Watafiti kutoka Uingereza na
Marekani wanasema kuwa mabadiliko ya hali ya hewa huenda yakazua ongezeko kubwa
la maambukizi ya ugonjwa wa Malaria kote duniani huku ugonjwa huo ukienea
katika maeneo ya milimani barani Afrika na Amerika ya Kusini.
Katika matokeo ya utafiti yaliyochapishwa
kwenye jarida la Science, wanasayansi hao wanasema hata ongezeko dogo katika
viwango vya joto siku za usoni huenda likaongeza kwa mamilioni maambukizi ya
malaria.
Mbu anayesababisha malaria.
Watafiti wamepata ushahidi kwamba mbu
anayebeba kimelea kinachosababisha malaria wanaelekea katika nyanda za juu
wakati viwango vya joto vikipanda.
Watu wanaoishi katika maeneo ya nyanda za juu
wanakosa kinga na hivyo kurahisisha maradhi ya malaria kuenea.
Takriban watu milioni mia mbili ishirini kote
duniani huambukizwa ukonjwa wa malaria.
Mbu aneyesababisha malaria
No comments:
Post a Comment