![]() |
Kikosi cha Mwadui FC |
Kocha
wa timu ya Mwadui FC ya Shinyanga Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amesema wanatarajia
kuuomba uogozi wa matajiri hao wa kanda ya ziwa kukiwezesha kikosi hicho kwenda
nchini Afrika Kusini kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa 2015-2016 ambapo
wao watashiriki ligi hiyo.
“Tunashukuru Mungu timu yetu imeanza ‘pre-season’ vizuri tukiwa na
wachezaji wetu wote wapya tuliowasajili pamoja na walioipandisha timu hii,
pre-season inaendelea vizuri tena sana kama tutaendelea hivi basi naamini
tutakujakuwa washindani kama ilivyokuwa Kajumulo enzi za uhai wake”, amesema
Julio, kocha mkuu wa Mwadui FC.
“Sunday Kayuni yeye ni ‘consultant’ kwahiyo amekuja huku kwa kazi hiyo na
yeye anatoa ushauri wa hapa na pale lakini tunafanya kazi kubwa kusema kweli
tunafurahia uwepo wake kwasababu yeye anaupeo mkubwa, kwahiyo tunaamini katika
huo u-consultant wake atatusaidia kwa namna moja au nyingine”, ameeleza.
“Tumeuomba uongozi ili tuone kama tunaweza kupata safari ya South Africa
maana sisi (Mwadui Mining) kule ndio makao makuu yetu ili tuweze kuendelea na
pre-season kidogo kuimalizia na baadae kupata mechi za kirafiki ambazo
zitatuweka pazuri”, ameongeza.
“Mbeya City walifanya vizuri kwasababu wako nje ya Dar es Salaam,
Dar es Salaam kuna vishawishi vingi sana lakini unapokuwa sehemu kama Mbeya,
kule unafanya mazoezi magumu ambayo yanaingia ndani ya mwili, kwahiyo sisi hapa
kwetu Mwadui ni sehem nzuri tupo mgodini tuna uwanja mzuri ambao nafikiri
katika Tanzania ni uwanja wa pili baada ya uwanja wa Taifa”, alimaliza Julio.
Source:http://shaffihdauda.co.tz/
No comments:
Post a Comment