Thursday, January 10, 2013

OMARY OMARY AZIKWA KATIKA MAZINGIRA YA VURUGU

MWANAMUZIKI mkongwe wa miondoko ya mnanda, Omar Omar Mfungilo, ambaye alifariki usiku wa kuamkia jana ( Jumatatu) nyumbani kwao Temeke-Mkoroshini amezikwa leo katika
makaburi ya karibu na nyumbani kwao.

Mazishi hayo ambayo yalihudhuriwa na watu wengi, yalitawaliwa na vurugu ambazo zilisababisha baadhi ya waombolezaji kuporwa vitu vyao kama simu, pesa, saa na vitu vingine.

Wakati wa kwenda kumzika, vijana waliojiita ‘kikosi kazi cha mazishi’ waling’ang’ania jeneza lililobeba mwili wa marehemu na kulipeleka wao makaburini huku baadhi yao wakifanya vitendo vya uporaji njiani wakati wa kwenda kumzika.







Dully akiwa na Sunche na Kapeto

Baadhi ya wanamuziki wa kizazi kipya

Mwili wa marehemu ukisaliwa nyumbani kabla ya kupelekwa makaburini, na hapa ni kabla ya vurugu

Mlevi akicheza mbele ya waombolezaji

No comments:

Post a Comment