MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imesema ifikapo Desemba
31 mwaka huu, haitazima mitambo yote ya analojia kwenda dijitali na
badala yake, itazima mitambo hiyo kwa awamu katika mikoa kadhaa nchini.
Imesema imechukua uamuzi huo kwa kuzingatia
kuwa maeneo mengi nchini, hayajafikiwa na huduma ya digitali na kwamba
inatoa nafasi katika maeneo hayo, ili kufikia hatua hiyo kwanza.
No comments:
Post a Comment