Friday, June 12, 2015

COPA AMERICA KUMEKUCHA

Michuano mikubwa barani Amerika imeanza hapo jana kwa wenyeji wa mashindano hayo Chile kumenyana na Ecuador na wenyeji kuibuka na ushindi mnono wa Magoli 2-0.Mpambano huo ulifanyika katika jiji la Santiago.
Ikubukwe kuwa Chile haijachukua ubingwa huo kwa takribani miaka 99 sasa.
Kwa ushindi huo unawapa Chile ari ya kufanya vizuri zaidi katika mashindano ya mwaka huu.

Arturo Vidal akifunga goli la kwanza kwa penati


Wachezaji wa Chile wakishangilia ushindi baada ya mechi kuisha


Picha kwa hisani ya bbc sport

NAFASI ZA MASOMO CHUO CHA MAENDELEO NA USIMAMIZI WA MAJI


Nigeria na mikakati dhidi ya Boko Haram

Serikali ya Nigeria na nchi nyengine nne majirani zimekubaliana kuunda vikosi vya jeshi la pamoja ili kupambana na wapiganaji wa kiislamu wa Boko Haram.
Kikosi hicho kitapiga kambi katika mji mkuu wa Chad, Ndjamena, lakini kitakuwa chini ya usimamizi wa Nigeria.Nchi ya Chad, Cameroon, Niger na Benin pia zitatoa wanajeshi wake.
Baada ya mkutano huo uliofanyika katika mji mkuu wa Nigeria Abuja, katibu mkuu wa wizara ya ulinzi ya Nigeria, Aliyu Ismail, amesema kikosi hicho kitakuwa tayari kuanza kazi ifikapo mwezi July mwaka huu:"viongozi wa nchi na serikali za nchi za ukanda wa ziwa Chad na Benin zimechukua uamuzi ufuatao.
kupitisha dhana ya ufanyaji kazi, mikakati ya ufanyaji kazi na nyaraka zinazohusiana na kuundwa kwa vikosi vya pamoja katika kupambana na kundi la kigaidi la wapiganaji wa Boko Haram, kupitisha kupelekwa kwa vikosi hivyo katika makao makuu ya Ndjamena, Chad, kwa utekelezaji wa rasilimali watu na mahitaji ya kifedha.

Kwa hisani ya http://www.bbc.com/


GAZETI LA MWANANCHI LEO 12.6.2015




DIRA YA DUNIA ALHAMISI 11.06.2015