Tuesday, August 19, 2014

Ebola:Wagonjwa 17 wapatikana Monrovia


Mmoja wa wanaume waliovamia kituo hicho na kumbeba mgonjwa
Waziri wa habari wa Liberia Lewis Brown amesema kuwa wagonjwa wote 17 wa Ebola waliokuwa wametoweka kutoka kwa kituo cha kuwatenga na umma wamepatikana.
Kupatikana kwao imekamilisha idadi ya wote 37 waliokuwa katika zahanati iliyovamiwa na wenyeji jumamosi iliyopita.

Waziri Brown ameviambia vyombo vya habari kuwa wote walijipeleka katika hospitali kuu ya JFK katika mji mkuu wa Monrovia.
Wagonjwa 37 walikuwa katika kituo hicho cha Ebola kilichoko karibu na kitongoji cha WestPoint Viungani mwa mji mkuu wa Monrovia kabla ya wenyeji kukivamia na kuwaachilia huru wagonjwa waliokuwemo kabla ya kukipora.
Awali waziri huyo alielezea kutamaushwa kwake na wizi huo ambao alisema ni jambo la kipuzi kujishirikisha na wagonjwa wa Ebola ilihali watu wengi tu wamepoteza maisha yao.
'' tukio hilo la WestPoint ni la kuvunja moyo sana maanake inahujumu juhudi zetu zote za kuzuia kuenea kwa homa hii ya Ebola,natumai tutarekebisha hali hii'' alisema bwana Brown.
20 waliosalia wako katika zahanati mbalimbali karibu na mji mkuu Monrovia .
Zahanati moja inaendeshwa na Hospitali kuu ya John F. Kennedy ilihali wengine wako katika zahanati ya ELWA nje ya mji huo.
Wote hao watachunguzwa kabla ya hatua madhubuti kuchukuliwa kwa maslahi ya Umma.
Katika hatua ya kushtua sana wakaazi wa vitongoji vya mji wa Monrovia walivamia zahanati hiyo iliyokuwa ikitumika kama kituo cha kuwatenga wagonjwa wa homa ya Ebola wakaipora na kuwaruhusu wagonjwa kutoroka.
''Kwa sasa tunashughulikia hali hii ilivyo kwani watu sasa wamerejea miongoni mwa jamii na hivyo kueneza maambukizi zaidi''
Zaidi ya watu 17 bado hawajulikani waliko baada ya kutoroka kutoka kituo cha kuwatenga wagonjwa wa Ebola.
''Kufuatia uvamizi huo tumejifunza mengi ''
Ajabu ni kuwa watu walikuja ndani ya kituo hicho walijileta huko wenyewe kwa hivyo sisi tunachukulia kuwa labda wagonjwa hao walitaka kusalia huko lakini wakalazimishwa kutoroka kukimbilia maisha yao kwa sababu wavamizi walikuwa wanapora mali ya Westpoint.
Brown alisema kuwa kwa sasa zahanati hiyo ya Westpoint Imefungwa lakini kuna mipango ya kuifungua tena.
''Tunafahamu kuwa kuna watu ambao bado wanashauku iwapo Ebola ipo ama hakuna lakini ukitizama takwimu kutoka jimbo la Lofa utaona kuwa idadi ya wahasiriwa imeanza kupungua.''
Lofa ndiyo iliyokuwa kitovu cha mlipuko ulioko sasa wa homa hii ya Ebola.
Zaidi ya watu 17 bado hawajulikani waliko baada ya kutoroka kutoka kituo cha kuwatenga wagonjwa wa Ebola.
Taharuki ilitanda kote nchini humo ,baada ya kituo kilichotengwa na kuwekewa kwa sababu ya kutoa matibabu kwa wagonjwa wa Ebola, kilishambuliwa na zana kuporwa katika mji mkuu wa Liberia, Monrovia.
Watu 37 waliowekwa hapo kuangaliwa kama wana dalili za Ebola walitoroka baada ya kituo hicho kuporwa Jumamosi usiku.
Washambuliaji walipora magodoro na vitu vingine.
Mafisa wakuu nchini Liberia wanajaribu kuwatafuta wagonjwa waliotoroka ili kuwarejesha tena kwenye kituo hicho.

Watu zaidi ya 400 wamekufa kwa sababu ya ebola nchini Liberia kati ya zaidi ya 1,000 katika kanda ya Afrika Magharibi.

Mkasi | SO9E09 with Dudubaya