Monday, April 14, 2014

Madaktari wakuza 'uke' katika maabara

Madaktari nchini Marekani wamefanikiwa kuwatengezea wanawake wanne sehemu ya uke kwa njia ya kisayansi.
Walitumia mfano wa seli ya uke na mifupa ya mwili kuweza kukuza uke huo katika maabara kwa kuzingatia wastani na umbo la kila mwanamke.
Baada ya matibabu hayo, wanawake hao wote inaarifiwa walielezea kupata hisia sawa na kamilifu,matamanio, kuridhishwa wakati wa tendo la ndoa pamoja na kutopata maumivu yoyote wakati wa tendo la ndoa.
Wataalamu walisema kuwa utafiti wao, ambao matokeo yake yalichapishwa katika jarida la kisayansi la Lancet, ni mfano wa hivi karibuni wa nguvu za mbinu tofauti na za kisasa za matibabu.
Wanawake hao walizaliwa na uke ambao haukuwa umeumbika vyema yaani ulikuwa na kasoro ya maumbile , tatizo linalojulikana kama ‘vaginal aplasia.’
Matibabu ya kisasa kwa tatizo kama hilo la kiafya yanaweza kuhusisha upasuaji ambapo ngozi au sehemu ya utumbo inatumika.
Celi zilichukuliwa kutoka kwa kizazi cha kila wanawake hao ambacho kilikuwa na kasoro ya maumbile na kukuzwa katika maabara ili kuweza kuzaana.
Picha za kizazi cha wanawake hao zilitumia kuwarekebishia uke wao.
Hili bila shaka ni jambo geni katika sayansi ya matibabu na pia inatoa taswira ya mambo yatakavyokuwa katika siku za usoni.
Jambo la Kutumia celi za mwili kubadilisha maisha ya wagonjwa tayari limefanyika na kuwasiaidia wagonjwa kupata kibofu cha mkojo, mishipa ya damu na koo.
Sasa unaweza kuongeza kwenye orodha hiyo, uke na pua.

Kwa hisani ya BBCSWAHILI


GURUMO HATUNAYE TENA

DARAJA LA MTO MZINGA NA KONGOWE KIGAMBONI LAHARIBIKA VIBAYA

Kutokana na mvua kubwa zilizonyesha siku ya jumamosi na jumapili zimeleta athari kubwa kwa wakazi mbalimbali wa jiji la Dar es salaam,ambapo miundombinu na makaazi ya watu yameathiriwa vibaya na mvua hizo na kuacha baadhi ya familia kupoteza ndugu zao na kukatisha usafiri kutoka eneo moja kwenda jingine.
Hili nililishuhudia jana eneo la Mbagala(Darajani mzinga)ambapo jana asubuhi daraja hili lilikuwa linapitika kwa waenda kwa miguu peke yake na kuacha magari na bodaboda kubaki upande uliokuwepo .Pichani ni baadhi ya sehemu hizo korofi.

Wakazi wa Kongowe wakiangalia maafa yaliyoletwa na Mvua hizo

Roli Kubwa la Mafuta lililotumbikia likijaribu kuvuka kwenye Daraja hilo la Kongowe likitokea Kigamboni

Sehemu ia daraja iliyoondolewa na maji


Wananchi wakijaribu kuvuka kwenda upande wa pili wa daraja baada ya maji ya mto kupungua


Add caption


Kibao kikionyesha kuwa barabara hiyo imefungwa kwa muda


Hapa ni Darajani Mzinga sehemu yalipokuwa yakihifadhiwa mabomba ya gesi

Wachina waliokuwa wakiishi eneo hilo wakiokoa vitu vyao


Jinsi kulivyokuwa kukionekana


Mto Mzinga Umefurika


Umati wa watu wakijaribu kuvuka 

Umati wa watu wakijaribu kuvuka


Daraja limefungwa na wananchi wanapita kwa zamu upande mmoja




Friday, April 11, 2014

Ukraine yawatuliza wanaotaka kujitenga

Waziri Mkuu wa Mpito wa Ukraine
Waziri Mkuu wa mpito wa Ukraine Arsenity Yatsenyuk amewaambia viongozi wa eneo la mashariki mwa nchi hiyo kwamba amekusudia kuwaongezea madaraka zaidi kwenye eneo hilo.
Hata hivyo hajafafanua ni kwa kiasi gani atawapa mamlaka hayo na kwamba madaraka hayo kama yanaweza kuwaridhisha wakazi wa eneo hilo lenye viwanda la Mashariki mwa Ukraine ambalo linataka kujitenga.
Bwana Yatsenyuk ameutembelea mji wa Donetsk katika jitihada zake za kushughulikia msimamo wa waandamanaji wanaounga mkono Urusi ambao wameteka majengo ya serikali za mtaa na kutangaza uhuru kutoka nchi ya Ukraine.
Wanaharakati pia wameendelea kushikilia majengo ya serikali katika mji wa Luhansk.
Tayari Ukraine imeishutumu Urusi kwa kuchochea uvunjifu wa amani nchini Ukraine.


UN yatowa onyo kali kwa serikali ya Burundi

Umoja wa Mataifa umetuma onyo kali kwa Serikali ya Burundi na kuitaka kuchukua hatua za haraka kushughulikia vurugu za kisiasa na kuheshimu haki za binadamu. “Tuna imani kwamba serikali ya Burundi itazingatia haraka iwezekanavyo na kushughulikia (matatizo yote) yanayosababisha vurugu na ukiukwaji wa haki za bin adamu”, amesema msemaji wa Umoja wa Matiafa Stéphane Dujarric.
Aidha, umoja huo umebainisha kuwa endapo vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu na uchochezi wa vurugu vitaendelea, basi wahusika watawajibika mbele ya mahakama za kimataifa.
“iwapo hakutochukuliwa hatua, huku ukiukwaji wa haki za binadamu zikiendelea, hatutosita kuwachukuklia hatua za kisheria wahusika, na ikiwezekana wafikishwe mbele ya mahakama ya kimataifa wajibu tuhuma zinazowakabili”, ameendelea kusema Dujarric.
Mshauri maalumu wa Umoja wa Mataifa wa kitengo cha kuzuia mauaji ya kimbari, Adama Dieng yuko ziarani mjini Bujumbura, ambako atajadili hofu hio ya kutokea kwa mauaji ya kimbari na viongozi wa Burundi.
Onyo hilo ni miongoni mwa tahadhari ziliyokua zikitolewa hivi karibuni na Umoja wa Mataifa pamoja na balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa, Samantha Power.
Akiwa ziarani mjini Bujumbura hivi karibuni, balozi Samantha Power, aliwatajka viogozi wa Burundi kuheshimu uhuru wa kisiasa, na vilevile kuheshimu katiba ya nch, ambayo utawala unajaribu kuifanyiya marekebisho.
 Tunasisitiza kuheshimu katiba ya nchi, ambayo ni sheria mama ya Burundi, na vilevile kuheshimu haki za binadamu,” alisema Samantha Power baada ya mazungumzo na rais Pierre Nkurunziza.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, lilielezea aprili mosi wasiwasi wake, juu ya mvutano wa kisiasa unaoendelea nchini Burundi.
Katika tangazo liliyotolewa jana alhamisi, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, limeelezea kwa mara nyingine wasiwasi wake juu ya uhuru wa kujieleza na mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa vya upinzani na mashirika ya kiraia.
Wajumbe 15 wa baraza hilo, wameelezea wasiwasi wao juu “ya vitisho na kufungwa kiholela pamoja na machafuko yanayotekelezwa na vijana kutoka vyama vya kisiasa”.
Wajumbe hao wametoa wito kwa serikali ya Burundi kutowafumbia macho wafuasi wa chama tawala ambao wamekua wakijihusisha na maovu mbalimbali, mkiwemo unyanyasaji na ukiukwaji wa haki za binadamu.
Kwa wiki kadhaa Umoja wa Mataifa umepata taarifa za kuaminika za usambazaji wa silaha na sare za kijeshi kwa vijana wa chama tawala Imbonerakure, shutuma ambazo zimetupiliwa mbali na serikali ya Burundi.
Ni kweli kwamba kumekuwepo na matukio ya vurugu baina ya vijana wa vyama mbalimbali vya kisiasa na sio tu chama tawala. Pia hakuna hali ya kutokuwajibika kwa sababu uchunguzi unafanyika kuhusiana na matukio hayo na tunapenda kuwaambia wananchi na jumuiya ya kimataifa kuwa nchi ya Burundi haisanbazi silaha kwa vijana wa chama hicho tawala”, naibu msemaji wa rais wa Burundi, Willy Nyamitwe.
Burundi inapitia wakati huu mgogoro mkubwa wa kisiasa kutokana na mgawanyiko kati ya chama cha rais Pirrea Nkurunzia, chenye wahutu wengi na chama cha UPRONA, chenye watutsi wengi.
Bunge la Burundi lilikataa katikati ya mwezi wa machi kuidhinisha mswada wa sheria ya kufanya marekebiho ya katiba, ambayo kwa mujibu wa upinzani ingelisababisha taifa hilo kuingia katika dimbwi la machafuko ya kikabila kama yale yaliyoshuhudiwa katika miaka ya 1993-2006.
Vyombo vya sheria vya Burundi viliwahukumu hivi karibuni kifungo cha maisha jela wafuasi 21 wa chama cha upinzani cha MSD kwa kuwatuhumu kwamba “walianzisha vurugu wakitumia silaha”, baada ya makabiliano na polisi ambayo iliwakatila wasifanye mazowezi ya kukimbia, wakati vijana wa chama tawala wamekua wakifanya mazoezi hayo kila jumamosi.


Mkasi - SO8E13 With AY