Watafiti wa mambo ya kale nchini Israel wamegundua makaburi ya kwanza ya
Wafilisti.
Makaburi hayo,
yaliyopatikana eneo la Ashkelon, yaligunduliwa mwaka 2013, lakini habari hizo
zilifichuliwa Jumapili.
Habari hizi ziliwekwa
siri muda huo wote kuzuia kushambuliwa na waandamanaji wa makundi ya Wayahudi
wahafidhina ambao hawakutaka makaburi hayo yafukuliwe.
Mafanikio
hayo yalitokea mwisho wa mwaka wa 30 wa uchimbaji ulioongozwa na kundi la Leon
Levy Expedition.
Viongozi
wa uchimbaji huo wanasema walipata makaburi yaliyozingirwa na manukato,
vyakula, mapambo, vito na silaha.
Yanadaiwa
kujengwa na kutumiwa kati ya karne ya 11 na karne ya 8 kabla ya kuzaliwa kwa
Yesu.
“Kwa
ugunduzi huu, tunakaribia kubaini siri za asili yao.”
![]() |
Profesa Lawrence E. Stager ni mmoja wa wanaoongoza utafiti huo |
Wanaakiolojia
hao sasa wanafanya uchunguzi wa DNA pamoja na uchunguzi wa miale ya ukaa
kubaini watu hao waliishi wakati gani.
Wafilisti
huoneshwa katika Biblia kama maadui wakuu wa Waisraeli, na inadhaniwa walihamia
Israel kutoka maeneo ya Magharibi karne ya 12 kabla ya kuzaliwa kwa Yesu.
Anayefahamika zaidi
ni Goliath, mpiganaji ‘jitu’ ambaye kwa mujibu wa Biblia, aliuawa na Daudi
kabla yake kuwa Mfalme wa Waisraeli.
Katika
Biblia, wanaoneshwa kama watu wakatili lakini mabaki yaliyopatikana yanaonekana
kuashiria kwamba walikuwa na ustaarabu fulani.
Habari kwa hisani ya BBCSwahili
No comments:
Post a Comment