MAHAKAMA Kuu kanda ya Dar es Salaam imebadilisha siku ya kusilizwa
kwa maombi ya dhamana ya Mwigizaji nyota wa filamu nchini, Elizabeth
Michael, maarufu kwa jina la Lulu,kutoka Ijumaa ya kesho hadi Juma tatu
ya January 28 mwaka huu.
Lulu anashtakiwa kwa kosa la kumuua aliyekuwa msanii mwenzake wa fani hiyo, Steven Kanumba, bila kukusudia.
Taarifa za ndani kutoka Mahakamani hapo zilizolifikia tovuti ya Habarimpya.com na
kudhibitishwa na vyanzo vya ndani kutoka Mahakamani hiyo zimedai kwamba
msanii huyo anaweza kupata dhamana hiyo na kurudi uraiani huku
akipangia tarehe nyingine ya kuwasilini Mahakamani hapo kwa ajili ya
kesi hiyo.
Awali Lulu alikuwa akikabiliwa na kosa la kuua kwa kukusudia, katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, lakini baada ya upelelezi kukamilika
alibadilishiwa mashtaka na kuwa ya kuua bila kukusudia, kisha kesi hiyo
ikahamishiwa Mahakakama Kuu.
No comments:
Post a Comment