Monday, December 17, 2012

WAKAMATWA AFRIKA KUSINI

Njama ya kushambila mkutano wa wajumbe wakuu wa chama tawala nchini Afrika Kusini, cha African national Congress ANC, imetibuliwa.
Msemaji wa polisi nchini humo amethibitisha tukio hilo, na kusema kuwa washukiwa wanne wenye asili ya kizungu wenya itikadi za siasa kali wamekamatwa.
Rais Jacob Zuma, na maafisa wengine wakuu wa serikali na wa chama hicho wanaohudhuria mkutano huo unaoendelea Mangaung, wamepewa ulinzi mkali.
Viongozi wapya wa chama hicho wanatarajiwa kuchaguliwa na wajumbe hao.
Chama cha ANC, kimekuwa madarakani tangu kumalizika kwa utawala wa wazungu walio wachache mwaka wa 1994.
Msemaji wa polisi Phuti Setati, ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa washukiwa wanne ambao walikuwa wakipanga jinsi ya kuuweka bomu katika eneo la mkutano huo, unaofanyika katika chuo kikuu cha Free State iliyoko katika eneo la Mangaung.

No comments:

Post a Comment