Thursday, November 30, 2017

Raisi wa Nigeria apinga raia wake kuuzwa kama mbuzi Libya

Raisi wa Nigeria Muhammadu Buhar amesemaraia wote wa Nigeria ambao wamekwama Libya watarejeshwa nyumbani.
Amesema hayo baada ya video za hivi karibuni mitandaoni zikionyesha waafrika wakiuzwa kwenya soko la mnada wa watumwa huko nchini Libya
Buhari amesema”baadhi ya raia wa Nigeria wanauzwa kama mbuzi dola kadhaa Libya”
Kwenye video iliyotolewa na shirika la habari la CNN mapema mwezi huu ,vijana kutoka mataifa ya Afrika kusini mwa jangwa la Salahara walionekana wakiuzwa kama wafanyakazi wa mashambani .
Walikuwa wakiuzwa $400 katika eneo ambalo halikuwekwa wazi huko Libya                                                     


 Picha kwa hisani ya cnn.com



MAJALIWA NAYE AWASHA MOTO BANDARINI DAR

Wednesday, November 29, 2017

Raila atishia kujiapisha kama rais siku kuu ya Jamhuri Dei

SIMBA YALETA BEKI WA GHANA KUCHUKUA NAFASI YA MAVUGO

Klabu ya Simba ipo kwenye hatua za mwisho kumalizana na beki kisiki raia wa Ghana, Malik Ismaila wa Tema Youth, kwa mujibu wa Mwanaspoti umeripoti kuwa nyota huyo tayari yupo Dar es salaam na dili lake likifanikiwa anatarajiwa kuchukua nafasi ya Laudit Mavugo ambaye anatarajiwa kutolewa kwa mkopo katika klabu ya Gor Mahia


kwa hisani ya:http://www.goal.com/sw

Makamu wa rais wa Tanzania amtembelea Tundu Lissu Hospitalini Nairobi

Makamu wa Raisi wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan amemtembelea Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu ambaye amelazwa katika hospitali ya Nairobi ambapo anaendelea na Matibabu.Makamu wa Raisi alimtembelea Mbunge huyo wa Singida Mashariki  muda mfupi baada ya kuhudhuria kuapishwa kwa Raisi wa Taifa la Kenya Uhuru Kenyatta tarehe 28November 2017.

Mheshimiwa Lissu amekuwa akipata matibabu katika hospitali hiyo tangu Septemba 7 baada ya shambulio la kupigwa risasi na watu wasiojulikana katika jaribio la mauaji huko nyumbani kwake mjini Dodoma