao  tofauti , siwezi kutumia laini ya voda au Airtel kuwasiliana na mteja wa Tigo.
 “Hata kama mtu ‘akinibipu’ ni rahisi kumpigia hii ndiyo sababu nalazimika kutumia laini zaidi ya mbili,” anasema dereva huyo wa Bajaj.
 Kadhia ya kuwa na laini zaidi ya moja inayomsibu Hija huenda ikamalizika kesho, baada ya Mamlaka ya Mawasiliano nchini (Tcra) kushusha gharama za kupiga simu kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine. Tcra imeshuka gharama za siku kutoka Sh115 mpaka Sh34.92 kwa dakika moja.
 Hii ni habari njema kwa Hija na watumiaji wengine wa simu za mkononi ambao kwa mujibu wa taarifa za Tcra mpaka kufikia Septemba, mwaka jana kulikuwa na watumiaji wanaokadiriwa milioni 23.8 waliosajiliwa sawa na asilimia 93 ya watumiaji wote waliosajiliwa kutoka kampuni saba za simu za mkononi nchini.
Tcra ilifanya mabadiliko hayo baada ya kupitia gharama za mwingilio wa kampuni za simu na kuweka punguzo hilo.
Mkurugenzi Mkuu wa Tcra, Profesa John Nkoma anasema wameshusha gharama hizo ili watumiaji wa simu wawe huru kupiga simu kwenda mtandao wowote.
 Anasema gharama mpya zitawaondolea Watanzania mzigo wa kubeba laini nyingi za mitandao tofauti.
 Profesa Nkoma anasema uamuzi wa kushusha gharama za mwingiliano wa mawasiliano ya simu za mkononi itakuwa sheria ambayo kampuni zote za simu zitalazimika kuzitekeleza.


Source :Mwananchi

[AUDIO] Brand New: TID ft. Profesa Jay - Raha

EMPLOYMENT OPPORTUNITY

EMPLOYMENT OPPORTUNITY - PATA KAZI "GIZ Tanzania"

Junior Administrative Professional (Event Management)

As an international cooperation enterprise for sustainable development with worldwide operations, the federally owned Deutsche Gesellschaft für Internationale Zusammenarbeit (GIZ) GmbH supports the German Government in achieving its development-policy objectives.

The GIZ programme ‘Support to the East African Integration Process‘ is currently looking to fill the position of Junior Administrative Professional (Event Management)

Duty station: Arusha

Terms of the Contract: Fixed term contract

Responsibilities:

The Junior Administrative Professional (Event Management) is responsible for the coordination and logistical implementation of events, seminars and conferences of the GIZ Programme in Arusha and for the smooth running of the day-to-day office routine.

Tasks
He/she
• organises and coordinates logistical aspects for planning, holding and documenting meetings, workshops, seminars and other events
• liaises with the regional offices to ensure that tickets, boarding passes and travel claims are forwarded and handled timely and according to GIZ orientations
• ensures that events are supplied with the required materials and media (information leaflets, writing material, ID badges, …);
• keeps a register of service providers and collects information on client satisfaction with the service provided;
• arranges programs for visitors, makes travel arrangements such as booking tickets, flights, hotel reservations, transport etc.;
• handles telephone calls and receives visitors/suppliers and directs them to the officer in charge;
• assists in and/or carries out other office duties and tasks, as assigned.

Required Entry Qualifications and Competencies
• Bachelors Degree in Business Management and/ or Secretarial Services and/ or a Diploma in Secretarial Services, Business Administration/Management/Human Resource;
• At least 3 years’ professional experience in the field of Event Management, office management or similar;
• Very good working knowledge of ITC technologies (related software, phone, fax, email, the internet) and computer applications (e.g. MS Office);
• Very good knowledge of English, ideally knowledge of German;

Applications:
Interested candidates are invited to send their application letter together with their CV and copies of certificates addressed GIZ-EAC Office, P.O. Box 9433, Arusha, EAC Headquarters, Former State Lodge, EAC Close by [10.03.2013].
Applications sent by email are welcome and should be sent to: eac-germancooperation@giz.de

Only shortlisted candidates will be contacted.

Papa afanya misa ya mwisho kabla kujiuzulu

Papa Benedict amefanya misa yake ya mwisho hadharani kabla ya kujiuzulu rasmi hapo kesho, kitendo kama hicho kilifanyika katika Kanisa Katoliki miaka mia sita ilyopita.
Amewaambia maelfu ya watu waliokusanyika katika viwanja vya Mtakatifu Petro huko Vatican kwamba alikuwa anafahamu uzito wa aamuzi wake lakini amefarijika kutokana na imani yake kwa ungu na Kanisa Katoliki.
Papa aliwaambia mamia ya waumini waliofika kushuhudia misa yake kuwa anafahamu vyema athari za umauzi wake lakini alikuwa na amani kwa sababu ya imani yake kwa Mungu na kanisa.
Mara kwa amara waumini walishangilia hotuba zake akisema kuwa alihisi kupotewa na nguvu katika miezi ya karibuni na kumtaka Mungu kumsaidia katika kufanya uamuzi huu.
Pia alisema kuwa atamuombea mrithi wake atakayechaguliwa katika wiki chache zijazo

Monday, February 25, 2013

Rushwa yatajwa kutawala ndani ya JWTZ nchini

TANZANIA imetajwa kuwa ni miongoni mwa nchi zinazokabiliwa na tatizo la rushwa ndani ya jeshi.
Taasisi ya Transparency International (TI), ambayo hutafiti masuala ya rushwa duniani imeitaja Tanzania kwamba jeshi lake lina rushwa kubwa na ndogondogo.
Kwa mujibu wa gazeti dada la The Citizen la jana Jumapili, uongozi wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) umekanusha vikali taarifa ya taasisi hiyo.
TI inadai katika taarifa yake kuwa sekta ya ulinzi ya Tanzania inakabiliwa na tatizo hilo na hiyo ni kutokana na mambo yake kuendeshwa kwa usiri mkubwa.
“Hakuna kitu kibaya kama la rushwa kwenye jeshi, maana kuna fedha nyingi inatembea kutokana na ughali wa vifaa vya kijeshi. Bado Serikali nyingi zinafanya mambo haya kuwa siri na kutoa mwanya kwa rushwa kutembea.
“Fedha inayotumika vibaya kwa masuala ya kijeshi, ingeweza kutumia vizuri zaidi katika masuala ya maendeleo,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo iliyoandikwa na Mark Pyman, ambaye ni Mkurugenzi wa Kitengo cha masuala ya Ulinzi cha Transperancy International.
Transparency International inaeleza kuwa fedha ya rushwa inayotembea kwenye sekta ya ulinzi inakadiriwa kufikia kiasi cha Dola 20 bilioni (Sh32 trilioni).
“Ripoti ya Transparency International itufungue macho Watanzania maana kwa kawaida huwa kila watu wakihoji mapato na matumizi ya jeshi tunaambiwa hatuwezi kujibiwa kwa madai ya woga wa kuhatarisha usalama wa taifa,” alikaririwa mbunge mmoja na gazeti la The Citizen.
Tanzania, hata hivyo, iko juu ya nchi nyingi za Afrika kwa tatizo la rushwa ingawa inatakiwa kurekebisha mianya mingi kwenye sekta hiyo.
“Tunaona Tanzania ina changamoto ya kuimarisha vyombo vya kutupa jicho kwenye jeshi. Mathalani, kuna Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Mambo ya Nje, lakini haina meno ya kuingia kwa undani masuala ya kijeshi,” iliongeza Transparency International.
Msemaji wa JWTZ, Kanali Kapambala Mgawe, hata hivyo, alikaririwa na gazeti la The Citizen akidai kuwa taasisi yake imekuwa ikifanya kazi kitaalamu na kimaadili akitolea mfano jinsi wanavyoajiri wanajeshi kwa kufuata vigezo.
Transparency International inasema kuwa kuna Kitengo cha Utawala Bora cha Serikali ambacho hufanya ukaguzi kwenye jeshi ingawa halijatoa ripoti ya aina yoyote kuhusiana na ukaguzi wa bajeti ya jeshi. “Mfano kuna taarifa kuwa Kitengo cha Kilimo cha Jeshi la Kujenga Taifa (Suma-JKT) kuna kinajishughulisha na uchimbaji madini na biashara nyingine lakini kuna udhibiti mdogo,” iliongeza taarifa yao.
Julai mwaka jana, maofisa saba waandamizi wa Bodi ya Zabuni ya Suma-JKT walifunguliwa mashitaka ya matumizi mabaya ya ofisi na uhamishaji usio wa halali wa zaidi ya Sh 3.8 bilioni.
Waliotuhumiwa ni pamoja na Kanali Ayoub Mwakang’ata, Luteni Kanali Mkohi Kichogo, Luteni Kanali Paul Mayavi, Meja Peter Lushika, Sajini John Laizer, Meja Yohana Nyuchi na Luteni Kanali Felix Samillan wanaodaiwa kufanya makosa hayo mwaka 2009.
Tanzania imewekwa katika Kundi D kwenye orodha hiyo ya Transperancy International ya nchi zinazokabiliwa na kiwango cha juu cha rushwa na vigezo vinavyoangaliwa ni sekta za siasa, fedha, utumishi wa Kundi la D ni nchi ambazo zinakabiliwa na kiwango cha juu cha rushwa na katika orodha hiyo zimo pia nchi za Russia na China.
Hata hivyo, nchi zenye kiwango cha juu cha rushwa ziko katika Kundi F wakati zile zenye kiwango cha chini cha rushwa ziko Kundi A.

Source:Mwananchi

SEMINA YA NENO LA MUNGU NA MWL.CHRISTOPHER MWAKASEGE


Saturday, February 23, 2013

Mkasi - SO5E11 With Mad Ice

Mfuko wa Bima ya afya wafananishwa na wizi

WANACHAMA wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) wa mkoani Simiyu, wilaya ya Meatu wamesema mfuko huo pamoja na kutokuwa na tija kwao ni sawa mnyanganyi anayewanyang’anya sehemu ya mishahara yao kwa njia ya udanganyifu.
Wakazi wa maeneo mbalimbali ya wilayani humo, wanaeleza kusikitishwa kwao na kitendo cha kukatwa mishahara yao mara tu wanapoajiriwa, kwa maelezo kuwa wanakuwa wamejiunga na NHIF bila hata kuhojiwa ikiwa wapo tayari kujiunga na mfuko huo au la.
Tatizo kubwa zaidi linaelezwa kuwa ni kukatwa fedha hizo zinazoelezwa kutumika kugharamia huduma za matibabu ya mwajiriwa na wanafamilia wake wasiozidi wanne, lakini imebainishwa kuwa wahusika hawapati huduma hizo kutokana na kutokuwa na kadi za uanachama na hivyo, mbali na kukatwa mishahara bado hujikuta wakitoa fedha taslimu kugharamia huduma hizo pindi wanapougua.
Paul Nlimandago (42) mkazi wa Majengo alisema mshahara wake ulikuwa ukikatwa michango ya mfuko huo kwa kipindi cha miaka minne huku yeye na familia yake wakipata huduma za afya kwa kulipa fedha taslimu, kutokana na kutopatiwa kadi za uachama.
“Nilipata kadi ya uanachama miaka minne tangu mshahara wangu ulipoanza kukatwa michango ya uanachama…, nilikuwa najaza fomu, napeleka picha na fedha zinakatwa kila mwezi kwa kipindi chote hicho  bila kupata kadi,” anabainisha Nlimandago
Naye Juma Said (43) anabainisha kuwa wanachama hawana imani na mfumo unaotumika kulipia gharama wanazotumia, kwani hutakiwa kuweka sahihi ambazo hazioneshi kiasi cha fedha kitakachodaiwa na watoa huduma, kwa ajili ya malipo ya huduma.
“Bima ya afya  ni wizi mtupu, mtu unatibiwa kisha unapewa makaratasi usaini huku gharama unazodaiwa kutokana na huduma uliyopatiwa zikiwa hazioneshwi; hii siyo sawa, nashauri fomu ambazo wanachama tunasaini baada ya kuhudumiwa zirekebishwe, iwekwe sehemu ambayo mtu utaona deni lako ili uidhinishe malipo unayoafiki kuyatumia,” Said anaeleza na kushauri.
Anasema jambo la kusikitisha zaidi ni mtu kutakiwa kusaini karatasi ambayo haufahamu wataenda kudai kiasi gani cha fedha kisha unaelezwa, “dawa ulizoandikiwa zote hazipo, nenda ukanunue nje.” anasema inaumiza na kukatisha tamaa kuliko maana inayopatikana katika neno sana.
Shaban Alley (40) anashauri mamlaka husika zifuatilie kwa karibu huduma wanazopatiwa wanaochangia malipo ya huduma za afya, kwa kufanya uchunguzi wa kushtukiza na kwamba wanaotakiwa kutekeleza jukumu hilo ni wasioishi eneo linalochunguzwa, ili kuondoa uwezekano wa kufichiana dhambi na kulindana.
“Wakitaka wapate ukweli, wanatakiwa  wafike ghafla bila kutoa taarifa na kujifanya wagonjwa wenye kadi za kuchangia huduma za afya kupitia NHIF au CHF, wakihitaji kuhudumiwa hata kwenye hospitali binafsi ambazo zina mikataba na NHIF; watashuhudia jinsi wanachama wao wanavyopata shida mbalimbali wanapohitaji huduma hizo,” anaeleza Alley
Greyson Kakulu, mwanachama mwingine wa NHIF anapotakiwa kuzungumzi hali ya huduma za afya akiwa katika mpango huo wa kulipia huduma za afya kabla ya kuugua anasema: “Siridhishwi hata kidogo ni mwaka wa tatu sasa tangu nijiunge na mfuko huu, kila mwezi mshahara wangu unakatwa lakini sihudumiwi kama mwananchama kwa sababu sina kadi,”anaeleza na kuongeza:
“Nagharamia huduma za afya ninazopatiwa mimi na familia yangu lakini ninapokwenda kudai kurejeshewa fedha zangu sijawahi kurudishiwa; hali hii inaumiza sana, hasa ikizingatiwa mtu huwezi kukataa kujiunga wala kujitoa, naomba ishughulikiwe.”

Source:Mwananchi

AJALI MBAGALA

Mmoja wa majeruhi katika ajali hiyo

Hili ndilo gari lililopata ajali baada ya kuacha njia










majeruhi wa ajali hiyo

Kanisa katoliki laruhusu tembe za kuzuia mimba



Kanisa Katoliki nchini Ujerumani limeamua kuwa ni halali kwa mwanamke kutumia tembe ya kuzuia mimba mara tu baada ya kubakwa.
Uamuzi huu umefanywa kufuatia mkutano wa viongozi wa Kanisa Katoliki nchini Ujerumani baada ya mwanamke mmoja aliyekuwa amebakwa kusema kuwa alizuiwa kufanyiwa matibabu siku mbili mfululizo katika Hospitali zinazofadhiliwa na Kanisa Katoloki zikisema kuwa kuzima mimba ni kinyume cha maongozi yake.
Maaskofu nchini Ujerumani wamekuwa wakijikuta njia panda, ambapo upande mmoja wanahangaishwa na msimamo wa Kanisa Katoliki, na kwa upande mwingine tatizo lililompata mwanamke huyo aliyebakwa, kufukuzwa na hospitali zinazosimamiwa na Kanisa hilo zilizoko mjini Cologne.
Mwishowe Maaskofu hao walikubaliana kuwa itakuwa halali ikiwa tembe hizo zitatumiwa na mwanamke aliyebakwa kwa lengo la kuzuia kushika mimba badala ya kutoa mimba
Hii ina maana kuwa itaweza kutumiwa tu kama kifaa cha kuzuia kushika mimba lakini sio kuavya. Tembe hizo hutumiwa na wanawake wengi wasiotaka kushika mimba baada ya tendo la ndoa.
Hata hivyo Kanisa Katoliki nchini Ujerumani, ambako Papa wa sasa alitoka, limegawanyika kufuatia tendo hilo la ubakaji.
Ubishi kama huo nchini Marekani haukufikia uamuzi baada ya pande zote zilizokuwa zikibishania dawa hiyo kusema kuwa ni vigumu kujua kama baada ya kitendo cha ndoa asubuhi inayofuata mwanamke ameshika mimba au la.

Wednesday, February 20, 2013

[AUDIO] Brand New: Grace Matata ft. Otuck - Imba Nami





Mbowe: Sasa tumekuja kivingine

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeanza kubadili muundo wake, na kutekeleza wa sera yake ya majimbo.
Juzi chama hicho kilizindua jimbo la Kanda ya Kaskazini inayojumuisha mikoa ya Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga.
Uzinduzi wa Kanda hiyo umefanyika Jijini Arusha ambapo mbunge wa Karatu, Israel Natse ameteuliwa kuwa Mwenyekiti huku Amani Golugwa akiwa Katibu wake.
Katika mahojiano na gazeti hili, Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe amefafanua mikakati, malengo na sera hiyo akisema hailengi kujitenga wala kugawa nchi kama inavyodaiwa “waliofilisika kisera na kisiasa”.
“Kuwa na Kanda siyo kujitenga, bali ni kusogeza mfumo na shughuli za chama kila sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania badala ya mtindo uliozoeleka wa kila kitu kuendeshwa kutokea Dar es Salaam,” anafafanua Mbowe.
Mwenyekiti huyo ambaye ni kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, anasema Sera ya Kanda siyo ukabila, akitolea mfano Kanda ya Kaskazini inayoundwa na watu wa makabila zaidi 25 wenye imani na dini tofauti.
Anasema sera hiyo itawezesha wanachama wa Chadema waliotapakaa kila sehemu nchini kupata fursa ya kuonyesha na kutumia vipaji na uwezo wao wa uongozi katika harakati za kukijenga chama hicho kikuu cha upinzani.
Anasema mfumo huo utaondoa dhana kuwa Chadema ni Mbowe, Dk Willibrod Slaa, Zitto Kabwe, Godbless Lema, John Mnyika na wengine wachache wenye majina kitaifa, badala yake kila mwanachama atatumia kipaji na uwezo wake pale alipo kukijenga na kukieneza Chadema.
“Kinachotuunganisha na ambacho tunakisimamia kama chama cha siasa ni Utaifa wetu, umoja, mshikamano na heshima kwa kila mtu bila kujali dini, imani wala kabila lake,” anasisitiza
Kanda zingine na mikoa inayoziunda kwenya mabano ni Mashariki (Dar es Salaam na Pwani), Kusini (Lindi na Mtwara, Kati (Morogoro, Dodoma na Singida), Nyanda za Juu Kusini (Njombe, Iringa, Mbeya na Ruvuma) na Magharibi inayoundwa na mikoa ya Rukwa, Katavi, Kigoma na Tabora.
Kanda zingine ni Ziwa Mashariki (Shinyanga, Simiyu na Mara), Ziwa Magharibi (Mwanza, Geita na Kagera), Pemba (Kusini Pemba na Kaskazini Pemba) na Unguja (Mjini Magharibi, Kusini Unguja na Kaskazini Unguja).
Mbowe anasema utekelezaji wa sera na mfumo wa Kanda kutaiwezesha Chadema kutumia mbinu anazoziita za medani kwa kushambulia kwa kushtukiza kutoka kila kona bila ‘askari’ wake kujulikana.

Source:Mwananchi

[AUDIO] Brand New: Jux - Niwe Nawe




Jengo la ATCL hatarini kupigwa mnada

JENGO la Makao Makuu ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) liko hatarini kupigwa mnada kwa amri ya Mahakama kutokana na kushindwa kulipa deni inalodaiwa na Kampuni ya Huduma za Utalii ya Leisure Tours and Holidays.
Tayari Mahakama Kuu Kitengo cha Biashara imeamuru kampuni hiyo ifanye uthamini wa jengo hilo na kuwasilisha mahakamani taarifa hiyo leo.
Hatua hiyo inatokana na mao mbi yaliyowasilishwa mahakamani hapo na kampuni hiyo ambayo ni mshindi wa tuzo katika kesi ya madai namba 56 ya mwaka 2009 iliyotokana na mgogoro wa kibiashara baina yake na ATCL.
Kampuni hiyo inaidai ATCL Dola za Marekani 716,259.25 (Sh1.1 bilioni) baada ya kushindwa kulipia huduma za ukodishaji wa magari ambazo kampuni hiyo ilitoa kwa ATCL.
Mbali na kiasi hicho ambacho ni deni la msingi pamoja na riba ya asilimia 10 kwa kipindi cha miaka miwili, pia ATCL inapaswa kuilipa kampuni hiyo gharama za uendeshaji wa kesi hiyo.
Katika amri ya Mahakama hiyo iliyotolewa na Jaji Mfawidhi Robert Makaramba Februari 11, 2013, kabla ya kutoa amri ya jengo hilo kupigwa mnada, ilimwamuru mshinda tuzo kufanya uthamini wake.
Taarifa ya amri hiyo inasomeka: “Amri: Muombaji/mshinda tuzo anatakiwa kuwasilisha katika Mahakama hii taarifa ya uthamini wa jengo la ATCL, lililoko katika Mtaa wa Ohio, (Dar es Salaam) saa 3.00 asubuhi, Februari 20, 2013. Shauri litakuja kwa amri zaidi saa 3.00 asubuhi, Februari 25, 2013,” inasomeka amri hiyo.
Hata hivyo, Wakili wa mshinda tuzo, Jerome Msemwa wa Kampuni ya Msemwa & Company Advocates, alisema licha ya amri ya Mahakama kufanya uthamini wa jengo hilo, lakini maofisa wa mshindwa tuzo wamezuia kufanyika uthamini.
Wakili Msemwa alisema maofisa hao wa mshindwa tuzo walizuia uthamini huo kufanyika kwa madai kuwa watalipa.
Alisema kuwa kwa muda mrefu wamekuwa wakiahidi hivyo bila utekelezaji na kwamba leo anawasilisha mahakamani taarifa hiyo ya kuzuiwa na kisha kusubiri amri ya Mahakama.
Awali, Novemba 20, 2012, Mahakama hiyo ilimwamuru mshindwa tuzo kuwasilisha mahakamani hapo jedwali la malipo ndani ya kipindi cha mwezi mmoja tangu tarehe ya amri hiyo.
Hata hivyo, mshindwa tuzo hakutekeleza amri hiyo ndipo mshinda tuzo alipowasilisha maombi ya kukamata na kuuza jengo hilo.
Katika kesi ya msingi pande zote zilikubaliana kuzungumza na kufikia mwafaka nje ya Mahakama, makubaliano ambayo kila upande ulisaini ikiwa ni ishara ya kukubali kutekeleza.
Waliwasilisha mahakamani makubaliano hayo, Aprili 8, 2011 ili yaidhinishwe na kuwa uamuzi halali.
Katika makubaliano hayo, mshindwa tuzo anapaswa kumlipa mshinda tuzo kiasi cha Dola 596,882.97(Sh952 milioni) kwa awamu tatu za kiasi cha Dola 198,960.99 (Sh317 milioni) kwa kadri anavyopata fungu kutoka Hazina.
Pia, walikubaliana mshindwa tuzo amlipe mshinda tuzo kiasi cha Dola 119, 376.97(Sh190 milioni) kikiwa ni riba ya asilimia 10 kwa mwaka ya malipo ya msingi, kwa kipindi cha mwaka wa 2009 na 2010, kwa awamu tatu kadri anavyopata fungu kutoka Hazina.
Hata hivyo, ATCL haikutekeleza ulipaji wa fidia hiyo kama walivyokubaliana na jinsi Mahakama ilivyoamuru.

source:Mwananchi

AJALI MAENEO YA SOKOTA

Pikipiki ikiwa chini baada ya kugongwa na gari ndogo Toyota corrola na baadae kugonga Roli lililokuwa limesimama
Kwenye picha ni abiria aliyekuwa amepakiwa kwenye pikipiki iliyopata ajali maeneo ya Sokota,abiria huyo alikuwa amepata majeraha meneo ya kichwani

Monday, February 18, 2013

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE YATANGAZWA

Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Mh.Shukuru kawambwa leo ametangaza matokeo ya Kidato cha nne,maarifa na QT.

jumla ya watahiniwa waliofaulu ni 23520 kuanzia daraja la I hadi la IV,wasichana waliofaulu ni 7178,na wavulana ni 16342.Waliofaulu daraja la kwanza ni 6141,daraja la pili ni 6495,daraja la tatu ni 15426,na waliofeli ni 24903.

shule bora ni St.Francis Girls ya Mbeya,marian Boys ya Bagamoyo,feza Boys Dar es salaam,Marian Girls Bagamoyo na Sisini ambazo ndizo shule tano bora

                                  BOFYA HAPA KUONA MATOKEO

Watu watatu wamekamatwa kwa tukio la kupigwa risasi Padri Evaristi Mushi.

Friday, February 15, 2013

Breaking News

Polisi jijini DSM imepambana na baadhi ya watu wanaodaiwa ni Waumini wa dini ya Kiislam walioamua kuandamana katika maeneo ya Kariakoo licha ya kupigwa marufuku kwa maandamano hayo na jeshi la Polisi,na lengo la maandamano hayo ni kushinikiza kupewa dhamana kwa Sheikh Issa Ponda.

[AUDIO] Brand New: Diamond ft. Tanzanite - Mapenzi



Spika aongezewa ulinzi

SPIKA wa Bunge, Anne Makinda ameongezewa ulinzi pamoja na kubadilishiwa namba za gari analotumia kutokana na vitisho anavyovipata kutoka kwa wananchi ambao wamekuwa wakimtumia ujumbe wa simu.
Taarifa ambazo Mwananchi imezipata zinaeleza kuwa hatua hiyo imekuja baada ya viongozi wa Chadema kutoa namba za Spika na kuzigawa kwa wafuasi wake waliofika kwenye mkutano uliofanyika kwenye Viwanja vya Mwembe Yanga, jijini Dar es Salaam hivi karibuni ili wamtumie ujumbe mfupi wa simu.

Hivi karibuni gazeti hili liliripoti kuwa Spika Makinda amepokea ujumbe mfupi wa simu zaidi ya 400 na kupigiwa simu zinazofikia 200 za kumkashifu na vitisho.
Taarifa zilizopatikana jana zinaeleza kuwa Spika Makinda amekuwa akitumiwa ujumbe mfupi wa vitisho ambavyo inaonyesha kuwa wananchi wana hasira naye na ndiyo maana ameongezewa ulinzi.

Vyanzo vyetu vya habari vimeeleza kuwa gari la Spika Makinda limebadilishwa namba kwa kuondolewa herufi S ambayo humaanisha Spika na kuwekwa namba nyingine ambazo bado hazijajulikana.

“Watu wanaomtumia ‘meseji’ wana hasira, wanaweza kumdhuru na ndiyo maana ameongezewa ulinzi. Hata magari yake aliyokuwa akitumia yamebadilishwa na kupewa mengine tofauti,” kilieleza chanzo chetu cha habari.

Spika Makinda mwenyewe alipopigiwa simu ili kueleza kuhusu suala hilo la kuongezewa walinzi simu yake ilikuwa ikiita tu bila kupokelewa.

Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah naye simu yake ilikuwa ikiita tu bila kupokelewa.Tangu Chadema wagawe namba hiyo baada ya kumtuhumu Spika pamoja na msaidizi wake, Job Ndugai kuwa amekuwa akipindisha kanuni wakati wa kuliongoza Bunge.

Taarifa zilieleza kuwa wamekuwa wakisumbuliwa na kutumiwa ujumbe za vitisho.Wakati hayo yakitokea, tayari Ofisi ya Bunge imesema itawachukulia hatua kali wale wote waliotumia lugha chafu kwa ujumbe mfupi ama kupiga moja kwa moja kwa Spika na Naibu wake.

Katibu Mkuu wa Bunge, Dk Kashililah juzi alisema kuwa kutoa namba si tatizo, bali kuzitumia namba hizo kinyume na taratibu ndiyo haitakiwi, jambo ambalo linaweza kusababisha baadhi yao kuchukuliwa hatua za kisheria.

“Wote waliotoa lugha za matusi kwa Spika Makinda na Naibu Ndugai watachukuliwa hatua za kisheria. Tutawatafuta kwa njia zote, hii itasaidia kuwa fundisho kwa watu wenye tabia kama hizo ambao wanapewa namba kwa manufaa ya wananchi, lakini wanazitumia kinyume chake,” alionya Kashililah.

“Tutawasaka kwa kila hali, tutawabaini tu kwa kushirikiliana na idara mbalimbali ikiwemo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Polisi ili wachukuliwe hatua kali.”
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika alipoulizwa jana kuhusu msimamo wa chama chake baada ya kutoa namba hizo kwa wananchi alisema; “Bunge halijatuuliza ila wakituuliza tutajibu.”

[AUDIO] Brand New: Diamond - Ukimwona



[AUDIO] Brand New: Nikki wa II ft. Joh Makini & G-Nako - Nje Ya Box






Thursday, February 14, 2013

Ofisa usalama mbaroni wizi kontena

VIGOGO watano akiwamo Ofisa wa Usalama wa Taifa wanashikiliwa polisi, kwa tuhuma za kutaka kusafirisha kontena la madini aina ya Tantalite yenye thamani ya Dola 22,000 za Marekani yaliyokuwa  yakisafirishwa nje ya nchi.
Akizungumza na Dar es Salaam jana, Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe aliapa kuilinda Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kwa udi na uvumba.
Kiapo hicho alikitoa jana wakati akiwataja watu  wanaoshikiliwa na polisi kwa kuichafua TPA,  wakati yeye akifanya jitihada za kuisafisha.
Aliwataja watu hao  kuwa ni Mfanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mmiliki wa Kampuni ya Uwakala wa Kusafirisha Mizigo ya GFC na msaidizi wake.
Wengine ni  Ofisa wa Mamlaka ya Ukaguzi Madini (TMAA),  Mmiliki wa Bandari Kavu na Ofisa wa Usalama  wa Taifa.
Dk Mwakyembe alisema mzigo huo uliokamatwa ukitaka kusafirishwa kwenda nje ya nchi,  madini yake aina ya Tantalite hayapatikani nchini, bali nchi za Burundi, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Alisema walibaini katika nyaraka  zinazohusiana na kusafirishwa kwa madini hayo kuwa, zinaonyesha madini hayo yanatoka nchini wakati siyo kweli.
Kuhusu Ofisa wa Usalama wa Taifa, Mwakyembe alisema ni mtu muhimu ambaye taifa linamwamini kuficha siri za nchi, lakini akashangaa kuwamo kwenye mlolongo huo.
“Yaani sisi tunafanya kazi ya kuisafisha bandari, watu hawa wanaichafua kuifanya kuonekana ni uchochoro wa kusafirisha magendo,” alisema Dk Mwakyembe na kuongeza:
“Kutokana na hili, kampuni mbili za meli za Safmaline na Maikesi zimesitisha kusafirisha mizigo yao, kutokana na michezo michafu kama hii, watu siyo waaminifu wanabadilisha mizigo halisi  kama madini wao wanaweka simenti au magadi ambayo yana uzito sawa na mzigo halisi.”
Aliongeza kuwa mmiliki wa Bandari Kavu ya PMM na mtendaji wake mkuu nao pia wanahojiwa  polisi kutokana na tuhuma hizo.
Kuhusu mfanyakazi wa TRA, Dk Mwakyembe alisema ndiye aliyetoa ridhaa ya mzigo huo kusafirishwa  kwa magendo.
Pia, Dk Mwakyembe alisema amewaagiza maofisa wa polisi kumtafuta raia wa Congo aliyepeleka mzigo huo bandarini, kwa lengo la kuusafirisha  kwenda  nchini Romania.

MSIMAMO WA LIGI YA VODACOM


NEW TARCK BY WALTER-SIACHI

Tuesday, February 12, 2013

[AUDIO] Brand New: Banana Zorro ft. Baby Madaha & Chidi Beenz - Sio Kama Wale...








SITTA NA LOWASA WATEMWA KAMATI KUU CCM




Makada wa CCM waliotangaza nia ya kugombea Urais katika Chama hicho wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 wametoswa katika nafasi ya Ujumbe wa Kamati Kuu ya Chama hicho CC.
Waliotoswa katika nafasi hiyo ni pamoja na Waziri Mkuu aliyejiuzuru, Edward Lowassa pamoja na mawaziri wengine walioko madarakani kama  Samuel Sitta (Ushirikiano wa Afrika Mashariki) na Bernard Membe (Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa).
Mbali na mawaziri hao makada wengine waliotoswa katika uchaguzi huo ni pamoja na January Makamba, Martin Shigela, Willison Mukama, Mohamed Seif Khatib, Omar Yusufu Mzee hata hivyo taarifa za ndani ya NEC ya CCM iliyonaswa na imedai kwamba baadhi ya makada hao wametoswa kutokana kile kinachoelezwa kwamba wanadalili na makundi ndani ya Chama hicho.
Kwa upande wa wale ambao majina yao yalipishwa katika uchaguzi huo lakini wakaangukia pua ni pamoja na Balozi Ali Karume, Gwaride Jabu, Dk Raphael Chegeni, Dk Cyril Chami, Michael Lekule Laizer, Ramadhan Madabida, Hassan Wakasuvi, Dk Fenella Mukangara, Shamsa Mwangunga na Said Mtanda.