Friday, July 10, 2015

Ugiriki yatoa mapendekezo mapya kwa wakopeshaji wake

 Viongozi wa Ugiriki wametuma mapendekezo ya mageuzi ili kupata makubaliano na wakopeshaji wake na kukomesha mgogoro unaoendelea.
Viongozi hao wamepania hasa kuongeza VAT na mageuzi ya pensheni. Mapendekezo ambayo, dhidi ya matatizo yote, hayaonekani kuwa tofauti sana na kile kilichokuwa kinatakiwa na wakopeshaji wa Athens, ambao wanapaswa kuyajadili leo Ijumaa asubuhi.
Ugiriki hatimaye imetuma mapendekezo yake kwa ajili ya mageuzi kabla ya kutamatika kwa muda wa mwisho uliyowekwa na viongozi wa Ulaya. Mapendekezo hayo yanapaswa kufuata mkondo wa masharti yaliyopendekezwa na wakopeshaji wa wake.
Serikali ya Ugiriki imejikubalisha kuongeza VAT kwa asilimia 23 kwa ajili ya chakula na asilimia 13 kwa ajili ya hoteli. Serikali ya Ugiriki pia imepania kufuta au kusamehe polepole VAT zinazotozwa katika visiwa vya Ugiriki.
Ugiriki pia imepania kuongeza kodi katika makampuni makubwa na mashrika mengine yasiyo ya kiserikali. Kodi kwa bidhaa za anasa na matangazo ya biashara kwenye televisheni itawekwa mara moja. Bajeti takatifu katika sekta ya ulinzi itapunguzwa Euro milioni 300 na ubinafsishaji uliosimamishwa baada ya Alexis Tsipras kuchukua hatamu ya uongozi wa nchi, utarejeshwa.
Mageuzi mapya ya pensheni pia yanatazamiwa pia kufanyika. Umri wa miaka 67 unapaswa kuwa kigezo cha kukatisha tamaa ya kustaafu mapema pamoja na kufuta au kusamehe polepole posho ya mshikamano (EKAS).
Kulingana na nakala ya mapendekezo iliyotolewa na serikali ya Ugiriki, Ugiriki inataka suluhisho " ili kurekebisha" madeni yake makubwa, kwa asilimia 180 ya Pato la Taifa, pamoja na "pakiti ya Euro bilioni 35" iliyotengwa kwa ukuaji. Serikali ya Ugiriki imesema pia iko mbioni kutafuta fedha kwa jumla ya Euro bilioni 53.5 ifikapo mwishoni mwa mwezi Juni mwaka 2018 ili kufidia majukumu yake yanayohusiana na malipo yake ya mkopo.

No comments:

Post a Comment