Viongozi nchini Guinea wamesema tayari
wamepata maiti kadhaa za timu ya wahudumu wa afya pamoja na wanahabari
waliotoweka walipokuwa wakiendeleza harakati za kuwaelimisha na kuwahamasisha
wananchi kuhusu ugonjwa wa Ebola.
Msemaji wa serikali ya Guinea amesema kati ya miili hiyo ni ile
ya wanahabari watatu wa timu hiyo.
Timu hiyo ilisemekana kupotea baada ya kushambuliwa hapo jumanne
katika kijiji kimoja kilicho karibu na Mji wa Nzerekore ulio kusini mwa Guinea.
Mlipuko wa Ugonjwa huo ndio hatari zaidi kote duniani kwa sasa,
huku viongozi wakitahadharisha kwamba huenda watu zaidi ya 20,000
wakaambukizwa.
Timu hiyo ya madaktari watatu na wanahabari watu walipotea baada
ya kushambuliwa kwa mawe na wakaazi wa kijiji cha Wome, walipofika katika
kijiji hicho kilicho karibu na mahala ambapo mlipuko wa Ebola ulianzia.
Kwa mujibu wa mwanahabari mmoja aliyeweza kunusurika aliwaambia
wanaripota kwamba alipokuwa amejificha, aliweza kusikia wakaazi hao wa Wome
wakiwatafuta.
Wajumbe wa serikali wakiongozwa na Waziri wa Afya walitumwa
maeneo hayo lakini hawangeweza kufika kwa kutumia barabara kwani daraja
lilikuwa limewekwa vizuizi.
Hapo Alhamisi msemaji wa serikali ya Guniea Albert Damantang
Camara alithibitisha kwamba maiti nane zilikuwa zimepatikana na miongoni mwa hizo
zilikuwa zile za wanahabari watatu.
Alieleza ya kwamba miili hiyo ilipatikana katika pipa moja la
shule ya msingi iliyo katika kijiji hicho, na kuongeza kuwa timu hiyo iliuawa
kinyama na wakaazi hao.
kwa hisani ya bbcswahili.com
No comments:
Post a Comment