Saturday, November 29, 2014

KERO BARABARA YA MBOZI CHANG'OMBE

Hii imekuwa kero sasa kwa watumiaji wa barabara ya Mbozi,Chang'ombe viwandani,
Imekuwa ni kama tabia ya kawaida kuwepo kwa mabwawa makubwa ya maji katika eneo maarufu la kilipokuwa kiwanda cha kutengeneza biskuti,
Chakushangaza ni kuwa barabara hiyo inatumiwa na viwanda vikubwa vilivopo katika eneo hilo
kama Azam,Konyagi,Kioo na vingine vingi ambavyo hatujavitaja.
Inasikitisha maana hata wafanyakazi wa viwanda hivyo pia ni waathirika wa tatizo hilo .
Wito wetu mamlaka inayohusika shughulikieni jambo hili ili kutatua kero hiyo.

Bwawa kubwa la maji machafu

Ni shida hata jinsi ya kuvuka kufika upande wa pili

Ona waenda kwa miguu wanavyopata shida kuvuka

baada ya kujaribu kuvuka gari hii ilinasa

Wasamalia wema wakienda kutoa msaada


Foleni ya magari yakisubiri kuvuka



No comments:

Post a Comment