Monday, October 28, 2013
Mourinho amsifia Torres kwa kuipa Cheslea bao la ushindi
Kocha wa klabu ya soka ya Chelsea nchini Uingereza Jose Mourinho amemsifu mshambulizi Fernando Torres baada ya kuisaidia timu yake kupata ushindi wa mabao 2 kwa 1 dhidi ya Manchester City katika mchuano wa ligi kuu ya soka nchini humo mwishoni mwa juma lililopita
Thursday, October 10, 2013
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MBEYA KWA UMMA-AJALI YA GARI KUACHA NJIA, KUPINDUKA NA KUSABABISHA KIFO NA MAJERUHIKwa
MNAMO TAREHE 08.10.2013 MAJIRA YA SAA 16:00HRS HUKO
KATIKA ENEO LA RELINI – MLOWO BARABARA YA MLOWO/KAMSAMBA
WILAYA YA MBOZIMKOA WA MBEYA. GARI T.353 APR AINA YA TOYOTA HILUX
P/UP LIKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE,
LILIACHA NJIA NA KUPINDUKA KISHA KUSABABISHA KIFO CHA MTOTO PETRO S/O
KAUNDA, MIAKA 3, KYUSA, PIA MAJERUHI KWA MAMA MZAZI WA MTOTO HUYO AITWAE
FAUSTA D/O MBUBA, MIAKA 35, MNYIHA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA ITEMPULA
AMBAYE AMELAZWA ZAHANATI YA NAZARETH – MLOWO. CHANZO KINACHUNGUZWA.
DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO. MWILI WA MAREHEMU
UMEHIFADHIWA KATIKA ZAHANATI HIYO. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA
WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA
SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA
KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI
ALIPO MTUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA
ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE.
WILAYA YA KYELA – KUPATIKANA NA
BHANGI. MNAMO TAREHE 08.10.2013 MAJIRA YA SAA 16:00HRS HUKO ENEO LA
MBUGANI WILAYA YA KYELA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA
WALIMKAMATA FRANK S/O ARON, MIAKA 27, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA MBUGANI
AKIWA NA BHANGI MISOKOTO 20 SAWA NA UZITO WA GRAM 120. MTUHUMIWA NI
MUUZAJI NA MVUTAJI WA BHANGI. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE
MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA
POLISI DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUACHA
KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA
YA MTUMIAJI.
[DIWANI ATHUMANI - ACP]KANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
KWA HISANI YA:mbeyayetu.blogspot.com
Subscribe to:
Posts (Atom)