Thursday, April 23, 2015


WAKIMBIZI AZIDI KUMIMINIKA NCHINI RWANDA

Kambi ya Gashora nchini Rwanda inazidi kupokea wakimbizi wanaotoka mkoa wa Kirundo nchini Burundi ,wengi wanakimbia nchini mwao  kutokana na usalama wa nchi hiyo,wakimbizi hao wanatoka mikoa mbalimbai ya Burundi,vijana wa chama tawala inasemekana kuwa wanahatarisha usalama wa nchi.Ujenzi wa mahema kwenye kambi hiyo unaendelea,ila wakambizi wanalalamikia kuwa chakula hakitoshi.Wasimamizi wa wakambizi wa nchi ya Rwanda wanasema kambi ni ya Muda tu ,Serikaliinafanya mpango wa kuwahamisha na kuwapeleka Kirehe.inasadikiwa idadi ya wakimbizi imefikia 10000.

Mkutano wa EU kuangazia tatizo la wahamiaji

Viongozi wa nchi za Ulaya wanakutana leo Alhamisi mjini Brussels, nchini Ubelgiji kuzungumzia tatizo la wahamiaji haramu wanaopitia katika bahari ya Mediterranean kwa kuingi Ulaya wakitokea pwani ya Libya.
Safari za wahamiaji hawa zimekua zikikumbwa na majanga hadi kusababisha vifo. Hivi karibuni wahamiaji zaidi ya 800 walifariki ndani ya majuma yasiyozidi mawili baada ya boti walizokuwemo kuzama maji katika bahari ya Mediterranean wakielekea Ulaya wakitokea katika pwani ya Libya.
Wakati ambapo matukio hayo ya kuzama kwa boti zinazowasafirisha wahamiaji haramu barani Ulaya yakiongezeka, Umoja wa Mataifa na mashirika yasiyo ya kiserikali hivi karibuni vilitoa wito kwa Umoja wa Ulaya kuchukua hatua zinazojitajiaka.
Jumatatu Aprili 20 mawaziri wa mambo ya nje wa nchi ishirini na nane za Ulaya walikutana mjini Luxembourg ili kujadili uwezekano wa kudhibiti hali hiyo.
Katika mpango wa kukabiliana na uhamiaji haramu uliyoandaliwa mjini Luxembourg Jumatatu wiki hii, kwanza kuna hatua ya kuzuia, inayounga mkono masuala ya upelelezi.
Taasisi za Europol na Eurojusts, polisi na majaji, pamoja na maafisa wa uhamiaji wanaoteuliwa kwenye balozi za umoja wa Ulaya katika nchi wanakotoka wahamiaji pamoja na nchi zinazowapokea, watakua wakitahmini kila siku orodha ya watu wanaosafiri kuelekea Ulaya wakipitia majini au nchi kavu.
Halafu kuna hatua ya kidiplomasia katika nchi zinazowapokea wahamiaji, hasa nchi ambazo zinazopakana na Libya, ambayo imekua sehemu ya mapokezi kwa wahamiaji wanaokimbilia Ulaya, kuchangia kudhibiti wimbi hilo la wahamiaji na kupunguza ajali za majini.
Halafu pia kuna kuzidisha mara dufu uwezo wa kifedha na meli kwa kazi ya uokozi na ulinzi wa mipaka inayoingia barani Ulaya. Meli hizi zinaweza kuingilia kati mahali popote katika maji ya kimataifa.
Hata hivyo bado kuna hatua zingine ambazo zitajadiliwa kataika mkutano mwingine wa Umoja wa Ulaya unaotazamiwa kufayika leo Alhamisi.
Hayo ya kijiri, takwimu zinazotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) zinabaini kwamba watu 800 walikufa maji katika ajali ya boti iliyotokea usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili Aprili 19, baada ya boti waliyokuwemo kuzama katika bahari ya Mediterranean. Boti hilo lilikua lilibeba mamia ya wahamiaji. Takwimu hizi zimetolewa kulingana na ushahidi uliyotolewa na manusura 28 kila waliowasili Catania, Sicily.








AMIRI JESHI MKUU RAIS JAKAYA KIKWETE AONGOZA MAZISHI YA ALIYEKUWA MKUU WA WILAYA YA KYERWA LUTENI KANALI BENEDICT KITENGA (MSTAAFU) LEO MKOANI MOROGORO

Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Kikwete (pichani kati)  na Waziri Mkuu Mh.Mizengo Pinda  (pichani shoto) wakishuhudia askari wa jeshi la Wananchi (JWTZ) wakipiga risasi hewani kama sehemu ya heshima ya kumuaga aliyekuwa mkuu wa wilaya mpya ya Kyerwa mkoani Kagera leo,Marehemu Luteni Kanali Benedict Kitenga (mstaafu) huko kwenye makaburi ya Mlima Kola Kigurunyembe mkoani Morogoro. PICHA NA IKULU.

Source:fullshangwe blog

Waandamana kupinga ubaguzi Afrika Kusini

Maelfu ya raia wa Afrika Kusini wanaandamana kupinga wimbi la visa vya hivi majuzi vya mashambulizi dhidi ya raia wa kigeni.
Mikutano mikubwa imeandaliwa katika mji mkuu Johannesburg na katika mji wa Port Elizabeth ulioko kusini mwa nchi hiyo ambao ulishuhudia mashambulio kadhaa dhidi ya wahamiaji wa mataifa ya kigeni mnamo mwaka 2008.
Makundi ya kiusalama yanafanya misako katika majumba ya makaazi katika mji wa Alexandra mjini Johannesburg, mahala ambapo mashambulio kadhaa dhidi ya raia wa kigeni hasa Afrika yalifanyika katika kipindi cha majuma kadhaa yaliyopita.

Mwaandishi wa BBC anasema kuwa, kuonekana kwa walinda usalama barabarani kumeleta udhibiti na amani.
Source:bbcswahili.com

Saturday, April 4, 2015

Mkasi Special Show - Extended Version

Mpango wa Nyuklia wa Iran : makubaliano yafikiwa

Kwa siku ya nane ya mazungumzo kati ya Kundi la nchi 6 zenye nguvu duniani na Iran katika mji wa Lausanne Alhamisi jioni Aprili 2, makubaliano kati ya pande mbili hatimaye yamefikiwa.
Aprili 2 mwaka 2015, katika mji wa Lausanne, Uswisi, makubaliano ya kisiasa yakifikiwa kati ya Tehran na mataifa yenye nguvu duniani kuhusu suala la mpango wa nyuklia wa Iran.
Iran na serikali za Magharibi wamesema "vigezo muhimu" kwa "mfumo wa makubaliano" au "hatua" hatimaye zimepigwa.
"vigezo muhimu" kwa mfumo wa makubaliano kuhusu mpango wa Nyuklia wa Iran vimepatikana, ametangaza mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya, Federica Mogherini, katika mkutano na vyombo vya habari, akiwa pamoja na mwenziye wa Iran katika mji wa Lausanne. Maneno haya yametumiwa na upande wa Iran pamoja na waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry.
Umoja wa Ulaya na Marekani watasitisha vikwazo vyote vya kiuchumi na kifedha vinavyohusiana na nyuklia. " Tuko mbioni sasa kuandika rasimu ya Nakala ya mpango wa utekelezaji wa pamoja, ikiwa ni pamoja na maelezo ya kiufundi katika wiki na miezi ijayo", amesema Federica.
Ni kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter ambapo Rais wa Iran Hassan Rouhani akifuatiwa na viongozi kadhaa wa nchi za Magharibi wametoa taarifa kwamba makubaliano kuhusu masuala nyeti ya mpango wa nyuklia wa Iran yamepatiwa ufumbuzi. Zoezi la kuandika makubaliano ya mwisho linaweza kuanza mara moja, kwa mujibu wa Hassan Rouhani. Mkataba wa mwisho unaweza kutiliwa saini " Juni 30", Iran imethibitisha.
Makubaliano haya ya msingi yanaeleza kwamba theluthi mbili ya uwezo wa sasa wa Iran wakurutubisha uranium usitishwe na kufuatiliwa kwa kipindi cha miaka kumi, kwa mujibu wa chanzo cha Magharibi. vituo 6000 kwa jumla ya 19000 vinavyorutubisha uranium vitafuatiliwa, vyombo vya habari vya Iran vimethibitisha. " Uwezo wa kuipa thamani ya juu uranium kutoka Iran utapunguzwa", amesema Federica Mogherini.


Burundi : Spika wa bunge azuiliwa kusafiri

Joto la kisiasa limeendelea kupanda nchini Burundi kufuatia nia ya rais Pierre Nkurunziza ya kugombea muhula wa tatu, huku wafanyakazi wa serikali wanaopinga kugombea kwa Pierre Nkurunziza muhula wa tatu wakifutwa kazi.
Wakati huohuo, Spika wa Bunge nchini Burundi, Pie Ntavyohanyuma amezuiliwa Alhamisi wiki hii kusafiri kwenda nchini ubelgiji katika ziara ya kikazi. Wizara ya fedha imemuomba kiongozi huyo kutoa maelezo kuhusu matumizi ya Euro elfu thelathini aliyopewa alipofanya ziara ya kikazi nchini Kenya. Lakini wengi wanaona kwamba kuzuiliwa kwa Spika huyo, kunaambatana na malumbano yanayojiri wakati huu katika chama madarakani Cndd-Fdd.
Aliyekuwa kiongozi wa chama cha Cndd-Fdd, Hussein Radjabu ameikosoa nia ya rais Nkurunziza ya kutaka kugombea muhula watatu, akisema kwamba iwapo rais huyo atafanya hivyo atakua amewakosea wafuasi wa chama cha Cndd-Fdd pamoja na raia wa Burundi kwa ujumla.
Hayo yakijiri, wito uliyotolewa na mashirika ya kiraia wa kuwataka raia popote pale walipo kupiga honi, firimbi na kogonganisha vyuma saa sita mchana Alhamisi Aprili 2, umeitikiwa mjini Bujumbura na katika sehemu mbalimbali za nchi.
Jumatano wiki hii katika mkutano na waandishi wa habari kiongozi wa muungano wa mashirika ya kiraia Forsc, Vital Nshimirimana, amesema wito huo kwa raia ni kama kadi nyekundu anayopewa mchezaji wa soka aliyefanya madhambi, akibaini kwamba rais Nkurunziza atakua amepewa kadi nyekundu.
Hayo yanajiri wakati Kaskazini mwa nchi hiyo, hasa katika mkoa wa Kirundo zaidi ya raia 300 wamekimbilia nchi jirani ya Rwanda, wakisema wanahofia usalama wao kutokana na hali inayojiri wakati huu nchini mwao. Waziri wa Rwanda mwenye dhamana ya wakimbizi, Serafine Mukantabana amesema serikali yake imejenga kambi mbili ambapo watapewa hifadhi wakimbizi hao.
Waziri Mukantabana ameongeza kuwa wako mbioni kuwapatishia matibabu baadhi ya wakimbizi ambao wameanza kusumbuliwa na maradhi mbalimbali.


Kila lakheri Young Africans

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amewatakia kila la kheri wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye kombe la Shirikisho barani Afrika Young Africans, katika mchezo wa marudiano dhidi ya FC Platinum ya Zimbabwe utakochezwa siku ya jumamosi kwenye uwanja Mandava uliopo Gweru Bulawayo.
Malinzi amesema Young Africans hawapaswi kubweteka na ushindi walioupata awali wa mabao 5-1, kikubwa wanapaswa kwenda kupambana kusaka ushindi ugenini ili kuweza kufuzu kwa hatua inayofuata ya timu 16.
Endapo Young Africans itafanikiwa kuwatoa FC Platinum itaingia katika hatua ya 16 bora na itakutana na mshindi kati ya timu za Benifica de Luanda ya Angola au Etoile du Saleh ya Tunisia.


Waandamana dhidi ya Al-shabaab Garissa

Wananchi wa mji wa Garissa nchini Kenya wamefanya maandamano kupinga vitendo vya kundi la Al Shabaab, lililoshambulia chuo kimoja kikuu mjini humo na kuwaua watu 147 wengi wao wakiwa wanafunzi hapo jana.
Waandamanaji pia wameelezea kutoridhika na vyombo vya usalama nchini humo wakisema havikuchukua hatua za kutosha kutoa ulinzi kwa waliouawa na kwa raia wengine kwa jumla.Wazazi, jamaa na marafiki wa wanafunzi waliouawa katika chuo kikuu cha Garissa wamekuwa wakiendelea kuwasili katika eneo hilo kuitambua miili ya wapendwa wao.Waliojeruhiwa wanaendelea kupata matibabu .

Kwa hisani ya BBC Swahili