Wednesday, November 29, 2017

Makamu wa rais wa Tanzania amtembelea Tundu Lissu Hospitalini Nairobi

Makamu wa Raisi wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan amemtembelea Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu ambaye amelazwa katika hospitali ya Nairobi ambapo anaendelea na Matibabu.Makamu wa Raisi alimtembelea Mbunge huyo wa Singida Mashariki  muda mfupi baada ya kuhudhuria kuapishwa kwa Raisi wa Taifa la Kenya Uhuru Kenyatta tarehe 28November 2017.

Mheshimiwa Lissu amekuwa akipata matibabu katika hospitali hiyo tangu Septemba 7 baada ya shambulio la kupigwa risasi na watu wasiojulikana katika jaribio la mauaji huko nyumbani kwake mjini Dodoma


No comments:

Post a Comment