TANZANIA imetajwa kuwa ni miongoni mwa nchi zinazokabiliwa na tatizo la rushwa ndani ya jeshi.
Taasisi ya Transparency International (TI), ambayo hutafiti masuala ya rushwa duniani imeitaja Tanzania kwamba jeshi lake lina rushwa kubwa na ndogondogo.
Taasisi ya Transparency International (TI), ambayo hutafiti masuala ya rushwa duniani imeitaja Tanzania kwamba jeshi lake lina rushwa kubwa na ndogondogo.
Kwa mujibu wa gazeti dada la The Citizen la jana
Jumapili, uongozi wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) umekanusha vikali
taarifa ya taasisi hiyo.
TI inadai katika taarifa yake kuwa sekta ya ulinzi
ya Tanzania inakabiliwa na tatizo hilo na hiyo ni kutokana na mambo
yake kuendeshwa kwa usiri mkubwa.
“Hakuna kitu kibaya kama la rushwa kwenye jeshi,
maana kuna fedha nyingi inatembea kutokana na ughali wa vifaa vya
kijeshi. Bado Serikali nyingi zinafanya mambo haya kuwa siri na kutoa
mwanya kwa rushwa kutembea.
“Fedha inayotumika vibaya kwa masuala ya kijeshi, ingeweza kutumia vizuri zaidi katika masuala ya maendeleo,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo iliyoandikwa na Mark Pyman, ambaye ni Mkurugenzi wa Kitengo cha masuala ya Ulinzi cha Transperancy International.

Transparency International inaeleza kuwa fedha ya
rushwa inayotembea kwenye sekta ya ulinzi inakadiriwa kufikia kiasi cha
Dola 20 bilioni (Sh32 trilioni).
“Ripoti ya Transparency International itufungue
macho Watanzania maana kwa kawaida huwa kila watu wakihoji mapato na
matumizi ya jeshi tunaambiwa hatuwezi kujibiwa kwa madai ya woga wa
kuhatarisha usalama wa taifa,” alikaririwa mbunge mmoja na gazeti la The
Citizen.
Tanzania, hata hivyo, iko juu ya nchi nyingi za
Afrika kwa tatizo la rushwa ingawa inatakiwa kurekebisha mianya mingi
kwenye sekta hiyo.
“Tunaona Tanzania ina changamoto ya kuimarisha
vyombo vya kutupa jicho kwenye jeshi. Mathalani, kuna Kamati ya Bunge ya
Ulinzi na Mambo ya Nje, lakini haina meno ya kuingia kwa undani masuala
ya kijeshi,” iliongeza Transparency International.
Msemaji wa JWTZ, Kanali Kapambala Mgawe, hata hivyo, alikaririwa na gazeti la The Citizen akidai kuwa taasisi yake imekuwa ikifanya kazi kitaalamu na kimaadili akitolea mfano jinsi wanavyoajiri wanajeshi kwa kufuata vigezo.

Transparency International inasema kuwa kuna
Kitengo cha Utawala Bora cha Serikali ambacho hufanya ukaguzi kwenye
jeshi ingawa halijatoa ripoti ya aina yoyote kuhusiana na ukaguzi wa
bajeti ya jeshi. “Mfano kuna taarifa kuwa Kitengo cha Kilimo cha Jeshi
la Kujenga Taifa (Suma-JKT) kuna kinajishughulisha na uchimbaji madini
na biashara nyingine lakini kuna udhibiti mdogo,” iliongeza taarifa yao.
Julai mwaka jana, maofisa saba waandamizi wa Bodi
ya Zabuni ya Suma-JKT walifunguliwa mashitaka ya matumizi mabaya ya
ofisi na uhamishaji usio wa halali wa zaidi ya Sh 3.8 bilioni.
Waliotuhumiwa ni pamoja na Kanali Ayoub Mwakang’ata, Luteni Kanali Mkohi Kichogo, Luteni Kanali Paul Mayavi, Meja Peter Lushika, Sajini John Laizer, Meja Yohana Nyuchi na Luteni Kanali Felix Samillan wanaodaiwa kufanya makosa hayo mwaka 2009.

Tanzania imewekwa katika Kundi D kwenye orodha
hiyo ya Transperancy International ya nchi zinazokabiliwa na kiwango cha
juu cha rushwa na vigezo vinavyoangaliwa ni sekta za siasa, fedha,
utumishi wa Kundi la D ni nchi ambazo zinakabiliwa na kiwango cha juu
cha rushwa na katika orodha hiyo zimo pia nchi za Russia na China.
Hata hivyo, nchi zenye kiwango cha juu cha rushwa
ziko katika Kundi F wakati zile zenye kiwango cha chini cha rushwa ziko
Kundi A.
Source:Mwananchi
Source:Mwananchi
No comments:
Post a Comment