Thursday, April 23, 2015

Mkutano wa EU kuangazia tatizo la wahamiaji

Viongozi wa nchi za Ulaya wanakutana leo Alhamisi mjini Brussels, nchini Ubelgiji kuzungumzia tatizo la wahamiaji haramu wanaopitia katika bahari ya Mediterranean kwa kuingi Ulaya wakitokea pwani ya Libya.
Safari za wahamiaji hawa zimekua zikikumbwa na majanga hadi kusababisha vifo. Hivi karibuni wahamiaji zaidi ya 800 walifariki ndani ya majuma yasiyozidi mawili baada ya boti walizokuwemo kuzama maji katika bahari ya Mediterranean wakielekea Ulaya wakitokea katika pwani ya Libya.
Wakati ambapo matukio hayo ya kuzama kwa boti zinazowasafirisha wahamiaji haramu barani Ulaya yakiongezeka, Umoja wa Mataifa na mashirika yasiyo ya kiserikali hivi karibuni vilitoa wito kwa Umoja wa Ulaya kuchukua hatua zinazojitajiaka.
Jumatatu Aprili 20 mawaziri wa mambo ya nje wa nchi ishirini na nane za Ulaya walikutana mjini Luxembourg ili kujadili uwezekano wa kudhibiti hali hiyo.
Katika mpango wa kukabiliana na uhamiaji haramu uliyoandaliwa mjini Luxembourg Jumatatu wiki hii, kwanza kuna hatua ya kuzuia, inayounga mkono masuala ya upelelezi.
Taasisi za Europol na Eurojusts, polisi na majaji, pamoja na maafisa wa uhamiaji wanaoteuliwa kwenye balozi za umoja wa Ulaya katika nchi wanakotoka wahamiaji pamoja na nchi zinazowapokea, watakua wakitahmini kila siku orodha ya watu wanaosafiri kuelekea Ulaya wakipitia majini au nchi kavu.
Halafu kuna hatua ya kidiplomasia katika nchi zinazowapokea wahamiaji, hasa nchi ambazo zinazopakana na Libya, ambayo imekua sehemu ya mapokezi kwa wahamiaji wanaokimbilia Ulaya, kuchangia kudhibiti wimbi hilo la wahamiaji na kupunguza ajali za majini.
Halafu pia kuna kuzidisha mara dufu uwezo wa kifedha na meli kwa kazi ya uokozi na ulinzi wa mipaka inayoingia barani Ulaya. Meli hizi zinaweza kuingilia kati mahali popote katika maji ya kimataifa.
Hata hivyo bado kuna hatua zingine ambazo zitajadiliwa kataika mkutano mwingine wa Umoja wa Ulaya unaotazamiwa kufayika leo Alhamisi.
Hayo ya kijiri, takwimu zinazotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) zinabaini kwamba watu 800 walikufa maji katika ajali ya boti iliyotokea usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili Aprili 19, baada ya boti waliyokuwemo kuzama katika bahari ya Mediterranean. Boti hilo lilikua lilibeba mamia ya wahamiaji. Takwimu hizi zimetolewa kulingana na ushahidi uliyotolewa na manusura 28 kila waliowasili Catania, Sicily.








No comments:

Post a Comment