Raisi wa Burundi Pierre Nkurunzizaamewatangazia raia wake
kuwa sasa amani imerejea nchini humo ikiwa ni siku tatu baada ya kushindwa kwa
jaribio la mapinduzi ya kijeshi.
Akihutubia
wananchi kupitia runinga Pierre Nkurunziza ametoa onyo juu ya jaribio lingine
lolote la kuchukua madaraka kwa nguvu litasababisha vita umasikini na majanga
yalikwisha onekana katika taifa hilo.
Hayo
yanajiri wakati Marekani ikitoa onyo hapo jana kwa raisi wa Burundi Pierre
Nkurunziza kuhusu kutowania muhula wa tatu wa uongozi kwa vile kutazorotesha
usalama nchini humo na kutishia misaada ya kimataifa.
Msemaji
wa Washington Jeff Rathke ameeleza kuwa Marekani inawasiwasi kufuatia uwezekano
wa kutokea ghasia zaidi baada ya raisi Nkurunziza kurejea nchini Burundi.
Msemaji
wa washington amesema kuwa marekani bado inamtambua Nkurunzinza kama raisi
halali wa Burundi licha ya kusisitiza kiongozi huyo kutowania muhula wa tatu.
Baadhi ya
maafisa wa kijeshi walioshiriki kuongoza mapinduzi wamekamatwa huku wengine
wakitokomea na kusakwa na majeshi tiifu kwa serikali akiwemo kiongozi wa mapinduzi
hayo Generali Godefroid Niyombare, ambaye awali aliiambia AFP kuwa
angejisalimisha kwa serikali.
No comments:
Post a Comment