Makamu wa Raisi wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan
amemtembelea Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu ambaye amelazwa katika
hospitali ya Nairobi ambapo anaendelea na Matibabu.Makamu wa Raisi alimtembelea
Mbunge huyo wa Singida Mashariki muda
mfupi baada ya kuhudhuria kuapishwa kwa Raisi wa Taifa la Kenya Uhuru Kenyatta
tarehe 28November 2017.
Mheshimiwa Lissu amekuwa akipata matibabu katika hospitali
hiyo tangu Septemba 7 baada ya shambulio la kupigwa risasi na watu
wasiojulikana katika jaribio la mauaji huko nyumbani kwake mjini Dodoma
No comments:
Post a Comment