Wednesday, April 17, 2013

BI KIDUDE HATUNAYE TENA

TASNIA ya Sanaa ya Muziki nchini Tanzania imepata pigo jingine baaada ya Gwiji la muziki wa mwambao wa pwani Fatuma Binti Baraka "Bi Kidude" kufariki dunia muda mfupi uliopita.
Taarifa za kifo cha mwanamuziki huyo zimetufikia  hivi punde toka kwa familia yake zinasema Bi Kidude aliekuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Hindu Mandal amefariki leo.
Bi Kidude atakumbukwa kama mwanamuziki mkongwe zaidi nchini ambaye alianza muziki akiwa na umri wa miaka 10 tu na aliwahi kupokea tuzo mbalimbali kutokana na mchango wake katika muziki wa mahadhi ya mwambao. Hakika sanaa nchini imepoteza moja ya nguzo kubwa.

hii ni baadhi ya nyimbo zake alizowahi kuimba enzi za uhai wake

The Churchill Show Season 3, Episode 5

VIDEO BOSTON BOMB BLAST

Deadly explosions at Boston Marathon in pictures

















Tuesday, April 16, 2013

The Churchill Show Season 3, Episode 4

Wyre featuring JuaCali - Khadija (Remix)

MOTO MAENEO YA POSTA

Moto umetokea jijini Dar maeneo ya Posta katika jengo moja ambalo wanaishi watu. Mwandishi wetu Zainab Chondo aliyekuwapo katika tukio ametuambia kwamba ghorofa hiyo ni mali ya NHC, na moto huo umeharibu jengo lenyewe na kuunguza vitu vilivyokuwa ndani. chanzo hakijajulikana, endelea kutufuatilia kwa taarifa zaidi.

 
Kikosi cha zimamoto kikicharibu kuuzima moto huo

Monday, April 15, 2013

The Churchill Show

Panya mwokozi wa maisha

Panya akiwa kwenye mafunzo
Shirika moja lisilo la kiserikali la Ubelgiji APOPO limeanza kuwafundisha panya namna ya kutambua mabomu yaliyofukiwa ardhini. Panya hao ambao ni wakubwa kuliko panya wa kawaida wanafanyiwa majaribio Morogoro Tanzania .Inaaminika wanauwezo mkubwa wa kunusa kuliko mbwa. Hii inatokana na kuwa pua zao zipo karibu na ardhi,hali ambayo inawasaidia katika kazi yao ya utambuzi wa mabomu. 
Panya wanafundishwa jinsi ya kunusa wakiwa wadogo, kwa kuwekewa vitu vyenye madini ya milipuko.Tangu mwaka 2000, APOPO imekuwa ikiwafunza panya kwenye chuo cha Sokoine,Morogoro. Mwaka 2006 panya wa hao walianza zoezi la kutafuta mabomu ya ardhini huko Msumbiji. Kabla ya panya kuanza kazi ya kunusa wapi mabomu yalipo, lazima wafuzu mtihani kutimiza viwango vya kimataifa vya kutambua mabomu ardhini.
Panya hujifunza kufuta eneo fulani hatua kwa hatua. Waya au kamba hufungwa mwilini kutoka kwenye ufito. Wasimamizi wawili husimama kila upande wa ufito na kumruhusu panya kutembea toka mwanzo wa ufito hadi upande mwingine kwa kufuata jinsi waya au kamba alizo fungwa mwilini. Katika mafunzo ya awali panya hufunzwa kunusa kemikali aina ya TNT ndani ya chombo cha chuma.
Baadaye kila panya hufanya mafunzo kwenye eneo ambalo kuna mabomu ya ardhini yaliyofukiwa na vifaa ambayo huzuia mlipuko. Ikiwa panya ameweza kunusa na kutambua yalipo madini asilia ya TNT huwa anasimama na kuanza kufukua sehemu hiyo ya ardhi iliyofukiwa bomu. Kuwafundisha panya kunachukua muda wa mwaka na inagharimu dola za Kimarekani $6,000 sawa na Euro 4,670.
 Wakati wa mafunzo panya hupewa zawadi kwa kufuzu vizuri kwa sauti maalumu ambayo inaashiria kufuzu kwake na kupewa kipande cha ndizi kama zawadi. Panya aliyefuzu vizuri huwa ana uwezo wa kuzunguka mita 400 za mraba kwa siku, wakati eneo kama hili litamchukua binadamu wiki mbili ili kuweza kugundua wapi kumefukiwa bomu. 
 Kulinganishwa na mbwa, panya wanaweza kutumiwa na mtu yeyote kwani hawana tabia ya kutokuwa na mahusiano ya karibu na mtu aliyemfundisha kama walivyo mbwa. Panya anaweza kufanya kazi ya kufichua mabomu, hata kama aliyemfundisha hayupo na huwa wanafanya kazi vizuri kwa ufanisi na mtu yeyote. Hakuna shida kwa panya aliyefundishwa Tanzania, kwenda kufanya kazi Msumbiji, Angola,Thailand na Kambodia.
 Hadi kufukia sasa nchini Msumbiji, zaidi ya mita za mraba milioni 6,5 za ardhi zimeshachunguzwa na mabomu 2,000 yaliyotegwa ardhini yamepatikana na kuharibiwa, pia bado mabomu 1,000 kuteguliwa na bunduki na silaha nyingine ndogo 12,000 zilipatikana. Na mpaka sasa kuna makundi saba yenye watu 54 ambayo yanashughulika na kazi ya kutegua mabomu kwa kuwatumia panya.

Waasi wa M23 waionya Tanzania

Wanajeshi wa M23
Waasi wa kundi la M23 wameitaka Tanzania kuachana na mipango ya kuchangia wanajeshi wake katika kikosi cha Umoja wa Mataifa kinachopangwa kutumwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kupambana na waasi .
Waasi wa kundi hilo la M23 ambao wamekanusha madai ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa kwamba nchi jirani za Rwanda na Uganda zinawaunga mkono,wameonya katika baruwa iliyotumwa na kiongozi wa kisiasa wa kundi hilo Betrand Bisimwa kwa Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania kwamba daima wamekuwa wakipata ushindi dhidi ya vikosi vikubwa vyenye silaha nzuri.
Bisimwa ameandika " Jambo kama hilo litawakuta kikosi hicho cha Umoja wa Mataifa cha kuingilia kati iwapo busara yao itashindwa kufanya kazi kuingilia kati na kuzuwiya hali ya hatari ilioko kwenye mkondo huo."
Bisimwa amesema kwa ajili hiyo kundi hilo la waasi la M23 linaomba bunge na wananchi wa Tanzania kufikiria upya kwa uangalifu juu ya hali hiyo na kuishawishi serikali ya Tanzania kutowapeleka watoto wao wa kiume na wa kike wa taifa hilo la uadilifu kushiriki kwenye vita vya kipuuzi dhidi ya ndugu zao wa Congo.

JK awaonya viongozi wanaoleta mvutano kuhusu barabara

Rais Jakaya Kikwete amewaonya viongozi wanaoleta mvutano juu ya wapi ipitishwe Barabara ya Tanga-Pangani-Saadani hadi Bagamoyo kwa kuwa wanaendesha ubishani unaoweza kuwachanganya wataalamu walioshughulikia suala hilo.
0are
Mkinga. Rais Jakaya Kikwete amewaonya viongozi wanaoleta mvutano juu ya wapi ipitishwe Barabara ya Tanga-Pangani-Saadani hadi Bagamoyo kwa kuwa wanaendesha ubishani unaoweza kuwachanganya wataalamu walioshughulikia suala hilo.
Amesema baada ya kumalizika kwa barabara ya Tanga-Horohoro,Serikali yake sasa kwa Mkoa wa Tanga itaelekeza nguvu zake katika ujenzi wa Barabara ya Tanga-Pangani-Saadani hadi Bagamoyo.
Alisema hayo juzi alipokuwa akifungua barabara mpya ya kiwango cha lami ya Tanga-Horohoro katika sherehe zilizofanyika kwenye kituo kipya cha mabasi cha Wilaya ya Mkinga kilichopo Kasera wilayani hapa.
Barabara hiyo ya Tanga- Horohoro ya urefu wa kilometa 65 imejengwa na Kampuni ya kutoka China ya Sinohydro Corporation Ltd iliyokabidhiwa rasmi kazi hiyo Januari 4, mwaka 2010 baada ya kuingia mkataba baina yake na mfadhili ambaye ni mfuko wa Millenium Challenge (MCC) na Serikali ya Tanzania kwa gharama ya Sh69.8 bilioni. Akizungumza katika sherehe hizo zilizohudhuriwa na mabalozi wa kutoka nchi za Marekani, India, Kenya, watendaji wakuu wa MCC, mawaziri, wakuu wa mikoa ya Tanga, Pwani na wananchi, Rais Kikwete aliwaonya wanaoleta mvutano juu ya barabara hiyo kwamba wanawavuruga wataalamu.
Alikuwa akizungumzia juu ya mvutano uliojitokeza kuhusu wapi ipite barabara hiyo, ambapo wapo wanaokubaliana na wataalamu wanaotaka ipitie ndani ya Hifadhi ya Mbuga ya Taifa ya Saadani huku wengine wakiwamo wanamazingira wakipinga kwa madai kwamba ikipitishwa katikati itawafukuza wanyama waliomo.
Hotuba hiyo ya Rais Kikwete ni majibu kwa kamati ya ushauri mkoa wa Tanga ambayo katika kikao chake kilichofanyika mwezi uliopita ulijitokeza mvutano wa wapi ipitishwe barabara huku wajumbe wengine wakitaka ipite katikati ya hifadhi na wengine wakihadharisha kuwa itaathiri ustawi wa wanyama.
Katika kikao hicho kilichofanyika chini ya uenyekiti wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Gallawa, wajumbe waliagiza iandikwe barua kwa Rais Jakaya Kikwete kumuomba kukubali pendekezo la kupitisha barabara nje ya hifadhi.
Barabara hiyo kama itapitishwa katika hifadhi ya Saadani itakuwa ya urefu wa kilomita 175 na ikiwa itazungushwa na kupitishwa nje ya hifadhi italazimika kuongezeka urefu wa kilomita 35 nyingine ambapo kwa sasa ipo kwenye hatua ya kufanyiwa usanifu.
Barabara hii ya Bagamoyo-Saadan-Pangani –Tanga itajengwa kwa ushirikiano wa nchi za Jumiya ya Afrika Mashariki,ambapo kwa upande wa Kenya mradi huu unahusisha ujenzi wa barabara ya Horohoro-Lungalunga-Mombasa hadi Malindi.

Source:Mwananchi

SHEREHE ZA KUAPISHWA KWA UHURU KENYATA KATIKA PICHA


MRITHI WA HUGO CHAVES APATIKANA

Rais Mpya wa Venezuela Nicolas Maduro
Tume ya uchaguzi nchini venezuela imetangaza kiongozi wa kisoshalisti Nicolas Maduro kama mshindi wa uchaguzi wa urais kwa asilimia 51 tu ya kura.
Hata hivyo ushindi huo dhidi ya mpinzani wake mkuu Henrique Capriles ulikuwa ni wa chini ya asilimia mbili, ikiwa ni chini ya robo ya kura zipatazo milioni 15 ya zile zilizopigwa .
Ni ushindi mdogo zaidi ikilinganishwa na ule alioupata kiongozi wa chama chake hayati rais Hugo Chavez,mwaka jana, muda mfupi kabla ya kifo chake.
Kufuatia tangazo la ushindi huo Bwana Maduro alivaa mavazi yenye rangi za bendera ya Venezuela akidai uchaguzi wake ni wa haki na wa kisheria na akawataka raia wawe watulivu. Aliahidi kuendeleza sera za Bwana Chavez.
Pindi habari zilizpojitokeza kuwa Maduiro alikuwa mshindi, wafuasi wake walianza kusherehekea mjini Caracas, huku wafuasi wa upinzani nao wakianza kupiga sufuria kuonyesha ghadhabu zao.
Katika hotuba yake ya ushindi akiwa nje ya ikulu ya rais, bwana Maduro, aliambia wafuasi wake kuwa ushindi wake ni halali na umeambatana na sheria.
Aliongeza kuwa kuchaguliwa kwake kunaonyesha kuwa marehemu Hugo Chavez anaendelea kushinda vita vikuu.
Aliwataka wale waliompigia kura na wapinzani wake kushirikiana kwa niaba ya ya nchi nzima.

Friday, April 12, 2013

Mzozo kuhusu makampuni ya Mandela

Wanawe rais mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela, wameamua kuchukua hatua za kuwaondoa wasaidizi wake watatu kutoka katika makampuni anayoyamiliki.
Hii ni kwa mujibu wa vyombo ya habari nchini humo.
Makaziwe na Zenani Mandela wanadai kuwa watatu hao hawana haki ya kuwa kwenye bodi mbili za kampuni hiyo ambazo ni za thamani ya dola milioni 1.1
Mmoja wa wasaidizi hao, ambaye pia ni wakili wa Mandela, George Bizos,amekana madai hayo.
Kesi hiyo inakuja wakati kuna wasiwasi mkubwa kuhusu afya ya Mandela mwenye umri wa miaka 94
Mandela aliondoka hospitalini baada ya kutibiwa ugonjwa wa mapafu pamoja na homa ya mapafu.
Mandela alilazwa hospitalini mara ya nne katika kipindi cha miaka miwili.
Duru zinasema kuwa kumekuwa na mzozo wa kichinichini tangu mwaka 2005 wa kudhibiti pesa zinazotokana na mauzo kwenye jina la Mandela hususan picha alizokuwa anachora akiwa jela.
Makaziwe na Zenani Mandela waliwasilisha kesi mahakamani wakidai kuwa bwana Bizo, waziri wa nyumba, bwana Tokyo Sexwale na wakili wa zamani wa Mandela, Bally Chuene, hawakuwahi kuteuliwa kama wamiliki au wakurugenzi wa kampuni ya Harmonieux Investment Holdings na Magnifique Investment Holdings, kulingana na gazeti la Star.
Pesa zinazotokana na makampuni hayo zinapaswa kuwafaidi wanawe Mandela na yeye mwenyewe.
"Bizos, Chuene na Sexwale hawakuwahi kuteuliwa rasmi kama washika dau katika kampuni hiyo.''
Bwana Bizos, wakili anayeheshimika sana na ambaye pia ni rafiki wa karibu sana wa bwana Mandela, alisema kuwa watajitetea vikali katika kesi hiyo.
Aliongeza kuwa wanawe Mandela walikuwa wanataka kuuza vitu ambavyo havipaswi kuuzwa .

Audio:Diamond - Mapenzi basi

Thursday, April 4, 2013

UJUMBE KUTOKA KWA PASTOR MYAMBA KWA FANS WAKE WOTE

MZEE MANDELA ANDELEA KUPATA NAFUU

Rais mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela anaendelea kupata nafuu wakati akitibiwa homa ya mapafu, kwa mujibu wa madaktari wake.
Taarifa kutoka kwa ofisi ya rais Jacob Zuma, ilisema kuwa Mandela alitembelewa na jamaa zake wakati akiendelea kupokea matibabu.
Inaarifiwa kwa sasa hali yake inaendelea kuwa nzuri ikilinganishwa na alivyokuwa wakati alipolazwa hospitalini tarehe 27 mwezi Machi
Mandela amelazwa hospitalini sasa kwa mara ya nne katika kipindi cha miaka miwili.
Mnamo Disemba alitibiwa homa ya mapafu na kibofu na alikaa hospitalini sana kuliko wakatii mwingine wowote.
Mnamo Februari alitibiwa maradhi ya tumbo.
Wiki jana rais huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 94,pia alibitiwa maradhi ya mapafu.
Mpaka sasa hakuna taarifa zozote kuhusu muda atakaosalia kuwa hospitalini.
Mzee Mandela alikuwa rais wa Afrika Kusini tangu mwaka 1994 hadi 1999 na anatazamiwa na wengi kama baba wa taifa hilo kwa kupigana dhidi ya enzi ya utawala wa ubaguzi wa rangi.
Licha ya kufungwa kwa miaka mingi jela, Mandela alisema aliwasamehe maadui zake na kuwataka wananchi wa taifa hilo kushirikiana.
Alishinda tuzo ya amani ya Nobel mwaka 1993

WASITISHA MSAKO WA KONY

Joseph Kony
Serikali ya Uganda inasema kuwa imesitisha msako wake wa kiongozi mtoro wa waasi wa LRA Joseph Kony, katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati.

Uganda inasema imeamua kuchukua hatua hiyo kufuatia mgogoro wa kisiasa unaokumba taifa hilo baada ya rais Francois Bozize kung'olewa mamlakani.

Pia imeelezea kuwa serikali ya mpito inayoongozwa na kiongozi wa waasi imetatiza shughuli zao.

Uganda inasema kuwa wanajeshi wake katika eneo hilo ambako waasi walichukua mamlaka siku kumi zilizopita, watasalia katika kambi zao hadi muungano wa Afrika utakapotoa mwongozo.

Joseph Kony anayeongoza kundi la waasi wa LRA, anatakikana na mahakama ya kimataifa ya jinai kwa tuhuma za uhalifu wa kivita.

Anaaminika kujificha na wapiganaji wake katika misitu inayopakana na Jamuhuri ya Afrika ya Kati, Sudan Kusini na Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo.

AJALI MAENEO YA MAKUTANO YA SOKOTA

Ajali ambayo imetokea asubuhi hii katika makutano ya barabara ya sokota kati ya gari ndogo na pikipiki.

Katika ajali hiyo dereva wa pikipiki alifariki hapohapo na kuchukuliwa na askari.

Mwili wa dereva wa pikipiki ukiwa chini

Pikipiki iliyopata ajali

Wednesday, April 3, 2013

Bonta -Leta Badae

VIWANGO VIPYA VYA USAFIRI WA DALA DALA NA MABASI TOKA SUMATRA



Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imekamilisha mchakato na kuridhia viwango vipya vya nauli kwa ajili ya usafiri wa mijini na usafiri wa kwenda mikoani. Viwango hivi vipya vimefikiwa baada ya kufuata taratibu za kisheria na za kiutendaji ambazo SUMATRA kama msimamizi na mdhibiti wa sekta ya usafiri wa barabara inapaswa kuzifuata kabla ya kuridhia viwango hivyo. Viwango vipya vya nauli vitaanza kutumika kuanzia tarehe 12 Aprili, 2013.

SUMATRA ina wajibu kisheria kuhakikisha pamoja na mambo mengine kuwa maslahi ya watumiaji na watoa huduma za usafiri yanalindwa ili kuwepo na huduma endelevu ya usafiri ulio bora, salama na wenye kukidhi mahitaji.  Aidha SUMATRA ina jukumu la kujenga na kulinda mazingira mazuri na ya kuvutia kwa watoa huduma ili huduma ya usafiri inayotolewa inakuwa katika kiwango na gharama zinazoendana na huduma zenyewe.  

Katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2011/2012, SUMATRA ilipokea maombi rasmi kutoka kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri wa barabara yakiwemo makampuni ya usafirishaji abiria ya Cordial Transport Services P.L.C, Happy Nation Co. Ltd, ABC Trans na Mwesigwa Mtazaha Kazaula yakipendekeza mapitio ya viwango vya nauli za mabasi yanayotoa huduma za usafiri mijini (Daladala) na mabasi yanayotoa huduma katika Mikoa kufuatia ongezeko la gharama za uendeshaji kwa mujibu wa mawasilisho yao.

Wakati maombi ya wamiliki wa Daladala yalilenga katika kuongeza viwango vya nauli kwa 149% ya viwango vya sasa, wamiliki wa mabasi ya masafa marefu waliomba nyongeza kati ya 35% na 48.5%.

Kwa mujibu wa Kifungu Na 18 cha Sheria ya SUMATRA, 2001, SUMATRA iliwashirikisha wadau mbalimbali katika kujadili na kupata maoni yao kuhusu maombi ya wamiliki ya kuongeza viwango vya nauli kabla ya kufanya maamuzi ya mwisho.

Aidha Mamlaka iliridhia viwango vipya kwa mujibu wa kifungu cha 16  Cha Sheria ya SUMATRA ambacho kinaipa Mamlaka kufanya mapitio ya nauli mara kwa mara kwa kuzingatia gharama za kutoa huduma, maslahi ya watoa huduma, faida, maslahi ya watumia huduma ya kulipa nauli yenye uwiano na gharama za huduma inayotolewa.

Kwa kuzingatia hoja za waombaji, maoni ya wadau, uchambuzi wa menejimenti, haja ya kupunguza gharama zisizo za lazima za uendeshaji na udhibiti wa vitendo vya uvunjaji wa Sheria na taratibu za uendeshaji shughuli za usafirishaji, Mamlaka ya SUMATRA iliamua kuongeza viwango vya juu vya nauli za Daladala kwa wastani wa 24.46%.

 Aidha kwa mabasi ya masafa marefu, viwango vimeongezwa kwa 20.3% kwa mabasi ya kawaida,   16.9% kwa mabasi ya daraja la kati na 13.2% kwa mabasi ya daraja la juu.
 Mchanganuo wa viwango vipya vya nauli ni kama ifuatavyo:

1. Nauli za Daladala – Jiji la Dar es Salaam

Umbali wa Njia
Kiwango Kipya cha Nauli
Mfano wa Njia
Kilomita kati ya 0 – 10 (Na mipaka ya Jiji Kati)
Sh 400/=
Ubungo – Kivukoni
Kilomita kati ya 11 – 15
Sh 450/=
Mwenge – Temeke
Kilomita kati ya 16 – 20
Sh 500/=
Tabata Chang’ombe – Kivukoni
Kilomita kati ya 21 – 25
Sh 600/=
Pugu Kajiungeni – Kariakoo
Kilomita kati ya 26 – 30
Sh 750/=
Kibamba – Kariakoo

Mamlaka imeandaa majedwali kwa njia zote za Dar es Salaam. Majedwali hayo yanaweza kupatika katika tovuti yetu www.sumatra.or.tz

Nauli ya Mwanafunzi itakuwa Sh 200/= ambayo ni nusu ya nauli ya mtu mzima ya kiwango cha chini cha nauli ya Sh 400/=. Nauli hii itatumika kwa njia zote za Jiji la Dar es Salaam.

2. Nauli za Mabasi ya Masafa Marefu

Daraja la Basi
Nauli ya zamani kwa km-abiria
Nauli mpya kwa km-abiria
Mfano wa kiwango kipya cha nauli kwa baadhi ya njia

Basi la Kawaida kwa njia ya lami
Sh 30.67
Sh 36.89
DSM–Mbeya Km 833
Sh 30,700
Basi la Kawaida kwa njia ya vumbi
Sh 37.72
Sh 46.11
S/wanga-KigomaKm 551
Sh 25,400
Basi la hadhi ya kati (Semi Luxury
Sh 45.53
Sh 53.22
DSM–Mwanza Km 1,154
Sh 61,400
Basi la hadhi ya juu (Luxury)





li kuhakikisha kuwa kuna uwiano kati ya viwango vipya vya nauli na ubora wa huduma ya usafiri, Mamlaka imetoa maagizo kwa wamiliki wa mabasi ya masafa marefu kuboresha maeneo yanayohusiana na huduma ya usafiri kama ifuatavyo:
  1. Wamiliki wa mabasi kutokutumia wapiga debe katika kuuza tiketi za safari
  2. Wamiliki wa mabasi kuhakikisha wanafuata Kanuni za SUMATRA za Udhibiti wa Tozo na Nauli (SUMATRA Tarrif Regulations) ambazo zinahimiiza kuwepo kwa kumbukumbu sahihi za mahesabu ili kurahisisha mapitio ya viwango vya nauli
  3. Kufuata Sheria, Kanuni na Masharti ya Leseni ya usafirishaji abiria
  4. Kutoza nauli kwa mujibu wa daraja la basi lenye sifa kamili la daraja husika kama ilivyoainishwa katika Kanuni za Usalama na Ubora
Aidha kwa mabasi ya mjini, Mamlaka imetoa maelekezo yafuatayo:
  1. Kuhakiksha kuwa abiria wote wanapatiwa tiketi
  2. Kudhibiti vitendo vya ukiukwaji wa Sheria ikiwemo kutokamilisha safari maarufa kama kukata ruti, kubadili njia na unyanyasaji wa aina yoteyote kwa abiria 
  3. Kutokutumia wapiga debe
  4. Wafanyakazi wa mabasi kuvaa sare nadhifu wakati wote.
 Mamlaka ya SUMATRA inaendelea kuimarisha ushirikiano kwa kufanya kazi kwa karibu  na Mamlaka zingine kama Wakuu wa Mikoa, Serikali za Mitaa, Mamlaka za Miji, Polisi, TBS, TANROADS, Kamisheni ya Bima na wananchi kwa ujumla, katika kuleta mageuzi kamili ya utoaji wa huduma za usafiri wa barabara kwa kiwango cha juu.

 A.S.K. Kilima
KAIMU MKURUGENZI MKUU
2 Aprili, 2013

Tuesday, April 2, 2013

Kidum Feat. Rally Joe - Impanuro (Official Video)

KIJIWE UGHAIBUNI



By:Dj luke

Shaa - Lava Lava ( Official Video HD)

NAFASI ZA KAZI 900 UTUMISHI WA UMMA


NAFASI ZA KAZI 900 UTUMISHI WA UMMA

 
Kumb. Na EA.7/96/01/D/23
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki, pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi ya Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 944 za kazi kwa waajiri mbalimbali kama ifuatavyo:
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Katibu Mkuu wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa Kimataifa, Afisa Mtendaji Mkuu Wakala wa Vipimo, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo Jinsia na Watoto, Katibu Mkuu Wizara ya Kazi na Ajira, Katibu Mkuu Wizara ya mifugo na Uvuvi, Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Katibu Mkuu Wizara ya Sayansi na Technolojia, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi, Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Katibu Ofisi ya Rais Maadili, Katibu Tawala Mkoa Kagera, Iringa, Ruvuma, Mbeya, Mwanza, Shinyanga, Manyara, Dar es Salaam, Morogoro, Geita, Pwani, Mara, Kilimanjaro, Lindi, Singida, Tabora, Tanga, Katavi na Arusha,Mkurugenzi Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Mkurugenzi Halmashauri Manispaa Iringa, Songea, Shinyanga,Morogoro, Singida, Kigoma/Ujiji na Temeke, Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya Mufindi, Kyera, Rungwe, Mbeya, Chunya, Biharamulo, Bukoba, Muleba, Namtumbo, Songea, Morogoro, Makete, Mkuranga, Mbinga, Tunduru, Ukerewe, Sengerema, Ilemela, Busega, Maswa, Meatu, Shinyanga, Kishapu, Kilosa, Msalala, Rufiji, Rorya, Ruangwa, Lushoto, Mkinga, Mpanda, Monduli, Ngorongoro,Kigoma, Nachingwea, Rombo, Same, Singida, Urambo, Tabora, Babati, Mbulu, Simanjiro, Kiteto, Handeni, Pangani, Kibondo, Chamwino, Mtwara, Nanyumbu, Mpwapwa, Kongwa na Tandahimba. Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Njombe, Kibaha, Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) na TEMESA.

bofya hapa: http://www.ajiraonline.com/jobs/nafasi-za-kazi-900-utumishi-wa-umma/