Saturday, May 16, 2015

Wanajeshi washika doria Bujumbura


Jeshi nchini Burundi linapiga doria kwenye mitaa ya mji mkuu Bujumbura ambapo waandamanaji wameahidi kufanya maandamano ya kupinga uamuzi wa rais wa kuwania muhula wa tatu.
Wanajeshi wana matumaini ya kuwakamata wanajeshi waasi ambao waliongoza mapinduzi ya wiki hii katika jaribio la kumpindua rais Pierre Nkurunziza.
Nkurunziza ametaka kusitishwa kwa maandamano hayo na kuyahusisha na jaribio hilo la mapinduzi.
Lakini baadhi ya makundi ya waandamanaji yamekana madai hayo na kumtaka tena rais kuiheshimu katiba.

Marekani nayo inasema kuwa Nkurunziza hastahili kuwania muhula mwingine ikiongeza kuwa serikali yake itawajibika kwa chochote kile kitakachotokea.

Kwa hisani ya BBC-Swahili

No comments:

Post a Comment