Friday, March 7, 2014

MALARIA YAWA UGONJWA HATARI ZAIDI

Watafiti kutoka Uingereza na Marekani wanasema kuwa mabadiliko ya hali ya hewa huenda yakazua ongezeko kubwa la maambukizi ya ugonjwa wa Malaria kote duniani huku ugonjwa huo ukienea katika maeneo ya milimani barani Afrika na Amerika ya Kusini.
Katika matokeo ya utafiti yaliyochapishwa kwenye jarida la Science, wanasayansi hao wanasema hata ongezeko dogo katika viwango vya joto siku za usoni huenda likaongeza kwa mamilioni maambukizi ya malaria.

Mbu anayesababisha malaria.
Watafiti wamepata ushahidi kwamba mbu anayebeba kimelea kinachosababisha malaria wanaelekea katika nyanda za juu wakati viwango vya joto vikipanda.
Watu wanaoishi katika maeneo ya nyanda za juu wanakosa kinga na hivyo kurahisisha maradhi ya malaria kuenea.
Takriban watu milioni mia mbili ishirini kote duniani huambukizwa ukonjwa wa malaria.


Mbu aneyesababisha malaria

No comments:

Post a Comment