Thursday, November 30, 2017

Raisi wa Nigeria apinga raia wake kuuzwa kama mbuzi Libya

Raisi wa Nigeria Muhammadu Buhar amesemaraia wote wa Nigeria ambao wamekwama Libya watarejeshwa nyumbani.
Amesema hayo baada ya video za hivi karibuni mitandaoni zikionyesha waafrika wakiuzwa kwenya soko la mnada wa watumwa huko nchini Libya
Buhari amesema”baadhi ya raia wa Nigeria wanauzwa kama mbuzi dola kadhaa Libya”
Kwenye video iliyotolewa na shirika la habari la CNN mapema mwezi huu ,vijana kutoka mataifa ya Afrika kusini mwa jangwa la Salahara walionekana wakiuzwa kama wafanyakazi wa mashambani .
Walikuwa wakiuzwa $400 katika eneo ambalo halikuwekwa wazi huko Libya                                                     


 Picha kwa hisani ya cnn.com



No comments:

Post a Comment