![]() |
Rais wa Gambia Jammeh |
Rais wa
Gambia Yahya Jammeh ametoa amri kuwa wafanyikazi wote wa umma watafanya kazi
siku nne pekee kwa wiki kuanzia leo Ijumaa . Ijumaa sasa itakuwa siku ya
mapumziko sawa na Jumamosi na Jumapili.
Rais
Jammeh anasema iwapo wananchi wa Gambia watafanya kazi siku nne kwa wiki
watapata muda zaidi wa kusali, kushiriki maswala ya kijamii na kulima mashamba
yao.
Kwenye
taarifa amesema wananchi wa Gambia wanapaswa kurejea mashambani na kupanda
chakula na kuhakikisha wanakula chakula hicho ili taifa hilo liwe tajiri na
lenye afya.
Amesema
kuwa mishahara yao haitapunguzwa kwa sababu kwa siku hizo nne watu watafanya
kazi zaidi ya saa za kawaida ili kulipiza siku ya tano.
Shule za
kitaifa hazitafunguliwa tena siku ya ijumaa.Sekta za kibinafsi zitafanya kazi
hadi ijumaa lakini hazitaweza kufanya biashara yoyote na serikali siku hiyo.
Rais
Jammeh mwenye historia ya kuwa na tabia za kustaajabisha, hajawapa wananchi
Gambia muda wa kujiandaa kwa mfumo huo mpya.
Mwaka
2007 alitangaza kuwa anaweza kutibu ungonjwa wa Ukimwi kwa muda wa siku tatu
akitumia mchanganyiko wa dawa za kienyeji. Tamko hilo lililaaniwa na wataalam
wa matibabu kote duniani.
Pia
amekuwa akishtumiwa kwa ukiukaji wa haki za binadam.
Mwaka
jana wafungwa tisa waliokabiliwa na hukumu ya kifo walipigwa risasi na maafisa
wa polisi huku rais Jammeh akiapa kuwaua wafungwa wote waliohukumiwa kifo
katika muda wa wiki kadhaa. Baadaye alisimamisha mauaji hayo baada ya
kukosolewa vikali na jamii ya kimataifa.
No comments:
Post a Comment