Wednesday, December 6, 2017

MWANAFUNZI AJIFANYA ASKARI WA JWTZ

Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam, inamshikilia mwanafunzi wa Sekondari ya Fahari iliyopo Goba, mwenye miaka 17 kwa kosa la kukutwa amevaa sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Kamanda Mambosasa amesema katika mahojiano ya awali, kijana huyo alijitambulisha kuwa ni askari kutoka 501 KJ Lugalo jijini Dar es Salaam.

Amesema baada ya kubanwa alikiri kupata sare hizo kwa rafiki zake na upekuzi ulipofanywa ndani ya begi alilokuwa nalo alikutwa na kofia nyingine moja ya jeshi hilo.


Pia, alikutwa na kitambulisho cha mtoto wa askari wa JWTZ Private Gabriel Kiwila wa 501 KJ. (Picha kwa hisani ya Mwananchi).

No comments:

Post a Comment