Wednesday, December 6, 2017
MWANAFUNZI AJIFANYA ASKARI WA JWTZ
Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam, inamshikilia
mwanafunzi wa Sekondari ya Fahari iliyopo Goba, mwenye miaka 17 kwa kosa la
kukutwa amevaa sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Kamanda Mambosasa amesema katika mahojiano ya awali, kijana
huyo alijitambulisha kuwa ni askari kutoka 501 KJ Lugalo jijini Dar es Salaam.
Amesema baada ya kubanwa alikiri kupata sare hizo kwa rafiki
zake na upekuzi ulipofanywa ndani ya begi alilokuwa nalo alikutwa na kofia
nyingine moja ya jeshi hilo.
Pia, alikutwa na kitambulisho cha mtoto wa askari wa JWTZ
Private Gabriel Kiwila wa 501 KJ. (Picha kwa hisani ya Mwananchi).
Thursday, November 30, 2017
Raisi wa Nigeria apinga raia wake kuuzwa kama mbuzi Libya
Raisi wa Nigeria Muhammadu
Buhar amesemaraia wote wa Nigeria ambao wamekwama Libya watarejeshwa nyumbani.
Amesema hayo baada ya video
za hivi karibuni mitandaoni zikionyesha waafrika wakiuzwa kwenya soko la mnada
wa watumwa huko nchini Libya
Buhari amesema”baadhi ya raia
wa Nigeria wanauzwa kama mbuzi dola kadhaa Libya”
Kwenye video iliyotolewa na
shirika la habari la CNN mapema mwezi huu ,vijana kutoka mataifa ya Afrika
kusini mwa jangwa la Salahara walionekana wakiuzwa kama wafanyakazi wa mashambani
.
Walikuwa wakiuzwa $400 katika
eneo ambalo halikuwekwa wazi huko Libya
Wednesday, November 29, 2017
SIMBA YALETA BEKI WA GHANA KUCHUKUA NAFASI YA MAVUGO
Klabu ya Simba ipo kwenye hatua za
mwisho kumalizana na beki kisiki raia wa Ghana, Malik Ismaila wa Tema Youth,
kwa mujibu wa Mwanaspoti umeripoti kuwa nyota huyo tayari yupo Dar es salaam na
dili lake likifanikiwa anatarajiwa kuchukua nafasi ya Laudit Mavugo ambaye
anatarajiwa kutolewa kwa mkopo katika klabu ya Gor Mahia
kwa hisani ya:http://www.goal.com/sw
Makamu wa rais wa Tanzania amtembelea Tundu Lissu Hospitalini Nairobi
Makamu wa Raisi wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan
amemtembelea Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu ambaye amelazwa katika
hospitali ya Nairobi ambapo anaendelea na Matibabu.Makamu wa Raisi alimtembelea
Mbunge huyo wa Singida Mashariki muda
mfupi baada ya kuhudhuria kuapishwa kwa Raisi wa Taifa la Kenya Uhuru Kenyatta
tarehe 28November 2017.
Mheshimiwa Lissu amekuwa akipata matibabu katika hospitali
hiyo tangu Septemba 7 baada ya shambulio la kupigwa risasi na watu
wasiojulikana katika jaribio la mauaji huko nyumbani kwake mjini Dodoma
Friday, February 17, 2017
Thursday, February 9, 2017
Wednesday, February 8, 2017
Subscribe to:
Posts (Atom)