Saturday, July 27, 2013

Majirani walonga kuhusu kiwanda cha bunduki Dar

Mtuhumiwa aliyekamatwa na polisi Julai 18 kwa tuhuma za kumiliki kiwanda cha silaha nyumbani kwake maeneo ya Kawe Mzimuni alifahamika na majirani zake kama fundi funguo.
Juzi, Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam ilitangaza kumshikilia mtu mmoja kwa tuhuma za kumiliki kiwanda cha kutengeneza silaha nyumbani kwake kinyume na sheria.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa kanda  hiyo,  Ally Mlege alisema  taarifa za uwapo wa kiwanda hicho walizipata baada ya kukamtwa kwa watuhumiwa wanne wa ujambazi.
Wakizungumza kwa masharti ya kutokutaja majina,  majirani hao walisema kijana huyo alikuwa akiishi katika nyumba ya familia pamoja na wazazi na  mkewe, na  alizoeleka mtaani kwa  jina la Makufuli na watu wengi walijua kutengeneza funguo ndio kazi yake iliyokuwa ikimpatia kipato.
Walisema alikuwa ni kijana wa kawaida na alikuwa akijumuika na vijana wengine wa mtaani kama kawaida na hawakuwahi kufikiria wala kuhisi alikuwa akijihusisha na biashara yoyote haramu katika nyumba hiyo ikiwamo  kumiliki  vifaa vya kutengenezea silaha kama SMG na Shotgun, zaidi ya ile ya ufugaji wa ngo’mbe  inayofanywa na familia hiyo
Wakielezea kukamatwa kwake mmoja wa majirani hao, alisema siku ya tukio majira ya saa sita mchana  waliona magari yakienda katika nyumba hiyo inayotazamana na Shule ya Msingi Kawe A na baadaye kuzuka purukushani zilizodumu kwa takribani  muda wa saa mbili.
Walisema baadaye  mtuhumiwa pamoja na mkewe walikamatwa kwa tuhuma hizo.
Walisema mtaa umekuwa kimya toka kutokee kwa tukio hilo kila mmoja akijaribu kutathimi ni kwa namna gani mtuhumiwa huyo aliweza kufanya biashara hiyo kwa siri ikiwa nyumba hiyo iko katika eneo la msongamano wa watu na pia karibu na uwanja ambao wanajeshi huwa wanafanyia mazoezi.
Jana nyumba aliyokuwa akiiishi mtuhumiwa  ilionekana kuwa kimya huku  mlango wa mbele ukiwa umefungwa, na nje kukiwa na zizi la ng’ombe.
Nyumba za jirani watu walioneka nje wakifanya shughuli zao kama kawaida,lakini wengi wao wakiwa makini kuongea .
Siku ya Jumanne Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam ilitangaza kumshikilia mtu mmoja kwa tuhuma za kumiliki kiwanda cha kutengeneza silaha nyumbani kwake kinyume na sheria.
Kaimu kamanda wa polisi wa kanda Maalumu ya Dar es Salaam Ally Mlege alisema  taarifa za kuwapo kiwanda hicho walizipa baada ya kukamtwa kwa watuhumiwa wanne wa ujambazi.

Source:Mwananchi

Mataifa jirani na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC yatakiwa kusitisha ufadhili wake kwa Kundi la Waasi la M23

Umoja wa Mataifa UN umetaka kumalizwa mara moja kwa ufadhili unaofanywa kwa Makundi ya Waasi ya nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC unaofanywa na mataifa jirani kitu kinachochangia kuendelea na vita Mashariki mwa Taifa hilo. Kauli hiyo imetolewa kwenye mkutano uliotishwa Jijini New York katika makao Makuu ya Umoja wa Mataifa UN ukiwa na dhamira ya kuangalia mbinu zinazofaa ili kumaliza machafuko yanayoendelea Mashariki mwa DRC kwa muda sasa. Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry ambaye aliongoza mkutano huo amesema wakati umefika sasa kwa mataifa yanayofadhili Kundi la Waasi la M23 waache kufanya hivyo mara moja kitu kitakachosaidia kupatikana kwa amani.
Kerry aliuambia mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UNSC nchi yake imekuwa ikisitikishwa na taarifa za Kundi la Waasi la M23 kuendelea kupatiwa ufadhili kutoka kwa nchi jirani na DRC.
Waziri huyo wa mambo ya Nje ambaye alikuwa Rais wa Mkutano huo amesema wakati umefika kwa pande zinazolifadhili Kundi la Waasi la M23 kijeshi kuacha kufanya hivyo kwa kuwa wanaushahidi unaothibitsha madai hayo.
Mkutano huo wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UNSC uliwaleta pamoja wanachama kumi na tano wa kudumu pamoja na Rwanda lengo likiwa ni kuhakikisha mkakati madhubuti unakuwepo kumaliza vita vya Mashariki mwa DRC.
Uingereza, Ufaransa na Mataifa mengine wameungana na Kerry kutaka ufadhili wowote wa kijeshi kwa Kundi la Waasi la M23 usitishwe mara moja kwa ajili ya mustakabali mwema wa eneo la Ukanda wa Maziwa Makuu ICGLR.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Ban Ki Moon ametoa wito kwa pande zote yaani Serikali ya Kinshasa na Waasi wa M23 kurejea kwenye meza ya mazungumzo huko Kampala yanayosimamiwa na ICGLR.
Ban amekiri mazungumzo ni moja ya njia muafaka kabisa kumaliza mapigano yanyoendelea kushuhudiwa Mashariki mwa DRC kati ya jeshi la Serikali la FARDC na Kundi la Waasi la M23.
Naye Mjumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika eneo la Ukanda wa Maziwa Makuu ICGLR Mary Robinson amekiri hatua ya kuendelea kufadhiliwa kwa Kundi la M23 inasikitisha na kuchochea machafuko zaidi.
Rwanda imekuwa ikinyooshewa kidole cha lawama kwa kuwasaidia Waasi wa M23 kupambana na Jeshi la FARDC na imesisitiza yenyewe inalengo la dhati kuhakikisha utulivu unakuwepo nchini DRC.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Louise Mushikiwabo amesema utulivu wa taifa hilo unategemea zaidi hali ya usalama katika nchi jirani ya DRC hivyo wao wanaunga mkono juhudi zinazochukuliwa kumaliza vita hivyo.

Thursday, July 25, 2013

Linah akizungumza kuhusu kubakwa



Source:http://millardayo.com/linah-2/

TRENI YAACHA NJIA NA KUANGUKA SPAIN YAUA 77

Ajali hiyo inasemekana kuwa kubwa kuliko ile ya Mlipuko wa Bomu wa Madrid mwaka 2004,ajali hiyo imesababisha vifo vya watu 77,na inawezekana ikaongezeka kutokana na baadhi ya sehemu hazifikiki.Treni hiyo ilikuwa na abiria wapatao200-218,Sehemu ambayo ajali imetoka ilikuwa na kona kali,treni ilikuwa ikitembea 108-200 km kwa saa,


ZIARA YA PAPA BRAZIL KATIKA PICHA

Papa Akiingia kwenye Ndege Rome tayari kwa safari ya Brazil

Papa ameshawasili Brazil akishuka kutoka kwenye ndege
papa akipokelewa na Mwenyji wake Raisi wa Brazil Dilma


Umati wa watu wakimkaribisha Papa



ufukweni Coppa Cabana kulikuwa kama hivi








Chumba atakacholala Papa

Tume Huru ya Uchaguzi Nchini Zimbabwe ZEC yatangaza kutoa vitambulisho kwa Waangalizi 20,000 wa Uchaguzi wa Urais

Mwenyekiti wa Tume huru ya Uchaguzi Nchini Zimbabwe Bi Joyce Kazembe 
ZEC imesema zoezi hilo la utoaji wa vitambulisho kwa waangalizi linakwenda sanjari na kutoa huduma kama hiyo kwa waandishi wa habari ambao watakuwepo nchini Zimbabwe kwa ajili ya kukusanya habari wakati wa uchaguzi na baadaye ya uchaguzi.
Makamu Mwenyekiti wa ZEC Joyce Kazembe akizungumza na waandishi wa habari pamoja na waangalizi hao amesema hadi sasa wameshatoa vitambulisho 18,000 kwa waangalizi wa ndani na vitambulisho 1,500 kwa waangalizi kutoka nje.
Kazembe amesema zoezi hilo lingali linaendelea na litafungwa rasmi siku nne kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huo uamuzi ambao umetolewa kwa kuwa Tume Huru ya Uchaguzi ZEC inataka ijue kabisa idadi ya vitambulisho ilivyotoa.
Tume Huru ya Uchaguzi ZEC imesema waangalizi ambao wamepewa vitambulisho hivyo watakuwa na ruhusa ya kuangalia kile kitakachokuwa kinafanyika kwenye vituo 9,650 vya kupigia kura vitakavyokuwa kwenye kata 1,958 nchi nzima.
ZEC imesema pia kila Ubalozi ambao upo nchini Zimbabwe umepewa nafasi zisizozidi tano za waangalizi wake huku pia Mashirika yote yasiyo na Kiserikali yakipewa fursa ya kufanya uangalizi pamoja na makanisa kutoka majimbo kumi.
Makamu Mwenyekiti wa ZEC amethibitisha hadi kufika sasa wameshatoa vitambulisho 294 kwa waandishi wa habari wa ndani huku waandishi 28 kutoka nje nao wakipewa ruhusa hiyo ya kuripoti uchaguzi huo.
Tume Huru ya Uchaguzi imeendelea kusisitiza waangalizi kutoka nchini Marekani na mataifa wanachama ya Umoja wa Ulaya EU hawataruhusiwa kushiriki kwenye zoezi hilo kutokana na wao kuiwekea vikwazo Zimbabwe.
Waangalizi ambao wameshawasili nchini Zimbabwe ni kutoka Umoja wa Afrika AU, Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC, COMESA pamoja na wengine ambao ni Mashirika yasiyo ya Kiserikali.

Uchaguzi Mkuu nchini Zimbabwe umepangwa kufanyika tarehe 31 mwezi Julai ambao kinyang'anyiro kikali kinatarajiwa kuwa kati ya Rais Robert Gabriel Mugabe anayetetea wadhifa wake dhidi ya Mpinzani wake Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai.

Urusi yatoa nyaraka za kumwezesha kuondoka Uwanja wa Ndege na kuvuka mipaka yake Mfanyakazi wa zamani wa CIA Snowden

Serikali ya Urusi imetoa nyaraka kwa Mfanyakazi wa zamani wa Shirika la Kijasusi nchini Marekani CIA Edward Snowden zinazomruhusu kuondoka katika eneo la Uwanja Ndege ambalo amekuwa akiishi tangu awasili akitoke China.
Shirika la Habari la Umma la Urusi RIA limethibitisha kupatiwa kwa nyaraka hizo kwa Snowden ambaye amekuwa akihaha kuomba hifadhi kipindi hiki akisakwa kwa udi na uvumba na Serikali ya Marekani baada ya kuvujisha siri za Shirika la CIA.
Nyaraka hizo zimetoa nafasi kwa Snowden kuweza kuingia nchini Urusi na kuomba hifadhi ay hata kuondoka na kueleka katika nchi yoyote ambayo itakuwa tayari kumhifadhi bila ya walinzi wa mpaka kumzuia.
Taarifa zinasema baada ya Snowden kupatiwa nyaraka hizo muhimu anatazamia wakati wowote ataondoka katika eneo la Uwanja wa Ndege wa Moscow alipokuwa anahifadhiwa sehemu ya abiria wanaopita nchi hiyo kueleka mataifa mengine.
Snowden amepata nyaraka hizo muhimu kutoka kwa usaidizi wa Mwanasheria wake Anatoly Kucherena ambaye amekwenda katika Uwanja wa Ndega wa Sheremetyevo kukutana na mteja wake.
Nyaraka hizo amekabidhiwa Kucherena ambaye ndiye atamkabidhi Snowden anayetajwa tayari ameshabadilishiwa hadi mavazi yake tayari kwa kuingia nchini Urusi na kuendelea na mchakato wa kuomba hifadhi ya kudumu.
Mwanasheria wa Snowden, Kucherena amesema iwapo mteja wake atakuwa tayari kupatiwa uraia wa Urusi atafanya kila linalowezekana ili kuhakikisha anapata nafasi hiyo ambayo huenda ikatolewa kwake bila pingamizi.
Mapema mwezi huu Snowden alijitokeza na kuomba hifadhi nchini Urusi ambapo aliambiwa mchakato wa yeye kupewa hadhi huyo huenda ungechukua hata kipindi cha miezi mitatu kabla ya kukubaliwa.
Mfanyakazi huyo wa zamani wa Shirika la Kijasusi la Nchini Marekani CIA Edward Snowden amekuwa akippata hifadhi ya muda nchini Urusi kitu ambacho kimechangia kuleta mgogoro wa uhusiano baina ya Serikali za Washington na Moscow.


William na Kate warejea nyumbani katika picha









Rais Kiir avunja baraza la mawaziri

Rais wa Sudan kusini,Salva Kiir
Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir, amelivunja baraza lake la mawaziri pamoja na kumfuta kazi makamu wa rais Riak Machar katika mabadiliko makubwa zaidi kuwahi kutekelezwa katika historia ya miaka miwili ya taifa hilo.
Aliyekuwa waziri wa habari, Barnaba Marial Benjamin, ameiambia BBC kuwa mawaziri wote kutoka kwa Makamu wa Rais Riek Machar wameondolewa.
Duru zinasema haijabainika iwapo kuna waziri yeyote miongoni mwa wale waliofutwa kazi atarejeshwa katika baraza jipya la mawaziri litakalobuniwa.
Pia hakuna sababu iliyotolewa kuhusiana na hatua ya rais kuwafuta kazi maafisa hao , lakini wadadisi wanasema kuwa Bwana Kiir na makamu wake Machar wamekuwa na mgogoro wa mamlaka kwa miezi kadhaa sasa.
Sudan Kusini imekumbwa na matatizo chungu nzima hasa ya kiuchumi tangu kujitenga na Sudan mwaka 2011.
Uthabiti wake umetatizwa na malumbano kati yake na Sudan kuhusu mipaka na swala la mafuta.
Hivi karibuni baadhi ya maafisa wa Bwana Kiir, wamekuwa wakizungumzia kuwepo minong'ono kuhusu uongozi wake.
Ripoti zinasema kuwa Kiir anajitahidi kusalia na ushawishi katika chama cha Sudan People's Liberation Movement (SPLM), ambacho kinathibiti serikali.
Kwa upande wake bwana Machar, ambaye mwezi Aprili alipunguziwa mamlaka, alisema huenda akagombea uongozi wa chama cha SPLM dhidi ya rais Kiir, kabla ya uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka 2015.
Kuvunja baraza la mawaziri ni dalili ya juhudi kubwa za rais kubadilisha sio tu serikali yake bali pia mamlaka na njia za kuingia madarakani nchini humo.

Ingawa mabadiliko yaliyotangazwa jana yamekuwa yakitarajiwa, wakati wa kutangazwa kwake ndio umeleta shaka na wasiwasi kuwa rais huenda anatumia mamlaka yake kubana upinzani na kuzuia mgawanyiko katika serikali yake.

IGP Mwema, Tendwa wakamia CHADEMA

JESHI la Polisi nchini na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, wanaonekana kuanza mkakati maalumu wa kukidhoofisha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa kuwaandama viongozi wake kuhusu ushahidi wa mlipuko wa bomu jijini Arusha na mpango wa kutaka kuanzisha kambi ya mafunzo ya ukakamavu kwa vijana kwa ajili ya ulinzi.
Kutokana na mlipuko huo wa bomu Juni 15 mwaka huu, eneo la Soweto jijini Arusha ulioua watu wanne na kujeruhi wengine zaidi ya 60 katika mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi mdogo wa madiwani, CHADEMA ilitangaza kuanza mpango wa kutoa mafunzo kwa vijana wake kwa ajili ya kulinda mikutano na viongozi wake.
Hata hivyo, msimamo huo wa CHADEMA ulitafsiriwa tofauti na Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jeshi la Polisi linaloongozwa na IGP Said Mwema, na Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa wakidai hatua hiyo ni kinyume cha sheria za nchi, katiba na sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992.
Kauli hizo zilipokelewa kwa mtazamo tofauti na wadau wa siasa nchini wakihoji jeshi hilo na Tendwa walikuwa wapi kwa kutoionya CCM yenye kikundi cha vijana cha Green Guard ambacho kinapewa mafunzo ya kijeshi kwa ajili ya shughuli za chama.
Licha ya vyombo vya habari kuonyesha picha kadhaa za mafunzo ya kikundi hicho cha CCM kikiwa na vijana wenye silaha, polisi na Tendwa wamekuwa na kigugumizi cha kuzungumzia jambo hilo badala yake wameendelea kuwatisha viongozi wa CHADEMA kuachana na mpango huo.
Katika suala hilo, Tendwa amekuwa na kauli za kujikanganya huku naye akikwepa kuizungumzia Green Guard wakati viongozi waandamizi wa polisi nao wamekuwa na ndimi mbili zinazokinzana kwenye suala hilo ambalo wamelibebea bango wakitaka kufifisha tukio la mlipuko wa Arusha.
Jumamosi iliyopita, gazeti hili lilichapisha barua iliyoandikwa na ofisi ya Tendwa kwenda kwa CHADEMA yenye kumb. Na RPP/CHADEMA/72/32 ikikiruhusu chama hicho kuanzisha vikundi vya ulinzi na usalama kama ilivyo katika katiba yao.
Ofisi hiyo ya msajili kupitia kwa Naibu Msajili, Sisty Nyahoza, jana ilitoa taarifa kwa vyombo vya habari ikikana kuwahi kutoa ruhusa kwa CHADEMA au chama chochote cha siasa kufanya mafunzo ya ukakavu au mafunzo ya kutumia nguvu ya aina yoyote kwa wanachama wake au mtu yeyote.
Hata hivyo, katika hali ya kuonyesha kuwa Tendwa anaibeba CCM, licha ya kutoa vitisho kwa CHADEMA kuwa atawachukulia hatua za kisheria endapo watashindwa au kukataa kutii agizo la kutoanzisha makambi hayo, hakusema chochote kwa chama tawala ambacho kinaendesha kambi za kujihami.
Julai 9 mwaka huu, CHADEMA kupitia kwa Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, walisema kufuatia mlipuko wa bomu Arusha, chama hicho kinakusudia kuanzisha kambi za mafunzo kwa vijana watakotumika kulinda viongozi katika shughuli zake kutokana na Jeshi la Polisi kushindwa kuchukua hatua stahiki.
Siku chache baadaye, Mbowe alivamiwa usiku wa manane nyumbani kwake na askari kadhaa wakidai kuwa walitaka awapatie ushahidi wa video ya mauaji aliyodai kuwa nayo ikiwaonyesha baadhi ya polisi walivyoshiriki kwenye tukio la mlipuko wa bomu Arusha.
Baada ya Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa kufichua tukio hilo kwenye mkutano wa hadhara kesho yake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura alidai hana taarifa za askari wake kufika nyumbani kwa Mbowe kumkamata.
Jeshi hilo kisha liligeuza hoja na kumtaka Mbowe ajisalimishe kwa ajili ya mahojiano kuhusu kauli yake ya kuhusu chama kutaka kuanzisha makundi ya mafunzo ya ukamamavu kwa vijana wao.
Julai 17 mwaka huu, Mbowe aliandikiwa barua akiamrishwa awasilishe ushahidi wa video aliyodai kuwa nayo, ikiwaonyesha baadhi ya polisi walivyoshiriki kwenye tukio la mlipuko wa bomu Arusha.
Wakati Mbowe akiamriwa kufanya hivyo kabla ya juzi saa nane mchana, jeshi hilo halijawahi kuwahoji Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Mwigulu Nchemba na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye ambao walinukuliwa wakidai wana ushahidi kwamba CHADEMA walijilipua wenyewe.
Juni 20 mwaka huu, Mkuu wa Mafunzo na Operesheni wa jeshi hilo, Paul Chagonja aliwaeleza wanahabari kuwa Mbowe anapaswa kuwa mkweli na kuacha kuuchezea umma kwani alichowaeleza polisi ni tofauti akisema hana ushahidi huo wa mlipuko wa bomu bali alielezwa na wafuasi wake.
Lakini katika hatua ya kushangaza, Chagonja huyo huyo ndiye amemwamuru Mbowe tena kupeleka ushahidi huo polisi akitamba kuwa baada ya kukaidi kufanya hivyo, polisi inao makachero wake wanaojua jinsi gani ya kuendelea na kazi hiyo.
Muda aliopewa Mbowe umemalizika bila kuwasilisha ushahidi huo, akidai kuwa hawezi kwenda kinyume na msimamo wa chama kwani walikwishamwandikia Rais Jakaya Kikwete, wakimtaka aunde tume huru ya majaji ndipo watapeleka ushahidi wao huo na mwingine.
Mbowe alisema kuwa jeshi hilo ni watuhumiwa, hivyo kamwe hawawezi kupeleka ushahidi huo kwao, na kukitaka chombo hicho cha dola kufungua kesi mahakamani ili CHADEMA wapeleke ushahidi huo huko.
Jana, Mbowe alijisalimisha tena polisi kama alivyokuwa ameamriwa, lakini hakupeleka ushahidi huo, na jeshi hilo lilimwamuru tena kupeleka ushahidi huo kwa maandishi Ijumaa wiki hii.


source:Tanzania Daima

Wednesday, July 24, 2013

TAHADHARI

Kuna taarifa ya utapeli hatari umeingia mjini..watu wanajifanya wanauza manukato(perfumes).Watakushawishi unuse kipande cha karatasi ambacho kimenyunyuziwa dawa yenye sumu ambayo ukinusa tu unaweza kujikuta umepoteza fahamu na hapo unawapa nafasi ya kuibiwa ulicho nacho.Tafadhari kuwa mwangalifu unapokutana na watu kama hao.

Mtumie ujumbe huu pia ndugu na rafiki yako na watu wote unaowajali .

Mkasi - SO6E03 with Jerry Silaa

Rais Kikwete atoa maelekezo kuhusu kodi ya simu za mkononi



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameagiza Wizara za Serikali zinahusika na kodi na mawasiliano pamoja na makampuni ya simu za mikononi nchini kukutana mara moja kutafuta jinsi gani ya kumaliza mvutano wa kodi mpya ya kadi za simu hizo za mikononi.

Rais kikwete ametoa maelekezo hayo jioni ya leo, Jumanne, Julai 23, 2013 wakati alipokutana na viongozi wa Wizara ya Fedha, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na wawakilishi wa makampuni ya simu ya TTCL, Airtel, Vodacom, Tigo na Zantel katika kikao cha pamoja kilichofanyika Ikulu, Dar es Salaam.

Rais Kikwete amesema kuwa lengo kuu la mkutano huo wa pamoja kati ya Wizara hizo za Serikali na makampuni ya simu yawe ya kupendekeza jinsi gani ya kuziba pengo la Sh. Bilioni 178 ambazo zitapotea katika Bajeti iwapo kodi hiyo kwa kadi za kuongelea za simu za mikononi italazimika kufutwa na Serikali kupitia marekebisho kwenye Muswada wa Fedha wa Bajeti ya Mwaka 2013/2014.

Rais Kikwete amewaambia wawakilishi wa pande hizo mbili kuwa huwezi tena kuifuta moja kwa moja kodi hiyo bila kutafuta njia nyingine za kupata fedha za kujaza pengo hilo la Sh. Bilioni 178 ambazo tayari Bunge limezipangia matumizi.
“Nawaombeni kaeni pamoja, wekeni bongo zenu pamoja, wekeni akili yenu pamoja tutafute namna gani tunaweza kujaza pengo hili la Sh. Bilioni 178 endapo tutakubaliana kuwa kodi hii inawabebesha wananchi mzigo mzito na kuwa pengine menejimenti ya kodi yenyewe ni ngumu,” Rais Kikwete amewaambia wawakilisho hao.

Katika Bajeti ya Serikali ya mwaka 2013/2014, Serikali imeweka kodi ya Sh. 1,000/= kwa mwezi kwa kila mtumiaji simu kwa ajili ya kufanya mawasiliano kwa kutumia simu ya mkononi.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu.

Dar es Salaam.

23 Julai, 2013

Tuesday, July 23, 2013

Sherehe London kwa kuzaliwa mwanamfalme


Tangazo la kuzaliwa mwana Mfalme likitolewa


Ujumbe wa heri njema umeendelea kutolewa kutoka kote duniani baada ya Kate na Prince William ambaye atakuwa wa tatu kwenye foleni katika kurithi ufalme wa Uingereza.

Mwanamfalme William na mkewe Kate ,wameamkia hospitalini asubuhi ya leo mjini London baada ya kupata mtoto wao wa kwanzaJumatatu jioni.
Mtoto huyo aliyezaliwa akiwa na takriban kilo tatu na nusu atafahamika kama mwanamfalme wa Cambridge, lakini hajapewa jina.

Katika taarifa fupi William,amesema wana furaha isiyo na kifani.
Baadaye leo jeshi la Uingereza linatarajiwa kutoa heshima kwa kuzaliwa mwanamfalme huyo kwa kurusha mizinga 40 hewani huko London na kengele la kanisa la Westminster Abbey zitalia.

Kawaida saluti ambayo hutolewa kwa mwanamfalme huwa ni mizinga ishirini na moja lakini huongezeka hadi arobaini na moja ikiwa itarushwa kutoka katika makao ya kifalme
Taarifa kutoka katika Kasri la Buckingham, zinasema kuwa Malkia Elizabeth na mumewe walifurahishwa sana na habari za kuzaliwa kwa mtoto huyo. Naye babake William
Prince Charles, alisema ana furaha isiyo kifani na ana raha sana kuwa babu kwa mara ya kwanza. 

Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron, alisifu sana kuzaliwa kwa mtoto huyo na kuitaja kuwa hatua muhimu sana kwa Uingereza.
Naye waziri mkuu wa Australia, Kevin Rudd, alitaja sherehe za jana kama muhimu sana kwa nchi za juimuiya ya madola, huku akiongeza kuwa watu wa Australia wanampenda sana Prince William baada ya kuzuru nchi hiyo akiwa mtoto mwenyewe.

Urine-Powered Fuel Cell Charges Mobile Phone

What do you think of the Bristol scientists’ experiment? Would you use a urine-powered fuel cell to charge your devices?

Thursday, July 18, 2013

Kodi ya kadi ya simu (SimcardTax): Maoni ya awali ya wananchi juu ya hatua za kuchukuliwa


Nawashukuru kwa maoni ambayo mmenitumia kuhusu hatua zinazopaswa kuchukuliwa kufuatia kuanzishwa kwa ushuru wa bidhaa kwa kadi za simu (sim card) kwa wamiliki wa simu za kiganjani/mkononi.

Bado naendelea kuchambua maelfu ya maoni yaliyotolewa katika mijadala na niliyotumiwa kwa barua pepe. Nitoe mrejesho wa awali kwamba kwa muktasari mapendekezo niliyoyachambua mpaka sasa yanapendekeza hatua zifuatazo kuchukuliwa: 

Kwanza, taarifa itolewe kwa wanahabari na umma yaliyojiri na yatokanayo na kupitishwa kwa kodi hiyo;

Pili, hatua zisiwe kwa kodi hii pekee yake bali zote zenye kuongeza gharama za maisha kwa wananchi.

Tatu; majina ya wabunge wanaodaiwa kutoa mawazo ya kupendekeza kodi hiyo kutozwa yatajwe;

Nne, muswada wa sheria upelekwe bungeni katika mkutano ujao kufuta kodi hiyo;

Tano, saini za wananchi zikusanywe kupinga kodi hiyo na kuwasilishwa bungeni au kwa Serikali;

Sita, Serikali itakiwe kusitisha utekelezaji wa kifungu husika cha sheria hiyo ili wananchi wasianze kubebeshwa mzigo huo wa gharama;

Saba, maandamano yaandaliwe kulaani kupitishwa kwa kodi hiyo na kutaka utozaji wa kodi hiyo usianze kutekelezwa;

Hatua ambazo tayari zimeanza kuchukuliwa:

Wakati nikiendelea na uchambuzi nimeanza pia kuchukua hatua namba moja mpaka tano. Nashukuru pia kwa upande wenu baadhi mmeanza kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kukusanya saini kupitia link hii:http://www.avaaz.org/en/petition/WITO_WA_KUSITISHA_TOZOKODI_YA_LAINI_YA_SIMU_KILA_MWEZI_KUFUATIA_MABADILIKO_YA_SHERIA_YA_KODI_2013/?aCqNffb Naunga mkono hatua hiyo iliyochukuliwa na nawahimiza wengine kuingia na kusaini. 

Aidha, natoa mwito kwa kila mwananchi aliyeguswa na suala hili kwa kutumia haki yake kwa kuzingatia wajibu muhimu kuwezesha hatua mbalimbali kuchukuliwa kwa kurejea mapendekezo yaliyotolewa.

Kwa upande wangu; Mosi, kupitia mkutano wa hadhara tarehe 13 Julai 2013 na njia nyingine niliendelea na mchakato ulionza kabla ya mkutano wa kumi na moja wa Bunge kuanza wa kukusanya saini za watu wanaotoa madai ya kutaka Bunge liisimamie Serikali kupunguza athari za ongezeko la gharama za maisha kwa wananchi na kudhibiti mfumuko wa bei nchini. Mpaka sasa zimeshafika saini 23569. 

Yeyote anayetaka kukusanya saini za wengine katika eneo lake naomba awasiliane na Afisa katika ofisi ya mbunge Gaston Garubimbi (0715/0767-825025) kwa ajili ya kutumiwa fomu.

Aidha, nitashiriki mkutano wa hadhara jumapili tarehe 21 Julai 2013 katika Uwanja wa Sahara kata ya Mabibo kuanzia saa 8 Mchana mpaka saa 11 Jioni. Hivyo, kwa wale mlio katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar Es Salaam mnaalikwa kuhudhuria mkutano huo ambapo mtapata pia fursa ya kusaini fomu tajwa.

Mkutano huo unalengo la kutoa mrejesho kuhusu yaliyojiri bungeni katika mkutano uliopita na kupokea masuala ya kuyawasilisha katika mkutano ujao. Aidha, uchambuzi utafanyika kuhusu rasimu ya katiba sanjari na juu ya mchakato wa katiba mpya. 

Pili, tarehe 15 Julai 2013 niliwasilisha kwa Katibu wa Bunge kusudio la kuwasilisha muswada binafsi wa sheria kuwezesha kufutwa kwa ushuru tajwa. Katika barua hiyo nimeomba masharti ya kanuni ya Kanuni ya 21(1) (d) (e) na (2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge yazingatiwe kuniwezesha kuchukua hatua hiyo katika Mkutano wa kumi na mbili wa Bunge uliopangwa kuanza mwezi Agosti 2013. Hivyo, yeyote ambaye angependa kujitolea 3M (Maarifa, Muda au Mali) kufanikisha maandalizi ya muswada huo awasiliane nasi kupitia barua pepe mbungeubungo@gmail.com. Maslahi ya umma Kwanza.

John Mnyika (Mb)
18 Julai 2013

PERUZI ZA MTANDAONI






Tuesday, July 16, 2013

Darfur tragedy: How they were attacked

Dar es Salaam. Fresh reports are emerging on the deadly attack on Saturday that claimed the lives of seven Tanzanian soldiers in Darfur, as Tanzania People’s Defence Forces (TPDF) forms a team of experts to investigate the mystery surrounding the incident.
The slain soldiers, who were part of the UN-Africa Mission in Darfur (Unamid) died on Saturday after gunmen ambushed a convoy comprising Tanzanian peacekeepers. Their 17 colleagues were seriously wounded in the incident described as the deadliest ever single attack on the international force in Sudan.
The unidentified assailants ambushed the convoy of the African Union and the United Nations Hybrid Operation in Darfur at Khor Abeche in southern Darfur, killing the seven Tanzanian soldiers instantly.
TPDF spokesman, Colonel Kapambala Mgawe, said on Sunday that a team of experts would travel to Khartoum and Darfur for talks with authorities over the attack.
Speaking from Sudan, a police officer who working in Nyala town, Darfur and who preferred anonymity for fear of reprimand toldThe Citizen yesterday that the attack occurred when the soldiers were on a search for UN vehicles which are said to have been stolen by a rebel group.
“The soldiers were in a normal patrol, but a week ago, unknown assailants attacked members of the army and disappeared with four vehicles without causing any injury,’’ he said, adding:
 “On Saturday our soldiers saw their vehicles parked somewhere, but when they moved to recover them, they were suddenly and viciously attacked.”
He described the incident as the biggest and that the surviving soldiers are engulfed in fear. “It is really traumatising here; I can tell you the rebels are fully armed with sophisticated weapons’’, said the police.
He added that of all the incidents he has witnessed while working as a security man, the one on Saturday was the most vicious.
As of yesterday, the TPDF was yet to reveal the names the fallen Tanzanians. Colonel Mgawe said the army was communicating with the UN in part of the process to bring the soldiers’ remains home. He, however, declined to give names.
“It is too early to divulge the names, but we are all set to receive their bodies which will be transported here by the UN,” he said.
Yesterday, Unamid spokesperson Chris Cycmanick, told The Citizen that plans to bring the bodies to Tanzania were underway and that by the end of the week, they would be in Dar es Salaam.

SourceThe Citizen

MKASI WITH VANESSA MDEE

Majambazi yateka mabasi mawili

Kagera. Kundi la watu wanaosadikiwa kuwa majambazi wameteka mabasi mawili ya abiria na kufanya uporaji katika Pori la Hifadhi ya Biharamulo Mkoani Kagera na kupora bunduki aina ya SMG iliyokuwa na askaRi aliyekuwa anasindikiza mabasi hayo.
Akithibitisha tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Philip Kalangi alisema majambazi wapatao kumi waliokuwa na silaha nzito za kivita asubuhi ya Jumatatu waliteka mabasi mawili ya abiria yaliyokuwa yakielekea katika majiji ya Arusha na Dar es Salaam.
Alisema silaha zilizoonekana eneo la tukio ambazo zilitumiwa na majambazi kujihami ni SMG sita na LMG mbili.
Kwa mujibu wa Kalangi, mabasi yaliyotekwa ni NBS lililokuwa likielekea Arusha na RS lililokuwa likielekea Dar es Salaam,ambapo kabla waliteka gari dogo na kulitumia kufunga barabara katika hali iliyoonekana lilikuwa limeharibika.
Katika tukio hilo, abiria mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Fredrick Rugaihura (47)mkazi wa mjini Bukoba alijeruhiwa shingoni kwa risasi, ambapo majambazi hao walipora mali mbalimbali za abiria zikiwemo fedha na simu.

Source:Mwananchi

Monday, July 15, 2013

PITIA VICHWA VYA HABARI MAGAZETINI LEO

MAGAZETI YA LEO









MAJINA YA ASKARI WA TANZANIA WALIOUWAWA DARFUR HAY HAPA

Majina ya askari saba wa Tanzania waliokufa muda mfupi uliopita kwenye shambulio la ghafla mjini Darfur yamepatikana.
Askari hao waliokufa ambao walikuwa kwenye vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa huko nchini Sudan ni Sajenti Shaibu Othuman, Koplo Oswald Chaula, Koplo Mohamed Juma, Koplo Mohamed Chikilizo, Pte. Rodney Ndunguru, Pte. Peter Werema na Pte. Fortunatus Msofe.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kwenye mtandao ni kwamba askari hao walikwenda kujaribu kumwokoa mwenzao (ambaye hakutajwa) ambaye alisemekana kutekwa na vikosi vya waasi nchini humo.
Wakati wakiwa wakijiandaa, ghafla wakazingirwa na askari hao waasi na kisha kushambuliwa kwa risasi hadi kufa.
Haikufahamika hali ya askari huyo ambaye alidaiwa kutekwa kama bado yu hai ama ni miongoni mwa waliokufa.
Mungu azilaze roho za askari wetu mahali pema peponi, Amina