Monday, September 22, 2014

Maandamano makubwa yaanza Hong kong



Maelfu ya wanafunzi mjini Hong Kong wameanza maandamano ya juma moja kupinga mpango wa serikali ya Uchina ya kuwakagua wagombea wa uchaguzi wa kiongozi wa eneo hilo.
Wengi waliandamana katika chuo kikuu cha Uchina kilichopo mjini humo.
Waliishtumu Uchina kwa kukiuka makubaliano ya kidemokrasia wakati Uingereza ilipoikabidhi uchina eneo hilo mnamo mwaka 1997.
Walimu 300 wa chuo hicho pia wanaunga mkono maandamano hayo,ambayo yanalenga kuanzisha kampeni kubwa ya uasi wa raia.
Uchina imekubali kufanya uchaguzi wa moja kwa moja mnamo mwaka 2017,lakini ina uwezo wa kuwachagua wagombea wachache wanaounga mkono Uchina.
Mkutano mkubwa zaidi umepangwa kufanyika mwezi ujao na kundi la Occupy Central ambalo limeahidi limeahidi kufanya maandamano makubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa HOng kwa niya ya kufunga eneo lote la katikati ya jiji hilo.


Raia 115 wa Afrika ya Kusini walifariki Nigeria

Serikali ya Afrika Kusini inasema kuwa watu miamoja na kumi na tano wengi wao wakiwa raia wa Afrika Kusini, walifariki baada ya kanisa kuporomoka nchini Nigeria.
Ndege iliyowabeba manusura wa mkasa huo, kumi na sita kati yao wakiwa wamejeruhiwa vibaya, imewasili mjini Pretoria.
Zaidi ya watu 300 kutoka Afrika Kusini walikuwa wametembelea kanisa hilo la 'All Nations in Lagos', ambalo linaongozwa na mhubiri T.B. Joshua.
Inaarifiwa jengo hilo liliporomoka kutokana na ujenzi mbovu.

Mhubiri TB Joshua, amezua wasiwasi baada ya kuzungumzia kuona ndege iliyokuwa inazunguka juu ya kanisa hilo kabla ya jengo lenyewe kuporomoka.

KINANA AKITOA MAONI YAKE KWA WAANDISHI JUU YA MUUNGANO WA SCOTLAND

Saturday, September 20, 2014

Kansiime Anne - Traditional Marriage

Churchill show Episode 50

Balozi Sefue afunguka Katiba Mpya

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue amesema hakuna uwezekano wa kubadili muundo wa muungano kutoka Serikali mbili kwenda Serikali tatu katika mchakato wa Katiba.
Kauli ya Balozi Sefue imekuja ikiwa ni siku chache tangu Rais Jakaya Kikwete kukutana na viongozi wa Kituo cha Demokrasia (TCD) na kutoa uamuzi wa kuahirisha mchakato wa Katiba hadi baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Suala la muundo wa muungano lilichukua mjadala mkali ndani ya Bunge Maalumu la Katiba huku wajumbe wanaounda kundi la Ukawa wakiunga mkono mapendekezo ya Rasimu ya Katiba ya muundo wa Serikali tatu na wajumbe wa CCM wakisisitiza muundo wa Serikali mbili.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili, Balozi Sefue alisema mchakato wa Katiba unahitaji maridhiano, lakini suala la muundo wa muungano halina maridhiano katika jamii hivyo litachelewesha upatikanaji wa Katiba:
“Katika historia ya nchi yoyote, wakati unafika wananchi wakawa na maridhiano fulani, wakaamua kuyaingiza ndani ya Katiba. Tatizo linajitokeza pale watu au makundi fulani yanapong’ang’ania kuingiza ndani ya Katiba mambo ambayo ni dhahiri hayana maridhiano ndani ya jamii. Mfano ni suala la muundo wa Muungano,” alisema na kuongeza:
“Uzoefu wa Bunge Maalumu hadi sasa ni kuwa hakuna uwezekano wa kupata maridhiano ya kubadili muundo wa Muungano kutoka Serikali mbili kwenda tatu. Hutapata maridhiano hayo ndani ya Bunge Maalumu na hutapata maridhiano ukienda kwa wananchi,” alisema.
Alisema anaamini wajumbe wa Bunge Maalumu walifanya uamuzi wa busara kuliweka kando jambo hilo linalotugawa, na kuendelea kujadili Rasimu ya Katiba kwa msingi wa mfumo uliopo wa Serikali mbili,” alisema.
Balozi Sefue aliongeza kuwa tangu suala hilo liwekwe kando kumekuwa na kasi na matumaini ya kupata Katiba Mpya.
Alisema jambo hilo ni kubwa na uzoefu unaonyesha lina uwezo mkubwa wa kutugawa na kuchelewesha kupatikana kwa Katiba Mpya.
Balozi Sefue alisema Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliamini yatapatikana maridhiano kuhusu kubadili muundo wa Muungano, ilivyo sasa, ni wazi kuwa maridhiano kuhusu mabadiliko hayo hayapo na hayatapatikana.
“Hakuna idadi ya makongamano na maandamano yatakayobadili hali hiyo sasa,” alisema.
Licha ya kusema kuwa kuna matumaini ya kupata Katiba Mpya, Balozi Sefue alisema ikishindikana Katiba iliyopo itafanyiwa marekebisho ili ituvushe hadi mchakato utakaporejeshwa tena.


RAISI WA UEFA AGOMA KURUDISHA SAA

Rais wa shirikisho la soka barani Ulaya UEFA Michel Platini
Rais wa shirikisho la soka barani Ulaya UEFA Michel Platini amesisitiza kuwa hatorejesha saa yenye thamani ya Yuro elfu kumi na sita aliyopewa kama zawadi na shirikisho la soka nchini Brazil CBF.
Shirikisho la soka duniani FIFA limewataka maafisa wote waliopewa saa hizo katika kombe la dunia kuzirudisha kwa kuwa zawadi hizo zinakiuka maadili ya sheria za FIFA.
Lakini Platini mwenye umri wa miaka 59 amesema yeye hawezi kurudisha zawadi.
Platini amesema kuwa FIFA ilikuwa na habari kwamba zawadi hizo zilitolewa mnamo mwezi juni ,lakini akashangazwa ni kwa nini shirikisho hilo halikuchukua hatua wakati huo.

Saa hizo zilitolewa na mmoja ya wafadhili wa shirikisho la soka

RATIBA YA EPL WIKIENDI HII


UFARANSA YAFANYA MASHAMBULIO DHIDI YA DOLA YA KIISLAMU

Ikulu ya Ufaransa imetangaza ijumaa wiki hii kwamba ndege zake za kijeshi zimeshambulia kwa mara ya kwanza ngome za wapiganaji wa Dola la Kiislam kaskazini mashariki mwa Iraq.

Ufaransa inashiriki katika vita vingine dhidi ya wapiganaji wa Dola la Kiislam nchini Iraq na Syria, baada ya kutuma wanajeshi wake nchini Mali na Jamhuri ya Afrika ya Kati. Ufaransa ni taifa la pili lenye nguvu duniani kuingia katika vita nchini Iraq, ikiiunga mkono Marekani katika vita vyake dhidi ya wapiganaji wa Dola la Kiislam.
Tangazo hilo la Ikulu ya Paris limebaini kwamba mashambulizi ya kwanza yameendeshwa katika baadhi ya maeneo mapema ijumaa wiki hii. Ndege za kijeshi zimekua zikilenga ngome za wapiganaji wa Dola la Kiislam kaskazini mashariki mwa Iraq.
Tangazo hilo limethibitisha kwamba ghala la vifaa vya kijeshi vya wapiganaji wa Dola la Kiislam limeteketezwa na mashambulizi hayo, huku likibaini kwamba mashambulizi hayo yataendelea hivi karibuni. Ndege hizo ziliyoendesha mashambulizi hayo zimerejea kwenye vitu vyao viliyotengwa katika mji wa Abou Dhabi kwenye umbali wa kilomita 1500 na eneo lililoshambuliwa.
Kwa mujibu wa wizara ya ulinzi, operesheni dhidi ya wapiganaji wa Dola la Kiislam imeendeshwa katika jimbo la Mossoul, nchini Iraq. Mashambulizi hayo yameendeshwa na ndege mbili za kijeshi ambazo zimekua zimebeba mabomu aina ya GBU 12, na aina nyingine ya ndege yenye chapa C-135FR pamoja na ndege nyingine ambayo imekua ikisaidia kupiga doria kwenye bahari Atlantic 2.
Mashambulizi hayo ya anga yametekelezwa chini ya uongozi wa jeshi la Ufaransa kwa ushirikiano na viongozi wa Iraq pamoja na washirika wa Ufaransa katika jimbo hilo, wizara ya ulinzi imebaini .
Alhamisi wiki hii katika mkutano na waandishi wa habari, rais wa Ufaransa François Hollande, alibaini kwamba muda umewadia wa kuanzisha mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa Dola la Kiislam.

Uhuru Kenyatta atakiwa mahakamani ICC 8,Octoba


Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) imemtaka raisi wa Kenya Uhuru Kenyatta kufika mahakamani tarehe 8 mwezi Oktoba licha ya majaji wanaotarajiwa kusikiliza kesi dhidi yake kuiahirisha.
majaji katika mahakama hiyo wanataka kumhoji juu ya madai kwamba serikali yake imeficha hati iliyoombwa na waendesha mashitaka wanaosikiliza kesi yake ya uhalifu dhidi ya ubinadamu.
Kesi hii imekuwa ikicheleweshwa mara kadhaa sasa.hata hivyo raisi kenyata amekanusha kuandaa mauaji ya kikabila baada ya uchaguzi mwaka 2007.
Takribani watu elfu moja mia mbili waliuawa na laki sita kuyakimbia makazi yao.

Wiki mbili zilizopita, waendesha mashitaka waliomba kesi dhidi yake kuahirishwa kwa muda usiojulikana, kwa vile hawakuwa na ushahidi wa kutosha kwa sababu ya serikali ya Kenya kuweka vizuizi.

Friday, September 19, 2014

Ebola:MAAFISA WA AFYA WALIUAWA

Viongozi nchini Guinea wamesema tayari wamepata maiti kadhaa za timu ya wahudumu wa afya pamoja na wanahabari waliotoweka walipokuwa wakiendeleza harakati za kuwaelimisha na kuwahamasisha wananchi kuhusu ugonjwa wa Ebola.
Msemaji wa serikali ya Guinea amesema kati ya miili hiyo ni ile ya wanahabari watatu wa timu hiyo.
Timu hiyo ilisemekana kupotea baada ya kushambuliwa hapo jumanne katika kijiji kimoja kilicho karibu na Mji wa Nzerekore ulio kusini mwa Guinea.
Mlipuko wa Ugonjwa huo ndio hatari zaidi kote duniani kwa sasa, huku viongozi wakitahadharisha kwamba huenda watu zaidi ya 20,000 wakaambukizwa.
Timu hiyo ya madaktari watatu na wanahabari watu walipotea baada ya kushambuliwa kwa mawe na wakaazi wa kijiji cha Wome, walipofika katika kijiji hicho kilicho karibu na mahala ambapo mlipuko wa Ebola ulianzia.
Kwa mujibu wa mwanahabari mmoja aliyeweza kunusurika aliwaambia wanaripota kwamba alipokuwa amejificha, aliweza kusikia wakaazi hao wa Wome wakiwatafuta.
Wajumbe wa serikali wakiongozwa na Waziri wa Afya walitumwa maeneo hayo lakini hawangeweza kufika kwa kutumia barabara kwani daraja lilikuwa limewekwa vizuizi.
Hapo Alhamisi msemaji wa serikali ya Guniea Albert Damantang Camara alithibitisha kwamba maiti nane zilikuwa zimepatikana na miongoni mwa hizo zilikuwa zile za wanahabari watatu.
Alieleza ya kwamba miili hiyo ilipatikana katika pipa moja la shule ya msingi iliyo katika kijiji hicho, na kuongeza kuwa timu hiyo iliuawa kinyama na wakaazi hao.

 kwa hisani ya bbcswahili.com

Mkasi | SO9E11 With Zitto Kabwe Extended Version

KILICHOTOKEA JANA KWA WAANDISHI WA HABARI



KWA HISANI YA ITV

NI MTIKISIKO

MTIKISIKO mkubwa wa kisiasa jana umelikumba taifa, baada ya wafuasi wa Chadema kupambana na polisi katika maeneo mbalimbali.
Hali hiyo, ilianza kuonekana mapema jijini Dar es Salaam, wakati Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe aliwapowasili Makao Makuu ya Jeshi la Polisi saa tano asubuhi kwa ajili ya kuhojiwa.
Mbowe aliitwa kuhojiwa na viongozi wa jeshi hilo kwa madai ya kutoa kauli za uchochezi wiki iliyopita.
Akizungumza kwenye mkutano wa Kamati Kuu ya chama chake, Mbowe alisema wataitisha maandamano na migomo isiyokuwa na kikomo nchi nzima kuishinikiza Serikali kusitisha Bunge Maalumu la Katiba linaloendelea mjini Dodoma.
Mbowe aliwasili polisi saa 5 asubuhi akisindikizwa na msafara wa magari matano yaliyobeba baadhi ya wanachama, mawakili na viongozi wa chama hicho.
Baada ya kuwasili katika eneo hilo, wanachama hao walipinga kiongozi wao kushuka ndani ya gari hadi atakapoingia ndani ya lango kuu.
Wanachama hao walisikika wakisema ‘Peoples’ huku wengine wakiitikia ‘Power’.
Kitendo hicho kilipingwa na polisi waliokuwa wakilinda lango hilo na kuamuru Mbowe ashuke na kuingia kwa miguu ndani ya jengo hilo.
Kitendo hicho kilionekana kuwakera wafuasi waliokuwa wamekusanyika eneo hilo na kuamua kusukuma lango hilo kwa nguvu ili waweze kuingia pamoja na kiongozi wao.
Kutokana na hali hiyo, wafuasi hao waligoma na kuanza kupambana na polisi ambao nao walijihami kwa kuzuia geti la lango wakiwa ndani.
Baada ya mabishano ya muda mrefu, ndipo polisi walipokubali Mbowe aingie na gari ndani ya jengo hilo huku wakizuia msafara wa magari mengine.
Kutokana na uamuzi huo, mawakili walilazimika kushuka ndani ya gari.
Mmoja wa askari aliyekuwa getini hapo, alisikika akisema anayepaswa kuingia ndani ya jengo ni Mbowe na mawakili wake.
“Tumekubaliana gari linaloingia ndani ni moja tu la mwenyekiti, msilazimishe matumizi ya nguvu,” alisikika akisema askari huyo.
Kitendo hicho kilipingwa na wanachama hao huku wakitaka wabunge, mawakili na viongozi wengine waingie ndani.
Kutokana na hali hiyo, polisi walikubali na kuwaruhusu viongozi hao kuingia ndani huku wakiwaamuru wanachama wengine na waandishi wa habari kusimama umbali wa mita 200 kutoka kwenye lango hilo.
Baada ya kutokea kwa tangazo hilo, wafuasi hao walikaidi amri hiyo na kusababisha askari D. D. Zahoro kuamuru kutumika nguvu kuwatawanya pamoja na waandishi wa habari hali iliyosababisha kujitokeza kwa vurugu katika eneo hilo.
Vurugu hizo zilidumu kwa muda wa saa moja na kusimamisha shughuli mbalimbali zinazoendelea ndani ya jengo hilo na njia kufungwa kwa muda.
Katika vurugu hizo,wafuasi  wanne wa chama hicho walikamatwa.
MWANDISHI APIGWA
Katika tukio hilo, mwandishi wa habari wa Gazeti la Tanzania Daima, Josephat Isango alijikuta akishambuliwa vibaya na askari kwa virungu.
Licha ya Isango kuonyesha kitambulisho, polisi hawakutaka kumsikiliza zaidi ya kuendelea kumshushia kipigo na kumsababishia maumivu katika mguu wa kulia.
Kipigo hicho kilisitishwa baada ya waandishi wengine kupiga kelele kuwaomba polisi kumwachia kwa sababu  alikuwa kwenye majukumu yake ya kazi.
MBOWE AHOJIWA
Wakati tukio hilo likiendelea, Mbowe alikuwa ndani ya jengo hilo akiendelea kuhojiwa  akiwa na mawakili wake sita.
Mawakili hao, ni Peter Kibatala, Profesa Abdallah Safari, Mabere Marando, Nickson Tugala, Tundu Lissu na John Malya.
Mahojiano hayo yalianza saa tano na kudumu kwa zaidi ya saa nne. Ilipofika saa 8:49 mchana, mawakili wanne wakiongozwa na Lissu walitoka nje na kuzungumza na wafuasi na waandishi wa habari.
“Mwenyekiti yuko salama, aliitwa kwa ajili ya mahojiano na yamefanyika vizuri chini ya mawakili.
“Polisi wameomba tuzungumze na nyie tuwaombe muondoke kwa sababu mwenyekiti akitoka na mkiwa wengi kunaweza kukawa na uvunjifu wa amani,” alisema Lissu.
Baadhi ya wanachama hao walisikika wakisema hawawezi kuondoka kwa sababu hawawaamini polisi.
“Sisemi nawaamini polisi au la, tumekubaliana kwamba mwenyekiti atapata dhamana, hivyo haitakuwa busara tukiondoka kwa maandamano, tulikuja kwa amani hatutaki mtu atoke hapa akiwa amedhurika,” alisema Lissu.
Baadhi ya wafuasi walikubali kuondoka huku wengine wakibaki.
Saa 9:17 alasiri, Mbowe alitolewa kwa kupitia mlango wa nyuma wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, huku akisindikizwa na magari manne kwenda Kituo cha Polisi Kati ambako  aliachiwa kwa dhamana.
MTIKILA
Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila alifika eneo hilo akiwa kwenye bajaj, lakini alizuiwa kuingia ndani.
DODOMA
Polisi mjini Dodoma, jana waliimarisha ulinzi kwa ajili ya kupambana na wafuasi wa Chadema waliopanga kuandamana kupinga Bunge Maalumu la Katiba linaloendelea mjini humo.
Miongoni mwa maeneo yaliyokuwa na ulinzi mkali ni pamoja na jengo la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Viwanja vya Nyerere Square na mitaa mbalimbali ya mjini hapo.
Polisi waliweka uzio wa kamba kilipo Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) na makutano ya barabara jirani na stendi ya mabasi ya abiria yanayokwenda mikoani ili kutoruhusu watu na magari kuelekea eneo la Bunge.
Jengo la Bunge lilikuwa limezungukwa na askari wengi wenye silaha, farasi na mbwa kuhakikisha usalama unakuwapo katika eneo hilo.
Ndani ya eneo la Bunge, nako ulinzi ulikuwa mkali kwani kulikuwa na idadi kubwa ya askari waliokuwa na silaha pamoja na mbwa.
Viwanja vya Nyerere
Katika viwanja vya Nyerere ambako wakazi wa Dodoma hupenda kukusanyika kwa ajili ya kupumzika na kupata huduma za chakula na vinywaji, jana shughuli zilisimama kwa muda kwa kuwa polisi walikuwa wameweka ulinzi tangu asubuhi.
Nje ya viwanja hivyo, kulikuwa na vijana waliokuwa na mabango likiwamo lililosomeka ‘Sitta tumia busara ahirisha Bunge la Katiba’.
Katika viwanja hivyo, polisi walionekana wakiwa wamekamata vijana wapatao kumi waliodaiwa kuwa walikuwa wakitaka kuandamana.
Wakati hali ikiwa hivyo katika maeneo hayo, ulinzi pia uliimarishwa katika mitaa mbalimbali ya mji huo kwani askari polisi waliokuwa na silaha na askari kanzu, walikuwa wametanda kila kona.
Chini ya ulinzi huo, magari yaliyokuwa yamejaa askari polisi yakiwamo ya askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), yalikuwa yakizunguka kila kona kuhakikisha hakuna maandamano yatakayofanyika.
Gari la Chadema
Pamoja na askari kuimarisha ulinzi huo, gari la Chadema lenye namba za usajili T 792 CAX likiwa na nembo ya M4C, nalo lilikuwa likipita katika mitaa ya mji huo ingawa haikufahamika lilikuwa likifanya hivyo kwa maana gani.
Kuanzia saa 12 alfajiri jana, ofisi za Chadema Mkoa wa Dodoma zilizoko eneo la Mji Mpya, zilikuwa zikilindwa na askari polisi waliokuwa na silaha.
Radio za kijamii zafungwa
Katika hali ambayo haikujulikana wazi, radio za kijamii za mjini hapa hazikuwa hewani jana asubuhi kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kudhibiti mawasiliano kati ya Chadema na wananchi.
Taarifa zilizopatikana baada ya mawasiliano hayo kukatika, zinasema redio hizo hazikuwa hewani kwa saa kadhaa jana kwa vile viongozi wa Chadema walikuwa wakizitumia kuhamasisha wananchi.
Miongoni mwa waliodaiwa kutumia redio hizo ni Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Dodoma, Jella Mambo ambaye awali alihamasisha maandamano hayo kupitia Redio Kifimbo na Nyemo FM.
Hata hivyo, taarifa nyingine zinasema redio hizo hazikuwa hewani kwa kuwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) walikuwa wakifanya marekebisho ya masafa.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Mambo alikiri kutumia redio hizo kuhamasisha maandamano kwa kuwa yalikuwa halali.
Pamoja na hayo, alisema kama Jeshi la Polisi limedhamiria kudhibiti maandamano yao, linatakiwa kuandaa fedha nyingi ili kukabiliana nayo.
“Hapa Dodoma maandamano yapo ila tunayafanya kimkakati kwani watu wametawanyika maeneo mbalimbali kila mmoja ana mabango yenye ujumbe tofauti, yakiwamo tunayompongeza Rais Jakaya Kikwete kwa busara yake aliyoitumia kutaka mchakato wa Katiba Mpya usikamilike kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015,” alisema Mambo.
Wakati huo huo, Mambo alisema gari moja la Chadema lililokuwa limebeba wajumbe wa Mkutano Mkuu waliokuwa wakitoka Dar es Salaam kuelekea Mwanza, lilikamatwa na askari polisi.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Emannuel Lukura alikiri kukamatwa kwa gari na wafuasi wanne wa chama hicho.
MBEYA
Habari kutoka mkoani Mbeya, zinasema polisi wameendelea kutunushiana misuli na Chadema kuhusu kufanyika au kutofanyika kwa maandamano ya kupinga kuendelea kwa Bunge Maalumu la Katiba.
Chadema imesisitiza kufanyika kwa maandamano hayo leo. Mratibu Kanda za Nyanda za Juu Kusini, Franky Mwaisumbe aliliambia MTANZANIA jana kuwa licha ya polisi kudai kuwa maandamano hayo ni batili, wao watahakikisha yanafanyika kwani lengo lao ni kufikisha ujumbe kwa wananchi.
Alisema wao wanachokifanya ni kutimiza azimio la Kamati Kuu lililotolewa wiki iliyopita na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi, alisema hadi jana jioni maandamano hayo yalikuwa hayajaombewa kibali.
ARUSHA
Mkoani Arusha, Chadema kimethibitisha kufanya maandamano leo, huku kikisema tayari majimbo 14 kati ya 33 yamewasilisha barua katika vituo vya polisi kwa ajili ya taarifa.
Katibu wa Kanda ya Kaskazini, Aman Golugwa akizungumza na MTANZANIA kwa njia ya simu jana, alisema tayari wamekwishajipanga kuhakikisha wanafanya maandamano ya amani ambayo hayatasababisha usufumbufu kwa watu wala kuvunja sheria yoyote.
“Lengo letu ni ujumbe ufike kwa wabunge Dodoma, kwamba kikao wanachoendelea nacho hakitatupa Katiba mpya. Sasa maandamano haya tumeyapa kwa mfumo wa pekee kabisa,” alisema.
Habari hii kwa hisani ya Gazeti la Mtanzania


SAA ZA GHARAMA ZAWAPONZA MAOFISA WA FIFA



Shirikisho la soka la dunia FIFA, limewaambia viongozi wanaounda kamati ya utendaji na viongozi wengine wa juu wa shirikisho hilo kurejesha saa zipatazo 65 za gharama walizopokea kama zawadi kipindi cha kuelekea kombe la dunia huko Brazil mwaka huu.
FIFA imesema kitendo cha kurejesha saa hizo ni kutunza nidhamu.
Saa hizo zinakadiriwa kuwa na gharama ya dolla elfu ishirini na tano kila moja na zinatakiwa ziudishwe Octoba 24 ,mwaka huu.
Saa hizo za kumbukumbu ya Parmigiani ziligawiwa na shirikisho la soka la Brazili (CBF) wakati wa mkutano wa maandalizi wa FIFA uliofanyika mjini Sao Paulo.
FIFA imesema kuwa kanuni za maadili zinazuia viongozi kupokea zawadi ambazo zinathamani zaidi au zenye kuonesha ishara fulani.

Inasemekana kwamba saa hizo zitatolewa kwa taasisi zinazojitegemea na si sile zinazojali maslahi huko Brazili.

MWAKA MMOJA TANGU TUKIO LA KIGAIDI KUTOKEA KENYA-WESTGATE

SCOTLAND YAKATAA UHURU KWA KURA YA KIHISTORIA





Raia wa Scotland wamefanya uamuzi wa mwisho kuwa wataendelea kubaki sehemu ya Uingereza , raia kwa pamoja wamekataa uhuru wa Scotland.
Maeneo 31 kati ya 32 wamepika kura ya HAPANA siku ya Alhamisi na kuongoza kwa kura 1,914,187 dhidi ya 1,539,920.
Ushindi huo ni asilimia 55 dhidi ya 45 waliokuwa wakiunga mkono hatua ya kujitenga.

Waziri Kiongozi wa Scotland Alex Salmond amesema ameridhia kuanguka katika mchakato wa kura ya maoni.