Tuesday, February 12, 2013

Makamu Mwenyekiti Chadema atinga CCM, Kikwete ampokea


Juliana Shoza akiwa ndani ya sare za CCM

Aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema (Bavicha) Juliana Shonza amehamia CCM rasmi na kupata mapokezi makuwa kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama hicho Rais Jakaya Kikwete.
Taarifa za Shonza kupokelewa katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM kinachoendelea Dodoma tangu juzi zimenaswa hivi punde.
Shonza alitimuliwa Chadema January 6 mwaka huu pamoja na baadhi ya wanachama wengine akiwemo Mtela Mwampamba, na  Habib Mchange wamefukuzwa uanachama katika chama hicho huku wengine wakisimamishwa uongozi na wengine kupewa onyo kali.
Hatua hiyo ilitafsiriwa kuwa ni msimamo wa Dk Slaa pamoja na mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe ambao wanaelezwa kuwa wanakisafisha chama kwa lengo la kuingia Ikulu kwa kishindo mwaka 2015.

No comments:

Post a Comment