Wednesday, December 6, 2017
MWANAFUNZI AJIFANYA ASKARI WA JWTZ
Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam, inamshikilia
mwanafunzi wa Sekondari ya Fahari iliyopo Goba, mwenye miaka 17 kwa kosa la
kukutwa amevaa sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Kamanda Mambosasa amesema katika mahojiano ya awali, kijana
huyo alijitambulisha kuwa ni askari kutoka 501 KJ Lugalo jijini Dar es Salaam.
Amesema baada ya kubanwa alikiri kupata sare hizo kwa rafiki
zake na upekuzi ulipofanywa ndani ya begi alilokuwa nalo alikutwa na kofia
nyingine moja ya jeshi hilo.
Pia, alikutwa na kitambulisho cha mtoto wa askari wa JWTZ
Private Gabriel Kiwila wa 501 KJ. (Picha kwa hisani ya Mwananchi).
Subscribe to:
Posts (Atom)