Wednesday, November 5, 2014

LILE SAKATA LA MKE KUISHI NA WANAUME WAWILI ZAIDI YA MIAKA 8 LACHUKUA SURA MPYA



Mume halali Rogers Halinga wakiwa na mkewe juliana Hosea kwenye kikao cha ndugu wa mume kijijini Ishungu


Sakata la mke kuishi na wanaume wawili lachukua sura mpya baada ya kikao cha ndugu wa mume halali Rogers Halinga kuketi kikao Kijiji cha Ishungu Kata ya Ruiwa Mbarali Mkoani Mbeya na kumtaka Biton Mwashilindi kufanya mazungumzo nao kabla hawajafungua madai ya ugoni Mahakani na kudai fidia.

Kikao hicho kizito kilichofanyika nyumbani kwa Baba mzazi wa Rogers Halinga mzee Jason Halinga(95) Novemba mosi mwaka huu na kuhudhuriwa na ndugu lukuki na kumsikiza mke wa Rogers ili abaini ukweli juu ya mtoto aliyezua utata kuwa ni wa nani baina ya Rogers au Biton Mwashilindi.

Mwanamke huyo  a(22) akijikanganya mara kadhaa katika kikao hicho akidai kuwa mtoto huyo ni wa Rogers kwa kuwa aliondoka baada ya kutokea mapishano na mumewe akiwa na ujauzito wa miezi minne ndipo alipoanza mahusiano ya kimapenzi na Biton hadi siku anajifungua mwaka 2012 akiwa mikononi mwa Biton ndipo alipoamua kumwandikisha mtoto katika kadi ya kliniki na cheti cha kuzaliwa jina la Biton.

Huku ndugu wakihamaki kutokana na kauli hiyo na kwamba yeye atamke wazi mtoto ni wa nani ndipo Juliana bila aibu kwa Baba Mkwe Mzee Jason Halinga alijibu kuwa mtoto ni wa Biton Mwashilindi,ambapo alimkabidhi mtoto huyo mwishoni mwa mwezi Octoba kwa hiari na wala hakuporwa kama alivyotoa taarifa Polisi.

Kauli hiyo ya Juliana ililazimu kikao kupiga simu kwa mzazi wa Juliana anayeishi Lwanjilo wilayani Chunya kujua mustakabali wa kauli ya mtoto wao kwani ilidaiwa kuwa Biton aliwahi kwenda huko kujitambulisha kuwa yeye anaishi na mtoto wao na kwamba Biton hakujua kuwa Juliana aliwahi kuolewa kwani alidai kuwa yeye ni mwanafunzi wa VETA Mbeya na asimwambie kuwa yeye ni mwanandoa.

Baba mzazi wa Juliana Hosea Mwalukasa alidai kuwa ni kweli Biton alifika kwake lakini hakumpokea kwa kuwa alidai kuwa Juliana ni mke halali wa Rogers Halinga hivyo kama amezaa na Juliana amefanya kosa na kwamba atatozwa ugoni kwani Juliana hakuwahi kupewa talaka na Halinga.

Kikao hicho baada ya mvutano wa muda mrefu kiliamua kuwa endapo Biton anadai kuwa mtoto aliyezaliwa na Juliana aliyefahamika kwa jina la Zalida Biton(2) ni mtoto wake basi alipe fidia ya kuzaa na mke wa mtu kiasi cha shilingi milioni kumi au alipe n'gombe saba ili aweze kumkomboa mtoto wake na kwamba Juliana bado ni mke halali wa Rogers.

Kwa upande wake Biton Mwashilindi alidai kuwa hayuko tayari kulipa pesa hizo na kwamba yeye alikabidhiwa mtoto kihalali na Jeshi la Polisi Ocktoba 31 mwaka huu kituo kikuu cha kat mbele ya maafisa wa Jeshi la Polisi na kwamba hana kesi ya kujibu na kwamba anasubiri tu mtoto afikishe umri wa miaka saba ndipo amchuke.

Katika suala hili baadhi ya wadau wamelalamikia Jeshi la Polisi kwa kuamua  masuala ya kisheria katika vituo vya Polisi badala ya mamlaka za kisheria zipo kama mahakama kuliko uamuzi uliotolewa na hali hii husababisha baadhi ya wananchi kujichukulia sheria mkononi.

Wamedai kitendo cha kukabidhiwa mtoto Biton bila kuchukuliwa vipimo vya DNA bado hakujatutua mgogoro huu na kwamba bado suluhu katika ndoa hiyo hiyo itakuwa ni kitendawiri kisicho na majibu.

Kwa hisani ya Mbeya yetu

No comments:

Post a Comment