Monday, July 18, 2016
Thursday, July 14, 2016
Tuesday, July 12, 2016
Mtoto apandikizwa pua mpya India
Madaktari nchini India wamepandikiza
pua mpya katika uso wa mvulana wa miaka 12 iliokuwa imemea katika paa lake la
uso.
Pua
ya Arun Patel iliharibika alipougua ugonjwa wa homa ya kichomi
Maambukizi
hayo yaliharibu pua yake akiwa mtoto mdogo.
Upandikizaji
kama huo ulifanywa nchini China mwaka 2013 ambapo mtu mmoja ambaye aliharibu
pua yake katika ajali alipewa pua mpya.
Wazazi
wa Arun walimchukua na kumpeleka katika daktari mwengine katika kijiji cha
jimbo la kati la Madhya Pradesh ambapo aliugua kichomi mda mfupi baada ya kuzaliwa.
Miaka
kadhaa baadaye,kundi moja la madaktari katika mji wa Indore liliamua kufanya
upasuaji usiokuwa wa kawaida ambapo Arun alipata pua mpya.
Mabaki ya Wafilisti yapatikana Israel
Watafiti wa mambo ya kale nchini Israel wamegundua makaburi ya kwanza ya
Wafilisti.
Makaburi hayo,
yaliyopatikana eneo la Ashkelon, yaligunduliwa mwaka 2013, lakini habari hizo
zilifichuliwa Jumapili.
Habari hizi ziliwekwa
siri muda huo wote kuzuia kushambuliwa na waandamanaji wa makundi ya Wayahudi
wahafidhina ambao hawakutaka makaburi hayo yafukuliwe.
Mafanikio
hayo yalitokea mwisho wa mwaka wa 30 wa uchimbaji ulioongozwa na kundi la Leon
Levy Expedition.
Viongozi
wa uchimbaji huo wanasema walipata makaburi yaliyozingirwa na manukato,
vyakula, mapambo, vito na silaha.
Yanadaiwa
kujengwa na kutumiwa kati ya karne ya 11 na karne ya 8 kabla ya kuzaliwa kwa
Yesu.
“Kwa
ugunduzi huu, tunakaribia kubaini siri za asili yao.”
![]() |
Profesa Lawrence E. Stager ni mmoja wa wanaoongoza utafiti huo |
Wanaakiolojia
hao sasa wanafanya uchunguzi wa DNA pamoja na uchunguzi wa miale ya ukaa
kubaini watu hao waliishi wakati gani.
Wafilisti
huoneshwa katika Biblia kama maadui wakuu wa Waisraeli, na inadhaniwa walihamia
Israel kutoka maeneo ya Magharibi karne ya 12 kabla ya kuzaliwa kwa Yesu.
Anayefahamika zaidi
ni Goliath, mpiganaji ‘jitu’ ambaye kwa mujibu wa Biblia, aliuawa na Daudi
kabla yake kuwa Mfalme wa Waisraeli.
Katika
Biblia, wanaoneshwa kama watu wakatili lakini mabaki yaliyopatikana yanaonekana
kuashiria kwamba walikuwa na ustaarabu fulani.
Habari kwa hisani ya BBCSwahili
Saturday, July 2, 2016
AZAM MARINE WAJA NA SEA TAX
Kampuni ya usafirishaji majini ya Azaam Marine imekuja na huduma mpya ya usafirishaji wa majini jijini Dar es salaam.
UJENZI WA DARAJA LA KONGOWE - KIGAMBONI WAENDELEA
Daraja linalounganisha maeneo ya Mbagala Kongowe na Kigamboni lililopo eneo la Mbagala Kongowe ambalo lilikuwa shida kupitika wakati wa mvua kubwa sasa linajeungwa upya.Daraja hili ni kiungo kikukwa sana kwa wakazi waishio maeno ya Toangoma,Kibada na Kigamboni Kutokea Mbagala Kongowe.
Friday, July 1, 2016
KUTOKA BUNGENI
Kutoka Bungeni jijini Dodoma ,Wabunge wa kambi rasmi ya Upinzani jana asubuhi waliingia Bungeni wakiwa wote wamevalia nguo nyeusi walipohudhuria kikao cha Bunge la Bajeti.Baada ya Naibu Spika Dk Tulia Ackson kuingia Bungeni na kuongoza dua ya kuliombea Bunge walianza kunyanyua mabango mbalimbali na kutoka nje
Subscribe to:
Posts (Atom)