Wednesday, July 22, 2015
Monday, July 20, 2015
Friday, July 17, 2015
Thursday, July 16, 2015
Wednesday, July 15, 2015
MWADUI KUTIMKIA AFRIKA KUSINI KUJIFUA
![]() |
Kikosi cha Mwadui FC |
Kocha
wa timu ya Mwadui FC ya Shinyanga Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amesema wanatarajia
kuuomba uogozi wa matajiri hao wa kanda ya ziwa kukiwezesha kikosi hicho kwenda
nchini Afrika Kusini kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa 2015-2016 ambapo
wao watashiriki ligi hiyo.
“Tunashukuru Mungu timu yetu imeanza ‘pre-season’ vizuri tukiwa na
wachezaji wetu wote wapya tuliowasajili pamoja na walioipandisha timu hii,
pre-season inaendelea vizuri tena sana kama tutaendelea hivi basi naamini
tutakujakuwa washindani kama ilivyokuwa Kajumulo enzi za uhai wake”, amesema
Julio, kocha mkuu wa Mwadui FC.
“Sunday Kayuni yeye ni ‘consultant’ kwahiyo amekuja huku kwa kazi hiyo na
yeye anatoa ushauri wa hapa na pale lakini tunafanya kazi kubwa kusema kweli
tunafurahia uwepo wake kwasababu yeye anaupeo mkubwa, kwahiyo tunaamini katika
huo u-consultant wake atatusaidia kwa namna moja au nyingine”, ameeleza.
“Tumeuomba uongozi ili tuone kama tunaweza kupata safari ya South Africa
maana sisi (Mwadui Mining) kule ndio makao makuu yetu ili tuweze kuendelea na
pre-season kidogo kuimalizia na baadae kupata mechi za kirafiki ambazo
zitatuweka pazuri”, ameongeza.
“Mbeya City walifanya vizuri kwasababu wako nje ya Dar es Salaam,
Dar es Salaam kuna vishawishi vingi sana lakini unapokuwa sehemu kama Mbeya,
kule unafanya mazoezi magumu ambayo yanaingia ndani ya mwili, kwahiyo sisi hapa
kwetu Mwadui ni sehem nzuri tupo mgodini tuna uwanja mzuri ambao nafikiri
katika Tanzania ni uwanja wa pili baada ya uwanja wa Taifa”, alimaliza Julio.
Source:http://shaffihdauda.co.tz/
Saturday, July 11, 2015
KITUO CHA POLISI BUNJU A CHACHOMWA MOTO
Wananchi wenye hasira waishio maeneo ya Bunju A wamechukua hatua hiyo ya kukichoma kituo hicho kidogo cha Polisi baada ya Gari kumgonga mtoto wa shule ya Msingi ya Bunju A na kufa hapo hapo.
Baada ya tukio hilo la kugongwa mtoto huyo,wanafuzi walikusanyika na kufunga barabara hiyo ya bagamoyo kwa kuishinikiza Tanroad kuweka matuta katika eneo hilo.Baada ya Muda si mrefu wananchi wa eneo hilo wenye hasira kali walichukua hatua hiyo ya kukivamia kituo hicho kilicho maeneo hayo na kuanza kukichoma moto na baadae Jeshi la Polisi kufika na kuwatanyisha wananchi hao.
Baadhi ya wanachi wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo

MAKADA WA CCM WAJITENGA NA MAAMUZI YA KIKAO
Wajumbe wa kamati kuu ya CCM hajakubaliana na maamuzi yaliyotoka kwenye kikao kilichofanyika jana usiku kuwateua wagombea wa nafasi ya Urais kupitia CCM kwa kutofuata katiba ,wanasema kikao hakikupokea majina yote, kililetewa majina machache yaliyojadiliwa na kamati ya maadili,Pia anasema katiba inataka mtu anayekubalika ndiye apewe nafasi lakini kikao kiliminya wanaokubalika kwa maslahi ya wasiokubalika haya yalisemwa na Mh.Nchimbi mbele ya waandishi wa habari,kwa sababu hiyo wajumbe hao wa kamati kuu ambao ni mh.Kimbisa,mh Sofia Simba na Mh.Nchimbi,wamejitenga na maamuzi ya kikao hicho na kutoyaunga mkono
Friday, July 10, 2015
Ugiriki yatoa mapendekezo mapya kwa wakopeshaji wake
Viongozi wa Ugiriki wametuma mapendekezo ya mageuzi ili
kupata makubaliano na wakopeshaji wake na kukomesha mgogoro unaoendelea.
Viongozi hao wamepania hasa kuongeza
VAT na mageuzi ya pensheni. Mapendekezo ambayo, dhidi ya matatizo yote,
hayaonekani kuwa tofauti sana na kile kilichokuwa kinatakiwa na wakopeshaji wa
Athens, ambao wanapaswa kuyajadili leo Ijumaa asubuhi.
Ugiriki hatimaye imetuma
mapendekezo yake kwa ajili ya mageuzi kabla ya kutamatika kwa muda wa mwisho
uliyowekwa na viongozi wa Ulaya. Mapendekezo hayo yanapaswa kufuata mkondo wa
masharti yaliyopendekezwa na wakopeshaji wa wake.
Serikali ya Ugiriki
imejikubalisha kuongeza VAT kwa asilimia 23 kwa ajili ya chakula na asilimia 13
kwa ajili ya hoteli. Serikali ya Ugiriki pia imepania kufuta au kusamehe
polepole VAT zinazotozwa katika visiwa vya Ugiriki.
Ugiriki pia imepania kuongeza
kodi katika makampuni makubwa na mashrika mengine yasiyo ya kiserikali. Kodi
kwa bidhaa za anasa na matangazo ya biashara kwenye televisheni itawekwa mara
moja. Bajeti takatifu katika sekta ya ulinzi itapunguzwa Euro milioni 300 na
ubinafsishaji uliosimamishwa baada ya Alexis Tsipras kuchukua hatamu ya uongozi
wa nchi, utarejeshwa.
Mageuzi mapya ya pensheni pia
yanatazamiwa pia kufanyika. Umri wa miaka 67 unapaswa kuwa kigezo cha kukatisha
tamaa ya kustaafu mapema pamoja na kufuta au kusamehe polepole posho ya
mshikamano (EKAS).
Kulingana na nakala ya
mapendekezo iliyotolewa na serikali ya Ugiriki, Ugiriki inataka suluhisho
" ili kurekebisha" madeni yake makubwa, kwa asilimia 180 ya Pato la
Taifa, pamoja na "pakiti ya Euro bilioni 35" iliyotengwa kwa ukuaji.
Serikali ya Ugiriki imesema pia iko mbioni kutafuta fedha kwa jumla ya Euro
bilioni 53.5 ifikapo mwishoni mwa mwezi Juni mwaka 2018 ili kufidia majukumu
yake yanayohusiana na malipo yake ya mkopo.
Alshabab lawaachilia wanajeshi 2 wa Kenya
Polisi nchini Kenya wanasema kuwa
maafisa wawili wa jeshi la Kenya waliotekwa na wanamgambo ya AL Shabaab yapata
miaka miwili iliyopita wameachiliwa huru.
Mkuu
wa polisi Joseph Boinnet amesema kuwa wanajeshi hao walikuwa wanahamishwa
hamishwa upande wa Somalia kutoka kambi moja ya Al shabaab hadi nyingine.
Hakutoa
maelezo zaidi juu ya namna walivyoachiliwa lakini amesema kuwa wako katika hali
nzuri ya afya.
MESSI SINGANO AMWAGA WINO AZAM FC
Mchezaji wa zamani wa Simba Messi Singano,amesajiliwa na Timu ya Azam FC kwa mkataba wa miaka 2.
Hii inaonyesha kuwa Messi alikuwa amepania kujiunga na timu hiyo ya Azam FC baada ya kumalizana na Simba iliyomkuza.
Hii inaonyesha kuwa Messi alikuwa amepania kujiunga na timu hiyo ya Azam FC baada ya kumalizana na Simba iliyomkuza.
![]() |
Messi akisaini mkataba huo mbele ya viongozi wa Azam FC |
![]() |
Uzi mpya atakaotinga Messi akiwa na Azam FC |
Wednesday, July 8, 2015
MAYWEATHER UVULIWA MKANDA WA UBINGWA
Hatua za kuvuliwa mkanda huo wa ubingwa wa WBO,uzito wa Welterweight unaohusisha kilo 67 na 77 ambao alishinda mwezi mei mwaka huu dhidi ya Manny Pacquiao kutokana na kushindwa kufuata sheria na kanuni za Shirikisho holo.
Kamati ya Mashindanoya WBO imesema kwamba haina jinsi ya kufanya zaidi ya kumvua mkanda huo Mayweather ambaye ameshindwa kulipa ada kutoka kwenye pambano alilopigana na Pacquiao.
Siku ya Ijumaa iliyopita ndio ilikuwa mwisho kwa Mayweather kutimiza vigezo hivo vya ubingwa wa WBO ikiwemo kulipa ada ya dola 200,000 kutoka katika pambano lake na Pacquiao pamoja na kujivua ubingwa wa uzito wa lightmiddleweight wa WBCna WBA

ZOEZI LA UANDIKISHWAJI DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA LAPIGA HODI MKOA WA PWANI
Jumla ya watu 11,248,194 wamekwishwa andikikishwa kwenye Daftari la kudumu la wapiga kura zoezi ambalo bado linaendelea kwa sasa nchini likiwa limepiga hodi mkoani Pwani.
Haya yalisemwa na Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi ya Taifa Ndg.Damiani Lubuva kijijini Msoga kata ya Msoga wilayani Bagamoyo mbele ya Mh.Raisi Dk.Jakaya Kikwete mara baada ya kujiandikisha.
Bw.Lubuva alisema kuwa lengo la Tume ni kuandikisha Watanzania Milioni 21 hadi23 kote nchinimara zoezi hilo litakapofikia tamati kati ya mwezi Julai na Agosti mwanzoni kama hakutatokea matatizo
Anasema changamoto zilizojitokeza ni za kawaida hasa kutokana na mfumo huo kuwa ni mpya hivyo lazima kuwe na changamoto kama ilivyo kwenye jambo lolote jipya lazima liwe na changamoto zake
Mkoa wa Pwani unajumla ya vituo 1,752 vya kujiandikisha na mashine 932 ambapo kata ya Msoga kuna jumla ya vituo 17.Zoezi hilo lilianza jana na litamalizika Julai 20.
Ni fursa kwa wakazi wa Mkoa wa Pwani kujiandikisha katika daftari lakudumu la kupiga kura na kupata nafasi ya kuchagua viongozi wanaowataka katika uchaguzi.

Raisi Akijiandikisha kwenye Mfumo Mpya wa Kielekroniki wa BVR |
![]() |
Raisi akichukuliwa Alama ya Vidole na Afisa Tehama wa Tume |
![]() |
Raisi akipokea kitambulisho chake cha kupiga Kura kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume Bw.Lubuva Picha kwa hisani ya Michuzi Blog |
Monday, July 6, 2015
BASIL MRAMBA NA DANIEL YONA WAHUKUMIWA
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam imewahukumu kwenda jela miaka mitatu aliyekuwa waziri wa fedha wa zamami Basil Mramba na aliyekuwa waziri wa Madini na Nishati wa zamani Daniel Yona baada ya kukutwa na hatia ya uhujumu uchumi na matumizi mabaya ya ofisi na kuisababishia Serikali hasara ya Sh.Bilioni 11.7
Subscribe to:
Posts (Atom)