Raia wa
Brazili wanaomboleza vifo vya watu mia mbili thelathini na watatu waliofariki
dunia katika ajali ya moto iliyotokea kwenye ukumbi wa muziki katika mji wa
kusini wa Santa Maria.
Maafisa
wanasema kuwa wengi wa waathiriwa walikuwa ni wanafunzi waliokufa baada ya
kushindwa kupumua kutokana na moshi mkubwa .
Wengine
zaidi ya mia moja wanapata matibabu hospitalini . Serikali ya Brazil imetangaza
siku tatu za maombolezo . Taarifa zinasema kuwa moto huo ulianza wakati
waimbaji wa bendi moja walipowasha fataki.
Maswali
sasa yamekuwa yakiulizwa kuhusu usalama wa kumbui za starehe, huku kukiwa na
madai kuwa cheti cha huduma za zima moto kilikuwa kimepitwa na wakati. Hili ni
jana kubwa la moto kuwahi kuikumba Brazil kwa zaidi ya miongo mitano
Familia
za waathiriwa wamekuwa wakiomboleza juu ya majeneza za jamaa zao katika ukumbi
wa mamozezi ambao unatuimika kama jumba la kuhifadhia maiti.
Kwa
sababu ya heshima kwa waliofariki, serikali iliakhirisha sherehe iliyotarajiwa
kufanyika leo Jumatatu katika mji mkuu, Brasilia, kuadhimisha siku 500, kabla
ya kombe la dunia kungo'a nagna nchini humo mwaka ujao.
Mazishi
ya kwanza mjini Santa Maria yanatarajiwa kufanyika leo , kwa mujibu wa magazeti
ya nchi humo.
Maafisa
wa utawala wametoa majina ya waathiriwa hao,230 huku maiti watatu wakisalia
kutotambuliwa.
Kulingana
na taarifa za kituo cha televisheni cha Globo,wengi wa waathiriwa walikuwa kati
ya umri wa miaka16 na 20.
Zaidi ya
watu 100 wanapokea matibabu baada ya kushindwa kupumua kutokana na moshi
mkubwa.
No comments:
Post a Comment