Monday, November 14, 2016
Friday, November 11, 2016
Thursday, November 10, 2016
Wednesday, November 9, 2016
Tuesday, November 8, 2016
Thursday, November 3, 2016
Kenya yatangaza kuondoa wanajeshi Sudan Kusini
Kenya imetangaza kuwa inawaondoa
wanajeshi wake kutoka kikosi maalumu cha Umoja wa Mataifa cha kudumisha amani
kilichoko Sudan Kusini, baada ya kamanda wake kutimuliwa kazini.
Wizara
ya Mashauri ya Kigeni imesema kuwa utaratibu wa kumuachisha kazi Jemedari
Johnson Mogoa Kimani Ondieki haukuwa na uwazi.
Katibu
Mkuu wa UN Ban Ki-moon alimfuta kazi Luteni Kanali Johnson Ondieki baada ya
ripoti ya uchunguzi kusema alikosa kuwajibika kulinda raia mapigano yalipozuka
upya nchini Sudan Kusini mwezi Julai.
Ripoti
hiyo imesema walinda amani waliokuwa chini ya jemedari huyo hawakuchukua hatua
yoyote wanajeshi wa serikali waliposhambulia kituo cha utoaji misaada mjini
Juba na kuwadhulumu raia.
Kenya
imesema uamuzi huo si wa haki na kutangaza kwamba itayaondoa mara moja majeshi
yake yanayohudumu chini ya UN nchini Sudan.
Kadhalika,
Kenya imejiondoa kutoka kwa mpango wa kutuma wanajeshi wa ziada kutoka nchi za
kanda ambao walitarajiwa kutumwa kuimarisha kikosi cha UN nchini humo.
Kwenye
taarifa yake, Kenya imesema kwa kumfuta Jenerali Gen Ondieki, Bw Ban alikosa
kuangazia kiini cha matatizo yaliyobainika kwenye ripoti hiyo ya uchunguzi.
Habari kwa hisani ya bbcswahili.com
Wednesday, November 2, 2016
RAISI MAGUFULI AWASILI KUTOKA ZIARA YA NCHINI KENYA
Rais Magufuli akilakiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Nairobi, Kenya.
- Alikuwa nchini Kenya katika ziara ya Kiserikali ya siku mbili
Mh.Raisi akisalimiana na viongozi wa juu Serikalini mara baada ya kutua
Subscribe to:
Posts (Atom)