Friday, January 10, 2014

Kenya:Al shabaab yapata kipigo

Jeshi la Kenya linalopambana na kundi la wanamgambo la al-Shabaab linasema angalau wapiganaji 30 wa kundi hilo wameuawa Kusini Magharibi mwa Somalia.
Msemaji wa jeshi hilo Meja Emmanuel Chirchir ameelezea kuwa jeshi la Kenya lilishambulia kwa mabomu mojawapo ya kambi za kundi hilo katika eneo la Gedo , Alhamisi Jioni.
Aliongeza kwamba miongoni mwa waliofariki ni makamanda kadhaa wa kundi hilo.
Al Shabaab hata hivyo hawajatoa tamko lolote kuhusu shambulizi hilo.
Kadhalika Al Shabaab walikiri kufanya shambulizi la kigaidi mjini Nairobi mwaka jana dhidi ya jengo la kifahari la Westgate na kuwaua watu 70.
Kenya imekuwa ikipambana na wapiganaji wa kundi hilo tangu mwaka 2011 Oktoba wanajeshi wake walipojiunga rasmi na vikosi vya muungano wa Afrika ambavyo tayari vilikuwa nchini Somalia kwa kazi hiyo.
Rais Uhuru Kenyatta ameahidi kuwa majeshi ya Kenya yataendelea va vita dhidi ya wanamgambao hao tangu waliposhambulia Kenya mwaka jana.

No comments:

Post a Comment