Monday, May 18, 2015

UNAFAHAMU NINI KUHUSU MTAJI WA KAMPUNI.

Huwezi kufikiria umiliki wa kampuni kabla ya kufikiria kuhusu mtaji wa kampuni. Mtaji wa kampuni ni suala nyeti kwa wenye wazo la kumiliki kampuni au wanaomiliki kampuni tayari. Mtaji ndio kila kitu katika kampuni. Tangu unapokuwa katika harakati za kusajili kampuni utalisikia neno hili mtaji karibia katika kila hatua unayopita. Niseme mapema kuwa mtaji mdogo ndio kampuni ndogo na mtaji mkubwa ndio kampuni kubwa. Kwa hili mitaji imegawanyika mara mbili upo mtaji wa maandishi unaokuwa kwenye katiba na waraka wa kampuni( MEMAT) na upo mtaji wa mali halisi ( physical assets)
Soma zaidi.http://sheriayakub.blogspot.com/2015/05/unafahamu-nini-kuhusu-mtaji-wa-kampuni.html

RAIS MSTAAFU MWINYI ATOA PONGEZI MAALUM KWA MAGUFULI

Saturday, May 16, 2015

Raisi wa Burundi Pierre Nkurunziza aonya juu ya jaribio lingine lolote la mapinduzi


Raisi wa Burundi Pierre Nkurunzizaamewatangazia raia wake kuwa sasa amani imerejea nchini humo ikiwa ni siku tatu baada ya kushindwa kwa jaribio la mapinduzi ya kijeshi.
Akihutubia wananchi kupitia runinga Pierre Nkurunziza ametoa onyo juu ya jaribio lingine lolote la kuchukua madaraka kwa nguvu litasababisha vita umasikini na majanga yalikwisha onekana katika taifa hilo.
Hayo yanajiri wakati Marekani ikitoa onyo hapo jana kwa raisi wa Burundi Pierre Nkurunziza kuhusu kutowania muhula wa tatu wa uongozi kwa vile kutazorotesha usalama nchini humo na kutishia misaada ya kimataifa.
Msemaji wa Washington Jeff Rathke ameeleza kuwa Marekani inawasiwasi kufuatia uwezekano wa kutokea ghasia zaidi baada ya raisi Nkurunziza kurejea nchini Burundi.
Msemaji wa washington amesema kuwa marekani bado inamtambua Nkurunzinza kama raisi halali wa Burundi licha ya kusisitiza kiongozi huyo kutowania muhula wa tatu.

Baadhi ya maafisa wa kijeshi walioshiriki kuongoza mapinduzi wamekamatwa huku wengine wakitokomea na kusakwa na majeshi tiifu kwa serikali akiwemo kiongozi wa mapinduzi hayo Generali Godefroid Niyombare, ambaye awali aliiambia AFP kuwa angejisalimisha kwa serikali.

TFF waigeuka kauli yao, sasa waibebesha msalaba CECAFA kuhusu Simba, Mbeya City

SHIRIKISHO la soka Tanzania, TFF, limeshindwa kuthibitisha moja kwa moja kama ni Simba au Mbeya City fc itakayoshiriki kombe la klabu bingwa Afrika mashariki na kati, maarufu kwa jina la ‘Kagame Cup’ linalotarajia kuanza kutimua vumbi Julai 11 hadi Agosti 2 mwaka huu jijini Dar es salaam.
Katibu mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine ameuambia mtandao huu kuwa CECAFA ndio watakaosema ni timu gani ya tatu nchini Tanzania wameialika kushiriki Kagame.
Kauli hii inatofautiana na ile aliyowahi kusema kupitia mtandao huu kuwa TFF wameichagua Simba badala ya washindi wa tatu wa msimu  wa 2013/2014 wa ligi kuu soka Tanzania bara, Mbeya City fc.
“Kimsingi na kwa taratibu wawakilishi wa Tanzania ni bingwa wa msimu uliopita (2013/2014) ambao ni Azam na mshindi wa pili ambaye ni Yanga anayefaidika na uenyeji wa Tanzania”. Amesema Mwesigwa na kuongeza: “Lakini Cecafa ina nguvu ya kuingiza klabu nyingine kutoka nchi mwenyeji au kutoka ukanda mwingine wa Cecafa. Watakaocheza ni Azam na Yanga, lakini tunategemea kupokea taarifa ya Cecafa kujua ni timu gani zimetumiwa mialiko. Cecafa yenyewe itathibitisha kuwa ni nani wa ziada wamemualika, lakini wanaoingia moja kwa moja kwa Tanzania kwa vigezo ni Azam (bingwa) na Yanga wanaofaidika na uenyeji wa Tanzania”.
Kauli hii inakinzana na kauli ya Mwesigwa aliyosema na kukaririwa na mtandao huu aprili 29 mwaka huu akisema Simba wamechaguliwa kuwakilisha Tanzania.
“Mbeya City walistahili, lakini niseme ukweli, tumeamua kumchukua Simba, kwanini? kwasababu ya rekodi yake. Amekuwa bingwa mara nyingi wa mashindano haya, kwahiyo ana nafasi yake sio katika Tanzania tu bali ukanda mzima,  na huwezi kumuondoa”. Alisema Mwesigwa na kuongeza: “Mwaka jana baada ya Azam kujitoa kushiriki mashindano mapya ya kagame, tuliwapa Mbeya City nafasi”.

Hata hivyo, Mbeya City fc wanaonekana kuisubiria kwa hamu nafasi hiyo na jana kocha mkuu wa Mbeya City Juma Mwambusi alisema bado hawana uhakika wa kushiriki kutokana na kushika nafasi ya tatu 2013/2014, lakini wanatamani kuona haki inatendeka.
Wadau wa soka wanasema tayari TFF wameshatuma jina la Simba, labda kwasasa wanawatupia mzigo Cecafa ili waonekane ndio wamewachagua Simba.
Hii inatokana na ukweli kwamba wapenda soka walichukizwa na kitendo cha TFF kuwatosa Mbeya City  fc wenye sifa na kuwapa nafasi Simba wasiokuwa na vigezo na sababu kubwa ikionekana ni maslahi kuliko kuendeleza soka.


 Kwa hisani ya http://shaffihdauda.co.tz/

Mgahawa wauza nyama ya binaadamu Nigeria

Mgahawa mmoja nchini Nigeria katika jimbo la Anambra umefungwa kufuatia viongozi wenye mamlaka nchini humo kung’amua kwamba moja ya vyakula vinavyouzwa mgahawani humo ni nyama ya binaadamu.

Polisi walipoitwa mgahawani hapo waliona vichwa viwili vya binaadamu vipya vyenye kuchuruza damu wakati walipokuwa wakiwakamata watu kumi na mmoja kutoka mgahawani hapo akiwemo mmiliki wa mgahawa huo,pia walikamatwa wanawake sita na wanaume wane, baada ya wasamaria wema kutoa taarifa hizo za kustaajabisha!
Damu zilizokuwa zikivuja kwenye vichwa hivyo vya wanaadamu,vilikuwa vimefungwa kwenye mifuko ya Rambo.
Polisi pia wamekamata bunduki aina ya AK-47 na silaha nyinginezo,seti ya magurunedi na simu kadhaa za kila aina wakati walipokuwa wakiwakamata watu hao.
Kila wakati nilipokuwa nikienda sokoni,na sababu kubwa hasa hoteli hiyo iko karibu na sokoni,nimekuwa nikishuhudia harakati za ajabu za watu kuingia na kutoka hotelini humo,watu wachafu na uchafu wao mwilini ni ule usioeleweka,hivyo sikushangazwa polisi walipogundua biashara hiyo haramu mapema wiki hii, anasema mkaazi wa eneo hilo.
Mchungaji mmoja akiwa katika mshtuko mkubwa baada ya kugundua kuwa alikuwa amekula nyama ya binaadamu,aliamua kwenda polisi kupeleka malalamiko yake .
Aliwaambia kuwa alikwenda kwenye mgahawa wa hoteli hiyo asubuhi na mapema,baada ya kupata staftahi,akaambiwa kwamba pande la nyama alilokula gharama yake ni naira 700 sawa na paundi mbili unusu alistaajabu mno.sikufahamu kuwa nimeuziwa nyama ya binaadamu nikaila na kwamba ilikuwa ghali sana.
Taarifa za watu nchini Nigeria kula nyama za watu zimekuwa ni uvumi wa muda mreefu, lakini hii ni mara ya kwanza mgahawa kuamua kuuza nyama za binaadamu tu.


Kwa hisani ya BBC-Swahili



Wanajeshi washika doria Bujumbura


Jeshi nchini Burundi linapiga doria kwenye mitaa ya mji mkuu Bujumbura ambapo waandamanaji wameahidi kufanya maandamano ya kupinga uamuzi wa rais wa kuwania muhula wa tatu.
Wanajeshi wana matumaini ya kuwakamata wanajeshi waasi ambao waliongoza mapinduzi ya wiki hii katika jaribio la kumpindua rais Pierre Nkurunziza.
Nkurunziza ametaka kusitishwa kwa maandamano hayo na kuyahusisha na jaribio hilo la mapinduzi.
Lakini baadhi ya makundi ya waandamanaji yamekana madai hayo na kumtaka tena rais kuiheshimu katiba.

Marekani nayo inasema kuwa Nkurunziza hastahili kuwania muhula mwingine ikiongeza kuwa serikali yake itawajibika kwa chochote kile kitakachotokea.

Kwa hisani ya BBC-Swahili

Wednesday, May 13, 2015

Taifa Stars yaelekea Afrika ya Kusini

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kesho Jumatano inatarajiwa kusafiri kuelekea nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kushiriki michuano ya kombe la COSAFA.
 
Michuano ya COSAFA inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Mei 17 mpaka Mei 30, 2015 katika viwanja vya Olympia Park na Moruleng jimbo la North West Province nchini Afrika Kusini ikishirikisha nchi za Kusini mwa Afrika huku Tanzania na Ghana zikiwa ni nchi waalikwa.
Taifa Stars itaondoka jijini Dar es salaam kesho majira ya saa 1 jioni, kwa usafiri wa shirika la ndege la Fasjet na kufika jijini Johanesburg saa 5 usiku.
Mara baada ya kupimwa afya jana na madaktari wachezaji Aishi Manula, Isihaka Hassan, Haroun Chanongo, Kelvin Friday na nahodha Nadir Haroub wamekutwa na majeruhi ambayo yamepelekea kutokuwepo katika kikosi kitakachosafiri kesho, watabakia nchini wakiendelea kufanya mazoezi chini ya ungalizi mpaka timu itakaporejea kutoka Afrika Kusini na kuungana kwa ajili ya maandalizi ya AFCON, huku Amri kiemba akipewa ruhusa kutokana na kuwa na matatizo ya kifamilia.
Msafara wa Taifa Stars utaongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa TFF, Ephaphra Swai ukijumuisha wachezaji 20 na benchi la ufundi, timu inatarajiwa kufikia katika hoteli ya Sun City iliyopo pembeni kidogo ya jiji la Rusterburg.

Barcelona yatinga fainali

Barcelona imetinga fainali ya michuno ya ligi ya Mabingwa, baada ya kumenyana Jumanne usiku wiki hii na Bayern Munich. Bayern Munich imeaga michuano hiyo, baada ya kuifunga Barcelona mabao 3-2 katika mchezo wa marudiano wa michuano ya nusu fainali ya Kombe la Mabingwa barani Ulaya.

Katika mchezo wa awali uliyochezwa wiki moja iliyopita, Barcelona iliifunga Bayern Munich mabao 3-0.
Barcelona inasubiri kucheza fainali Juni 6 mwaka 2015 na moja ya klabu itakayoshinda leo Jumatano usiku kati ya Real Madrid na Juventus.
Bayern Munich ndio iliyoanza kuona lango la Barcelona katika mchezo wa marudiano wa michuano ya fainali ya Kombe la Mabingwa barani Ulaya. Bao la kwanza la Bayern limefungwa na mchezaji kutoka Morocco Mehdi Benatia katika dakika ya 7 ya mchezo.

Katika dakiaka ya 15 Barcelona kupitia mchezaji wake Neymar ikasawazisha baada ya pasi aliyopewa na Luis Suarez kutoka kwa Muargentina Lionel Messi.
Barcelona iliendelea kushambulia lango la Bayern Munich na kufaulu katika dakika ya 29 kufunga bao la pili kupitia mchezaji wake Neymar, na kuongoza mabao 2-1 dhidi ya Bayern Munich.
Hadi wakati huo, Bayern Munich ilikua inataraji ifunge mabao 6-2 ili iweze kutinga fainali ya michuano ya ligi ya Mabingwa barani Ulaya. Lakini hali hiyo haikutokea.
Hata hivyo Bayern ilikuja juu na kufaulu kusawazishabao la pili kupitia Robert Lewandowski katika dakiaka ya 40. .
Katika dakika ya 74, Bayern Munich kupitia mchezaji wake Thomas Müller ilifunga bao la tatu. Hadi kipenga cha mwisho Bayern Munich iliongoza kwa mabao 3-2 dhidi ya Barcelona. Licha ya Bayern kuibuka mshidi katika mchuano huo, ililazimika kuaga michuano hiyo, baada ya kupoteza katika mechi ya awali ya nusu fainali wiki moja iliyopita, ambapo ilifungwa mabao 3-0.
Barcelona, wamefanikiwa kutinga fainali baada ya kuibwaga Bayern Munich kwa jumla ya mabao 5-3 yaliyopatikana katika mikondo yote miwili waliyokutana kwenye hatua ya nusu fainali.
Jumatatu usiku wiki hii kutakuwa na mchuano kati ya Real Madrid dhidi ya Juventus kwenye uwanja wa Benabeu.

Shughuli za uokozi zakwama upya Nepal


Wafanyikazi wa mashirika ya kutoa misaada wamesema kuwa tetemeko la hapo jana nchini Nepal limeathiri kwa kiasi kikubwa.juhudi za kutoa misaada kwa waathiriwa wa tetemeko la awali lililosababisha vifo vya zaidi ya watu 8000 takriban majuma mawili yaliyopita.
 
Mashirika ya misaada yanasema kuwa maporomoko mapya ya ardhi sasa yemekatiza usafiri baada ya kuziba mabarabara yaliyokuwa yamesazwa na tetemeko la awali.
Hadi kufikia sasa inakisiwa kuwa takriban watu 65 wamepoteza maisha yao nchini Nepal huko maafa zaidi yakitarajiwa nchini India na Tibet ,China.
Shughuli za uokozi zimerejelewa Nepal, ambayo kwa mara ya pili ndani ya wiki tatu imekumbwa na tetemeko kubwa la ardhi.
Lakini bado kuna watu waliozikwa kwenye vifusi.
Maafisa wa huko wanasema kuwa wanatarajia idadi hiyo kuongezeka.
Kufikia sasa takriban watu 1,000 wamejeruhiwa na tetemeko hilo lipya.

Waathiriwa wengi wameripotiwa kufunikwa na vifusi karibu na kitovu cha tetemeko hilo katika mji wa Chautara
Watu wengi wamelala nje wakihofia kuwa wanaweza kuathirika zaidi wakiwa ndani ya nyumba zao.
Wakati huo huo helikopta ya kikosi cha majini cha Marekani,ambayo ilikuwa ikifanya kazi ya kusaidia kusambaza huduma za kibinaadamu nchini Nepal, haijulikani iliko.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa, ndani ya helikopta hiyo kulikuwa na watu wanane,miongoni mwao, sita ni askari wa kikosi cha majini cha Marekani na askari wawili wa jeshi la Nepal.
Maofisa wa serikali wa Marekani wamesema kwamba helikopta hiyo ilikuwa maeneo ya jirani na kijiji cha Charikot, ambacho kiliharibiwa vibaya na tetemeko la ardhi.

 
Kwa hisani ya bbcswahili.com

 

Tuesday, May 12, 2015

BAADHI YA MADHARA YA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA JIJINI DAR

Hii ni barabara ya mbozi Chang'ombe 


Eneo la Sokota barabara ya Mandela

Kero hii ya mvua na miundombinu mibovu ni hata kwa waenda kwa Miguu

Picha zote kwa hisani ya Mdau wetu Roman Mallya

Thursday, May 7, 2015

ATHARI ZA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA JIJINI DAR

Hapa ni maeneo ya Mchicha kutokea Vingunguti njia imejaa maji na haipitiki
Vingunguti

Maeneo ya Chang'ombe Mbozi Road

Picha zote kwa hisani ya Mdau wetu Maonyesho Ndege