Wednesday, October 19, 2016

KUTOKA KWA MDAU WETU GUNDA FOUNDATION


vv
Mwaka 2016 Shirika la Twaweza Afrika Mashariki lilizindua utafiti wake (http://twaweza.org/go/uwezo-tz-2014) uliofanyika mwaka 2015 ukionesha ongezeko kubwa la watoto kushindwa kusoma ilhali wapo madarasa ya juu mfano darasa la nne nakuendelea.
Tafiti hizi sio za kusoma na kuangalia hivi hivi. Kila mmoja wetu anayo nafasi ya kusaidia anguko hili ambalo linazidi kumomonyoa na kuifanya Elimu kwa watoto wetu kuwa duni na yakukatisha tamaa.
Kama Marafiki wa Elimu kupitia Gunda Foundation Tanzania, tumekua tukifanya Harakati mbalimbali za kuwasaidia watoto kupenda kujifunza na kujisomea vitabu ili kukuza maarifa na kuboresha maendeleo ya ufahamu walionao.
Mwaka 2014 Gunda Foundation ilifanya Jitihada za mwanzo katika kuwasaidia watoto wa kata ya Msambara, Wilaya ya Kasulu mkoani kigoma kuweza kusoma.
Katika mradi huo ulijumuisha shule 7 za kata hio na jumla ya watoto 197 wa shule tano za kata hio waliingia katika utaratibu huu wakati wa likizo ya mwezi wa 12, 2014.
Watoto hawa walikua katika hatua tofauti tofauti za usomaji. Mbinu mbalimbali zilitumika ili kutambua uwezo halisi wa mtoto katika kusoma.
Utaratibu wa kuwatambua na kuwatenga watoto hawa ulikua kama ifuatavyo;
  1. Viliandikwa vikaratasi vikiwa na neno moja mpaka maneno mawili, kisha kutupwa katika eneo la shule vikiwa vya idadi ya kutosha;
  2. Wanafunzi wakiwa darasani waliruhusiwa kutoka darasani na kila mmoja alitakiwa aokote karatasi lolote atakalo liona katika mazingira ya shule yake na akisha okota basi akimbie mpaka katika uwanja wa shule na kusimama umbali wa mita 20 mbali na mwenzake;
  3. dsc02318
  4. Bila watoto kusomeana vikaratasi hivyo kutokana na umbali waliosimama mmoja hadi mwingine, Mwalimu alianza kuita mwanafunzi mmoja baada ya mwingine na akifika mwalimu humuomba mwanafunzi amsomee neno lililoandikwa katika karatasi aliyoiokota.
  5. Kwa njia hii makundi kadhaa yalitenganishwa kulingana na uwezo wa mtoto kusoma neno hilo kwa vigezo vya bila kusita;
  6. Watoto walioonesha udhaifu mkubwa waliingizwa darasani na kuandikiwa silabi “a” mpaka “z” ubaoni na walitakiwa wasome silabi zote mmoja baada ya mwingine ili mwalimu ajiridhishe zaidi katika uwezo wa mwanafunzi kusoma;dsc02326
  7. Hii ilifanyika ili kusaidia kumpa mtoto mkakati maalumu utakaomsaidia kusoma vizuri.
  8. Baada ya kuapata makundi ya uwezo tofauti wa usomaji mwalimu alianza mafunzo ya kuwaelekeza watoto kujifunza kusoma na programu hii ni ya mwezi mmoja na hufanyika katika kipindi cha likizo ya mihula ya wanafunzi.
  9. Kumbuka: Ukihitaji kuona video ya vitendo hivi au matokeo wasiliana nasi kwa namba 0674 14 12 09 au Baruapepe: gmpollo@gmail.comau fika Chuo cha Ualimu Korogwe onana na Mwalimu Gunda.
    Kuanzia mwaka huu 2016, Mwezi Octoba Marafiki wa Elimu kwa ushirikiano na Gunda Foundation wanatarajia kuifanya programu hii katika mkoa wa Tanga hususani katika Wilaya za Handeni Vijijini na Korogwe.
    Kwa Korogwe pia itahusisha Darasa la watu wazima na wale waliokosa nafasi ya kujiunga na darasa la kwanza wakiwa na umri mkubwa ili kuwapa fursa ya kujua kusoma na kuandika.
    Hivyo ukiwa kama mdau wa Elimu unaomba kama una mtoto, ndugu au jamaa asiejua kusoma na kuandika basi wasiliana nasi ili aweze kusaidiwa na HAKUNA MALIPO YOYOTE ATAKAYOCHANGIA KATIKA UJIFUNZAJI WAKE!
    9
    Sote tunawajibu kuwasaidia Watoto Wajifunze

No comments:

Post a Comment