Saturday, December 1, 2012

JIHADHARI KIGOGO MBUYUNI

Maeneo ya Kigogo Mbuyuni limeibuka kundi la vijana wenye umri kati ya miaka 12-14,linalojiita Panya Road ambalo limekuwa likihatarisha maisha ya wananchi wa maeneo hayo na wapitao maeneo hayo.Kundi hilo ambalo huwa na vijana kati ya 20 na 25 na wanatembea na mapanga na wakikutana na mtu yeyote wanafanya vitendo vya kialifu.Wananchi wa maeneo hayo wamelalamika juu ya kundi hilo.Wakati huohuo Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni Kamanda Charles Kenyela ametoa taadhari kwa kundi hilo kwa kuwa sasa watakuwa makini ili kulidhibiti kundi hilo.  

No comments:

Post a Comment