Viongozi wa Ugiriki wametuma mapendekezo ya mageuzi ili
kupata makubaliano na wakopeshaji wake na kukomesha mgogoro unaoendelea.
Viongozi hao wamepania hasa kuongeza
VAT na mageuzi ya pensheni. Mapendekezo ambayo, dhidi ya matatizo yote,
hayaonekani kuwa tofauti sana na kile kilichokuwa kinatakiwa na wakopeshaji wa
Athens, ambao wanapaswa kuyajadili leo Ijumaa asubuhi.
Ugiriki hatimaye imetuma
mapendekezo yake kwa ajili ya mageuzi kabla ya kutamatika kwa muda wa mwisho
uliyowekwa na viongozi wa Ulaya. Mapendekezo hayo yanapaswa kufuata mkondo wa
masharti yaliyopendekezwa na wakopeshaji wa wake.
Serikali ya Ugiriki
imejikubalisha kuongeza VAT kwa asilimia 23 kwa ajili ya chakula na asilimia 13
kwa ajili ya hoteli. Serikali ya Ugiriki pia imepania kufuta au kusamehe
polepole VAT zinazotozwa katika visiwa vya Ugiriki.
Ugiriki pia imepania kuongeza
kodi katika makampuni makubwa na mashrika mengine yasiyo ya kiserikali. Kodi
kwa bidhaa za anasa na matangazo ya biashara kwenye televisheni itawekwa mara
moja. Bajeti takatifu katika sekta ya ulinzi itapunguzwa Euro milioni 300 na
ubinafsishaji uliosimamishwa baada ya Alexis Tsipras kuchukua hatamu ya uongozi
wa nchi, utarejeshwa.
Mageuzi mapya ya pensheni pia
yanatazamiwa pia kufanyika. Umri wa miaka 67 unapaswa kuwa kigezo cha kukatisha
tamaa ya kustaafu mapema pamoja na kufuta au kusamehe polepole posho ya
mshikamano (EKAS).
Kulingana na nakala ya
mapendekezo iliyotolewa na serikali ya Ugiriki, Ugiriki inataka suluhisho
" ili kurekebisha" madeni yake makubwa, kwa asilimia 180 ya Pato la
Taifa, pamoja na "pakiti ya Euro bilioni 35" iliyotengwa kwa ukuaji.
Serikali ya Ugiriki imesema pia iko mbioni kutafuta fedha kwa jumla ya Euro
bilioni 53.5 ifikapo mwishoni mwa mwezi Juni mwaka 2018 ili kufidia majukumu
yake yanayohusiana na malipo yake ya mkopo.
No comments:
Post a Comment